Ado Shaibu amshtaki Rais Magufuli Mahakama Kuu kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

zitto anatafuta political mileage tu
Magufuli amebana kote,mara SGR,mara korosho mara stiglers gorge
Nasikia korosho zake nazo zimekumbwa na kile kimbunga cha kutaka kuona shamba lake! Kwani nasikia alinunua korosho nyingi sana huko mashambani kwa bei ya chini sana na kwa "kangomba" ili wakati wa msimu apige mahela! Mbinu hii alijifunza kutoka kwa yule rafiki yake na kigogo mmoja serikalini. Sasa wamepigwa - sijui BAO au CHINI!
 
Mimi siyo mwanasheria ila kama kweli yote uliyoyasema hapa yako kwenye Katiba, na kwamba sifa za weledi wa Mwanasheria Mkuu huyu ziko kama ulivyozitaja, then nadhani huko mbele ya safari inabidi tujaribu kuangalia uwezekano wa kuwa tuna-ammend baadhi ya vifungu vya Katiba yetu, kwa hati ya dharula kupitia Bunge. Hii itasaidia kuwalinda watu kama huyu, kwamba tunamhitaji sana lakini bahati mbaya Katiba inasema otherwise!

Hata mimi naona kuna haja ya kupunguza masharti ya sifa za mtu kushika madaraka katika utumishi wa serikali na utumishi wa umma hususani masharti yanayohusu uzoefu bila hivyo watu wenye weledi na ubobezi katika taalum mbalimbali watashindwa kulitumikia taifa katika nyazifa mbalimbali kama ambavyo tunaelekea kumkosa Dr. Kilangi, mwanasheria wenye weledi na ubobezi katika sheria za mafuta, gesi asilia na madini ambaye pia ni mwanataalum (academician) mzuri . Kwa mfano, kabla ya mwaka 2005, mwanasheria mkuu alitakiwa kuwa na uzoefu wa miaka 5 ya uwakili lakini leo katiba inataka uzoefu wa miaka 15, mara mbili ya zamani.
 
Hata mimi naona kuna haja ya kupunguza masharti ya sifa za mtu kushika madaraka katika utumishi wa serikali na utumishi wa umma hususani masharti yanayohusu uzoefu bila hivyo watu wenye weledi na ubobezi katika taalum mbalimbali watashindwa kulitumikia taifa katika nyazifa mbalimbali kama ambavyo tunaelekea kumkosa Dr. Kilangi, mwanasheria wenye weledi na ubobezi katika sheria za mafuta, gesi asilia na madini ambaye pia ni mwanataalum (academician) mzuri . Kwa mfano, kabla ya mwaka 2005, mwanasheria mkuu alitakiwa kuwa na uzoefu wa miaka 5 ya uwakili lakini leo katiba inataka uzoefu wa miaka 15, mara mbili ya zamani.

Halafu umeuona mwaka ambao hiyo sheria ilitungwa? Asilimia 75 ya waliomo humu JF walikuwa bado hawajazaliwa lakini yenyewe bado ipo na iko vile vile!
 
Mimi @AdoShaibu nimemwelekeza wakili wangu Fatma Karume ambaye ni wakili wa mahakama kuu, kufungua kesi mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kumshtaki Rais @MagufuliJP na Mwanasheria Mkuu kwa ajili ya kupinga uteuzi wa AG usiofuata masharti ya Katiba.


-----
KWANINI NIMEMSHTAKI RAIS MAGUFULI MAHAKAMA KUU KUPINGA UTEUZI WA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI?

Na Ado Shaibu

Jana tarehe 12 Desemba 2018 nilimwelekeza Mwanasheria Fatma Karume ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Lugango Kilangi.

Kwenye kesi hiyo, nimemwelekeza Wakili wangu kuwa Mdaiwa awe Ndugu John Pombe Magufuli na Ndugu Kilangi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali aunganishwe.

Kwa vile Wakili wangu amekwishaliingiza suala hili kwenye mchakato wa kimahakama, sitaingia kwenye kiini cha kesi na badala yake nitafafaua mambo mawili; msukumo uliosababisha kesi hii kufunguliwa na mbili, sababu za kumuunganisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Joseph Pombe Magufuli.

Nitayashughulikia masuala yote mawili kwa pamoja.

Kabla ya kuyashughulikia masuala hayo kwanza tutazame usuli wa suala lenyewe.

USULI (BACKGROUND) WA SUALA HILI

Tangu Dk. Kilangi ateuliwe na Rais kushika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mwezi Februari 2018, kumekuwepo na madai kwamba hayatimiza masharti ya kikatiba ya kushika nafasi hiyo.

Binafsi, kwa kutambua unyeti wa nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, sikuyachukulia madai hayo kuwa porojo linalostahili kupuuzwa au habari ya kawaida inayoweza kupita bila hatua yoyote kuchukuliwa. Niliamua kufanya utafiti wa kina kujiridhisha na madai hayo.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imempa Mwanasheria Mkuu wa Serikali madaraka makubwa. Yeye ndiye mshauri mkuu wa serikali kwenye masuala ya kisheria.

Hii ndio sababu katiba imeweka masharti maalum ya uteuzi wa mtu wa kushika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ibara ya 59 (2) imeweka masharti kuwa mtu anayeteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu ni lazima awe mtumishi wa umma mwenye sifa za kuwa wakili kwa miaka 15 mfululizo.

Utafiti wangu umebaini kuwa Dk. Kilangi amekuwa na sifa ya kuwa wakili kwa miaka saba tuu, chini ya hata nusu ya miaka iliyowekwa na katiba. Hana pia sifa ya kuwa mtumishi wa umma kwa miaka hiyo (
Rejea kiapo changu nilichoambatanisha kwenye andiko hili kujisomea zaidi)

MSUKUMO WA KESI

Binafsi, masuala matatu ndiyo yaliyonisukuma kwanza kupinga uteuzi wa Dk. Kilangi na pili kumjumuisha Rais Magufuli kwenye kesi hii.

1. Rais si Mfalme.

Zipo hisia potofu kwa baadhi ya watu kudhani kwamba Rais ni Mfalme. Watu wenye hisia hizi potofu hudhani kwamba Rais yupo juu ya sheria, hakosei na hapaswi kukosolewa.

Hisia hizi potofu zina mzizi wake wa kihistoria. Huko Ulaya enzi wa tawala za kifalme, iliaminika kwamba Mfalme ni mteule wa Mungu asiyeweza kufanya makosa. Hata Afrika ya kabla ya ukoloni, machifu walikuwa Alfa na Omega; mwanzo na mwisho.

Wakati wa ukoloni, Afrika ilikuwa chini ya udhibiti kijeshi, kisheria, kiuchumi na kisheria wa wakoloni walikuwa nchi za ng'ambo.

Mathalani, wakati wa ukoloni wa Uongereza, Tanganyika na Zanzibar yalikuwa makapu ya Malkia wa Uingereza kuchuma malighafi na rasilimali mbalimbali.

Mustakabali wa Afrika uliamuliwa ng'ambo. Kauli ya Malkia na serikali yake ilikuwa sawa na amri takatifu isiyoweza kupingwa.

Baada ya uhuru, Rais kwa katiba au utamaduni tuliourithi kutoka katika ukoloni, alikuwa na madaraka ya kifalme. Mwalimu Nyerere ameshawahi kusema katiba imempa madaraka yaliyopindukia.

Kwa yale madaraka ya kifame yanayotolewa na Katiba dawa yake ni kuendelea na mapambano ya kudai katiba mpya. Kwa yale ya utamaduni potofu, tunapaswa kuyaondoa kwa kuchukua hatua.

Kesi hii inalenga katika hilo la pili. Tunapaswa kuondosha utamaduni wa kufikiri kuwa Rais hawezi kugusika. Katiba ipo wazi kuwa Rais ni Mkuu wa nchi, Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa serikali.

Kwa maoni yangu, Katiba imempa kinga Rais dhidi ya masuala ya jinai na masuala ya madai ya kibinafsi. Kwa masuala mengine anayoyafanya kama Rais anaweza kuchukuliwa hatua. Kwa vile suala hili tunalifungua mahakamani, Mahakama yenyewe itaamua juu ya uhalali wake kisheria.

Iwapo suala lenyewe litafanikiwa, itamfanya Rais wa sasa na wa baadaye kuchukua kufanya teuzi na maamuzi mengine kwa umakini na kwa kuzingatia sheria kwa hofu ya masuala hayo kupingwa Mahakama.

2. Utii wa Katiba ni Wajibu wa Wote.

Ibara ya 26 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa wajibu kwa kila mtu kuheshimu katiba. Viongozi na wananchi sote tuna wajibu wa kuiheshimu na kuitii katiba.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano imeweka masharti kwenye uteuzi wa watu wa kushika baadhi ya ofisi nyeti. Kwa mfano, Rais hawezi kumteua mtu apendavyo kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka, Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali au Jaji bila kuzingatia masharti ya katiba.

Hivyobasi, Rais hakupaswa kumteua Ndugu Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati akifahamu kuwa mtu huyo hana sifa zilizowekwa na Katiba.

Dk. Kilangi naye hakupaswa pia kukubali kuteuliwa kushika nafasi ambayo hana sifa nayo. Alichopaswa kufanya ni kumshukuru Rais, kumweleza kuwa hawezi kushika nafasi hiyo kwa vile hana sifa na kumuomba Rais kumteua mtu mwingine. Hili lingemjengea heshima.

Haiwezekani mtu anayepaswa kuishauri serikali kufanya maamuzi yake kwa kuzingatia katiba huku yeye mwenyewe ameteuliwa kwa kuvunja katiba. HAIWEZEKANI.

Wakati tunaendelea na michakato ya kimahakama, Dk. Kilangi anaweza kulinda heshima yake kwa KUJIUZULU. Kwa kukosa sifa hawezi kumshauri Rais na Serikali kwa kujiamini huku akijua yeye mwenyewe hana sifa za kuwa Mwanasheria Mkuu.

3. Katiba ni Mali na Zao la Wananchi, Italindwa na Wananchi.

Kwenye petition yangu nimeeeka wazi kwamba mimi ni mwananchi na Kiongozi wa ACT Wazalendo. Kama mwananchi nina wajibu wa kuilinda na kuitetea katiba. Kama kiongozi wa chama cha siasa ninao wajibu wa kuitumia mahakama kama uwanja wa mapambano ya wanyonge na kupigania haki za binadamu na utawala wa sheria. Shauri hili linalenga kutekeleza wajibu wangu kama mwananchi na kama kiongozi wa chama.

Mahakama huamua kwa kupelekewa jambo. Nimechukua hatua hii kuitikia wito wa watetezi wa haki za binadamu kwa viongozi wa kisiasa kuitumia mahakama kupigania haki kwa kufanya mashtaka ya kimkakati (Strategic litigation).

Ado Shaibu,

Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi,
ACT Wazalendo.

View attachment 967124View attachment 967125View attachment 967126View attachment 967127View attachment 967128View attachment 967130View attachment 967131View attachment 967132View attachment 967133View attachment 967135
Mnatumia Akili kubwa kutatua tatizo dogo

Jinsi ya kutatua matatizo matatu ya Mwl. Nyerere (Ujinga, Umasikini na Maradhi) - JamiiForums
 
Nimepata habari kuwa Ndugu Ado Shaibu wa ACT-Wazalendo ametoa maelekezo kwa mwanasheria wake Bibi Fatma Karume kumfungulia mashtaka mahakamani mwanasheria mkuu wa Serikali Dr. Kilangi na Rais Magufuli kutokana na Rais kumteua Dr. Kilangi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati ambapo Dr. Kilangi ana sifa za kuwa mwanasheria mkuu.

Kwa mujibu wa Ibara ya 59 (2) ya katiba ya Tanzania, mtu anakuwa na sifa za kuwa mwanasheria mkuu wa serikali iwapo ana sifa zifuatazo;

(1) Ni mtumishi wa Umma mwenye sifa za kufanya kazi za wakili na amekuwa na sifa hii mfululizo kwa muda wa miaka 10.

(2) Ni wakili au mtu mwenye sifa za kuwa wakili na amekuwa na sifa hii mfululizo kwa muda wa miaka 10.

Swali ni je Dr. Kilangi ana sifa hizi? Kadri nijuavyo mimi ni kuwa Dr. Kilangi hana sifa hizi.

Kwanza, ukisoma wasifu (CV) ya Dr. Kilingi haioneshi mahala popote kuwa aliwahi kufanya kazi ya sheria katika utumishi wa umma ambayo inamfanya kuwa na sifa za kuwa wakili kama vile mwanasheria wa serikali, mwendesha mashtaka wa serikali au mwanasheria wa serikali za mitaa au kazi nyingine za sheria katika utumishi wa umma kama zilivyo tajwa na masharti ya kifungu cha 3 (2) cha sheria ya mawakili, Sura ya 341 au masharti ya Sheria ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (Kutimiza Majukumu), 2005 au Sheria ya huduma ya mashtaka ya taifa, 2008. Kutofanya kazi ya sheria katika utumishi wa umma moja kwa moja inamnyima Dr. Kilangi sifa ya kuwa na sifa hii kwa muda wa miaka 10 mfululizo. Mpaka hapo Dr. Kilangi ameshapoteza sifa ya kwanza ya kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Pili, kumbukumbu kutoka chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) zinaonesha kwamba Dr. Kilangi ni wakili mwenye Roll No. 2022 ambaye alipata uwakili tarehe 8 October 2011, hivyo bado Dr. Kilangi hajafikisha muda wa miaka 10 mfululizo tangia alipoapishwa kuwa wakili wa mahakama kuu na wakati anateuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali alikuwa bado hajafikisha miaka 10 mfululizo tangia amekuwa wakili.

Kutokana na maelezo haya ni wazi kabisa kuwa Dr. Kilangi hachomoki kwenye mtego huu labda kama atatawza kuchomokea kwenye sifa ya kwanza ya kufanya kazi ya sheria katika utumishi wa umma maana kwenye sifa hii sina ushahidi wa kutosha.

Kama huu ndo ukweli basi ni masikitiko yangu kwa taifa kumpoteza mwanasheria mkuu mbobezi katika sheria ya mafuta, gesi asilia na madini, mtu huyu tuna muitaji sana kulisaidia taifa katika sekta za mafuta, gesi asilia na madini, hivyo basi, ni imani yangu kuwa mhe. Rais atamteua kuwa mwanasheria kwenye nafasi nyingine katika sekta ya mafuta na gesi asilia au madini iwapo mahakama itaamua kuwa uteuzi wake kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ni batili.

Ushauri wangu kwa Mhe. Rais ni kuwa iwapo nafasi ya mwanasheria mkuu itabaki wazi basi kwa heshima na taadhima ninakushauri kuwa kwa mtizamo wangu watu wanao weza kuimudu nafasi ya mwanasheria mkuu wa serikali ni moja wapo katika ya watu (mawakili) watatu wafuatao;

(1) Francis Stolla (Rais mara 3 mfululizo wa TLS)

(2) Audax Kaendaguzi ( Mwandishi maarufu wa vitabu vya sheria na amicus curie wa mahakama ya rufaa)

(3) Dr. Onesmo Kyauke ( Mhadhiri wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam).

Sitataja au kueleza sifa za watu hawa maana Mhe Rais kwa kutumia vyombo vyake vya kimkakati ataweza kupata sifa za watu hawa.

Pia, Jaji Kiongozi, Dr. Feleshi anafaa kuwa mwanasheria mkuu lakini kwa wadhifa wake sio busara kumteua kuwa mwanasheria mkuu.

Ni hayo tu Mhe. Rais.

Asante kwa taarifa..
 
Back
Top Bottom