Ado Shaibu amshtaki Rais Magufuli Mahakama Kuu kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Sawa.....kuna kesi imefunguliwa juu ya hili... si ndio? Haki itatendeka...?
Ndio kuna kesi imefunguliwa juu ya swala hili. Swala la kwamba haki itatendeka siwezi kulisemea kwa sababu kipindi hiki uwezo wa kitaalum (uweledi), uadilifu na ujasiri wa majaji wa siku hizi unatiliwa shaka sana tofauti na majaji wa zamani kama Samatta, Lugakingira, Mwalusanya na Mapigano ambao walisifika kwa kutenda haki bila uoga na bila upendeleo kutoka na kuwa na uweledi, uadilifu na ujasiri usiotiliwa shaka hata kidogo.
 
Ina maana kwa sasa tunapaswa kuomba sana kwa Mungu, ndio pekee anaeweza kusaidia, au waonaje kiongozi....?

Mojawapo ya kanuni kuu ya utoaji haki ni kwamba uamuzi wa mahakama unapashwa kuwa predictable, uniform (uniformity) and consistent hususani kwa mawakili au wanasheria lakini kwa sasa ni vigumu sana ku predict uamuzi wa mahakama maana kila jaji anajiamulia kinachomuingia kichwani ndo maana kuna judgments na rulings nyingi za mahakama kuu na mahakama ya rufaa zinakinzana. Hivyo basi, swala la kupara haki mahakamani ni kwa kudra ya Mwenyazi Mungu. Siku hizi ni rahisi kupata haki kwa haraka na kwa ufanisi kwa Rais, waziri mkuu, waziri, mkuu wa mkoa, katibu mkuu, au mkuu wa wilaya kuliko mahakamani ndo maana Mhe. Makonda akitoa ofa ya kusaidia watu kwenye maswala ya utoaji haki upata maelfu ya watu, huu ni ushahidi kuwa watu wamepoteza imani kwa mahakama kwa sehemu kubwa.

Mimi ni mwanasheria na wakili lakini siamini kabisa kupata haki mahakamani.
 
Hili n eneo la watu "learned at law," msichokijua n kuwa Katba inamruhsu Rais "to dispense with, " hizo sifa "whenever he has reason to do so. "

Hili s eneo la mihemko... Soma uteuzi wa majaji!

Ndugu inaonesha hauko updated na mabadiliko ya katiba ya jamhuri, swala la Rais ku "dispense with" professional qualifications of attorney general liliondolewa na Ibara ya 11 ya Mabadiliko ya 14 ya Katiba ya mwaka 2005 (Sheria Na. 1 ya 2005) ambayo yalifuta Ibara ya 59 (2) ya Katiba iliyokuwepo kabla ya mwaka 2005 na kuweka maudhui mapya kwenye Ibara ya 59 (2) ya katiba ambapo rejea kwenye Ibara ya 109 (8) ya katiba iliondolewa au kufutwa kwenye Ibara ya 59 (2) ya katiba, hivyo, Rais alipokonywa mamlaka ya ku dispense with professional qualifications of attorney general kwa maana ya kwamba Rais alipokonywa au aliyang'anywa mamlaka ya kutengua sifa za kikatiba za mwanasheria mkuu wa serikali. Hatahivyo, Rais bado anayo mamlaka ya kutengua sifa za jaji wa mahakama kuu kuhusu muda wa uzoefu wa jaji wa mahakama kuu ambao unapashwa kuwa miaka 10 na anaweza kupunguza muda huu kadri atakavyoona inafaa lakini kwa kushauriana na tume ya utumishi wa mahakama.
 
si rahisi kuondolewa ktk hiyo nafasi kwasababu zilizotajwa hapo.
 
Hili mbona linajulikana kuwa sio rahisi kuondolewa katika nafasi husika lakini kama tuhuma hizo ni kweli basi zitamuondolea mwanasheria mkuu moral authority na kujiamini katika kutenda kazi zake, itakuwa ni moral defeat against AG.
 
Rais ana mamlaka ya ku dispense qualifications za majaji tu na hii ni kwa mujibu wa Ibara 109 (8) ya Katiba na Rais kamwe hana uwezo wa ku dispense qualifications za mwanasheria mkuu wa serikali na hakuna Ibara yoyote ya katiba inayompatia Rais mamlaka hayo.
Hajui kitu myinyi hata kwa majaji mlilishwa tango pori na Lissu mkaamini lakini kimyaa mpaka leo tena mmeletewa la AG nalo mnalishwa tango pori baada ya hapo kimyaa!! Wanatafuta kiki nyingine!! Yaani aliuewapa jina la mnyama wa serengeti anakipawa kizuri sana!
 
Kama unaweza badilisha katiba ili mwanasheria mkuu awe na sifa za kikatiba.
 
Nimepata habari kuwa Ndugu Ado Shaibu wa ACT-Wazalendo ametoa maelekezo kwa mwanasheria wake Bibi Fatma Karume kumfungulia mashtaka mahakamani mwanasheria mkuu wa Serikali Dr. Kilangi na Rais Magufuli kutokana na Rais kumteua Dr. Kilangi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati ambapo Dr. Kilangi ana sifa za kuwa mwanasheria mkuu.

Kwa mujibu wa Ibara ya 59 (2) ya katiba ya Tanzania, mtu anakuwa na sifa za kuwa mwanasheria mkuu wa serikali iwapo ana sifa zifuatazo;

(1) Ni mtumishi wa Umma mwenye sifa za kufanya kazi za wakili na amekuwa na sifa hii mfululizo kwa muda wa miaka 15.

(2) Ni wakili au mtu mwenye sifa za kuwa wakili na amekuwa na sifa hii mfululizo kwa muda wa miaka 15.

Swali ni je Dr. Kilangi ana sifa hizi? Kadri nijuavyo mimi ni kuwa Dr. Kilangi hana sifa hizi.

Kwanza, ukisoma wasifu (CV) ya Dr. Kilingi haioneshi mahala popote kuwa aliwahi kufanya kazi ya sheria katika utumishi wa umma ambayo inamfanya kuwa na sifa za kuwa wakili kama vile mwanasheria wa serikali, mwendesha mashtaka wa serikali au mwanasheria wa serikali za mitaa au kazi nyingine za sheria katika utumishi wa umma kama zilivyo tajwa na masharti ya kifungu cha 3 (2) cha sheria ya mawakili, Sura ya 341 au masharti ya Sheria ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (Kutimiza Majukumu), 2005 au Sheria ya huduma ya mashtaka ya taifa, 2008. Kutofanya kazi ya sheria katika utumishi wa umma moja kwa moja inamnyima Dr. Kilangi sifa ya kuwa na sifa hii kwa muda wa miaka 15 mfululizo. Mpaka hapo Dr. Kilangi ameshapoteza sifa ya kwanza ya kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Pili, kumbukumbu kutoka chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) zinaonesha kwamba Dr. Kilangi ni wakili mwenye Roll No. 2022 ambaye alipata uwakili tarehe 8 October 2011, hivyo bado Dr. Kilangi hajafikisha muda wa miaka 15 mfululizo tangia alipoapishwa kuwa wakili wa mahakama kuu na wakati anateuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali alikuwa bado hajafikisha miaka 15 mfululizo tangia amekuwa wakili.

Kutokana na maelezo haya ni wazi kabisa kuwa Dr. Kilangi hachomoki kwenye mtego huu labda kama atatawza kuchomokea kwenye sifa ya kwanza ya kufanya kazi ya sheria katika utumishi wa umma maana kwenye sifa hii sina ushahidi wa kutosha.

Kama huu ndo ukweli basi ni masikitiko yangu kwa taifa kumpoteza mwanasheria mkuu mbobezi katika sheria ya mafuta, gesi asilia na madini, mtu huyu tuna muitaji sana kulisaidia taifa katika sekta za mafuta, gesi asilia na madini, hivyo basi, ni imani yangu kuwa mhe. Rais atamteua kuwa mwanasheria kwenye nafasi nyingine katika sekta ya mafuta na gesi asilia au madini iwapo mahakama itaamua kuwa uteuzi wake kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ni batili.

Ushauri wangu kwa Mhe. Rais ni kuwa iwapo nafasi ya mwanasheria mkuu itabaki wazi basi kwa heshima na taadhima ninakushauri kuwa kwa mtizamo wangu watu wanao weza kuimudu nafasi ya mwanasheria mkuu wa serikali ni moja wapo katika ya watu (mawakili) watatu wafuatao;

(1) Francis Stolla (Rais mara 3 mfululizo wa TLS)

(2) Audax Kaendaguzi ( Mwandishi maarufu wa vitabu vya sheria na amicus curie wa mahakama ya rufaa)

(3) Dr. Onesmo Kyauke ( Mhadhiri wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam).

Sitataja au kueleza sifa za watu hawa maana Mhe Rais kwa kutumia vyombo vyake vya kimkakati ataweza kupata sifa za watu hawa.

Pia, Jaji Kiongozi, Dr. Feleshi anafaa kuwa mwanasheria mkuu lakini kwa wadhifa wake sio busara kumteua kuwa mwanasheria mkuu.

Ni hayo tu Mhe. Rais.

SHAHADA YA SHERIA (LL.B) PEKEE HAIMFANYI MTU KUWA NA SIFA ZA KUWA WAKILI.

Kuna wanasheria na wanasiasa hata raia wa kawaida wanaamini au kuaminishwa kuwa kupata shahada ya kwanza ya sheria (LL.B) pekee inamfanya mtu kuwa na "sifa za kuwa wakili" kwa minajiri ya kuteuliwa ya kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali. Watu wanaounga mkono hoja hii wanasema kuwa Dr. Kilangi alipata shahada ya kwanza ya sheria mwaka 2000 hivyo alikuwa na sifa za kuwa wakili kuanzia mwaka 2000, hii ikiwa na maana kwamba wakati anateuliwa kushika wadhifa wa mwanasheria mkuu tiyari alikuwa na zaidi ya miaka 15 akiwa na sifa za kuwa wakili. Wapinzani wa hoja hii wanasema kuwa Dr. Kilangi alipata sifa za kuwa wakili baada ya kufaulu bar examinations chini ya Baraza la Elimu ya sheria na kuwa wakili mwaka 2011 hivyo bado hajafikisha miaka 15 ya uwakili au ya kuwa na sifa za kuwa wakili. Maoni yangu kuhusu swala la shahada ya kwanza ya sheria kumpa mtu sifa za kuwa wakili ni kama ifuatavyo;

Ibara ya 59 (2) ya katiba imeweka masharti kuwa ili mtu ateulie kuwa mawanasheria mkuu wa serikali lazima awe "wakili" au awe na "sifa za kuwa wakili". Swala la kuwa "wakili" halina utata liko wazi mno na aliitaji mjadala kabisa na swala lenye utata ni mtu mwenye "sifa za kuwa wakili". Mtu mwenye shahada ya kwanza ya sheria hana kabisa "sifa za kuwa wakili" kwa sababu sheria mbili zinataja kwa uwazi mtu mwenye sifa za kuwa wakili. Sheria zimeweka aina tano (5) za watu wenye sifa za kuwa wakili kama ifuatavyo;

Kwanza, "mtu mwenye Post-Graduate Diploma in Legal Practice" ambayo imetolewa na Law School of Tanzania ana sifa za kuwa wakili, hii ni kwa mujibu wa section 12 (3) of the Law School of Tanzania Act, 2007 (sheria Na. 18 ya 2007). Na mtu kamwe hawezi kupata Post-Graduate Diploma in Legal Practice" ambayo imetolewa na Law School of Tanzania mpaka awe na shahada ya sheria au sifa zingine za kitaalum ambazo zinatambuliwa na Baraza la Elimu ya Sheria (Council for Legal Education), hii ni kwa mujibu wa section 11 (1) (a) and (b) of the Law School of Tanzania Act, 2007

Pili, mtu ambaye ana shahada ya sheria ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki au chuo kikuu chochote ambacho kinatambuliwa na Baraza la Elimu ya Sheria na awe amefauli "Bar examinations" inayosimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria , na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (i) and (b) (i) of the Advocate Act, Cap. 1.

Tatu, Mtu ambaye amekuwa wakili Zanziba, Kenya na Uganda kwa kipindi cha miaka 5 kabla ya siku ya kufanya maombi ya kuwa wakili, na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (i) and (b) (i) of the Advocate Act, Cap. 1.

Nne, mtu ambaye ni wakili wa mahaka zisizokuwa na mipaka ya mamlaka katika maswala ya jinai na madai katika nchi za jumuia ya madola au nchi nyingine zilizoteuliwa na waziri wa sheria kwa ajiri hiyo, na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (ii) of the Advocate Act, Cap. 1.

Tano, mtu ambaye ni solisita (solicitor) wa mahakama ya juu ya Uingereza (England), Northern Ireland, Jamhuri ya Ireland na Scotland (United Kingdom).

Hivyo basi, hitimisho langu ni kuwa mtu mwenye shahada ya sheria (LL.B) kamwe hawezi kuwa na sifa za kuwa wakili mpaka apate Post-Graduate Diploma in Legal Practice Kutoka Law School of Tanzania au afaulu mitihani inayosimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria (Council for Legal Education) au awe amekuwa wakili au solisita katika nchi za jumuia ya madola au awe amekuwa wakili katika Kenya, Zanzibar na Uganda kwa kipindi cha miaka mitano.
Mheshimiwa Rais kama unaiona hii post yangu pengine umepata nafasi ya kuutazama huu uzi (thread).Mimi naokuomba kama kuna ukweli katika hili pia ufyekelee haya ma-vigezo vikwazo kwa watu kupata ajira na kutumikia taifa,kila siku vijana hawapati kazi eti kisa uzoefu.Wazoefu wengine ndio hao wameiba wamefanya madudu,tafadhali endelea kutazama wapya katika kila sekta..Mtu akishindwa kumudu anatumbuliwa tu!
Lakini Baba yetu Magufuli
tunakuomba tukumbuke vijana wako toka vyuo vikuu tumechoka kukaa Nyumbani haya mauzoefu yanatuua kimya kimya..Mungu akusaidie katika utekelezaji wa majukumu yako.
 
Wakuu mbona naona kama address ya mshitakiwa namba moja haijakaaa sawa? Hii haiwezi kuleta shida kwenye mashtaka?
1545194873293.png
 
Elewa kwamba kama hii kesi itaanguka mbele ya mahakama za CCM, ikipelekwa The Hague, dikteta hachomoi!
 
Tundu Lissu ni mwanadamu wa kawaida kama ulivyo wewe na mimi, kwa mantiki hiyo hawezi kujua kila kitu.
Kweli kabisa, pamoja na uwezo wake mkubwa wa kiakili na uweledi mkubwa wa maswala ya kisheria bado Tundu Lissu hawezi jua kila kitu.
 
Ndugu inaonesha hauko updated na mabadiliko ya katiba ya jamhuri, swala la Rais ku "dispense with" professional qualifications of attorney general liliondolewa na Ibara ya 11 ya Mabadiliko ya 14 ya Katiba ya mwaka 2005 (Sheria Na. 1 ya 2005) ambayo yalifuta Ibara ya 59 (2) ya Katiba iliyokuwepo kabla ya mwaka 2005 na kuweka maudhui mapya kwenye Ibara ya 59 (2) ya katiba ambapo rejea kwenye Ibara ya 109 (8) ya katiba iliondolewa au kufutwa kwenye Ibara ya 59 (2) ya katiba, hivyo, Rais alipokonywa mamlaka ya ku dispense with professional qualifications of attorney general kwa maana ya kwamba Rais alipokonywa au aliyang'anywa mamlaka ya kutengua sifa za kikatiba za mwanasheria mkuu wa serikali. Hatahivyo, Rais bado anayo mamlaka ya kutengua sifa za jaji wa mahakama kuu kuhusu muda wa uzoefu wa jaji wa mahakama kuu ambao unapashwa kuwa miaka 10 na anaweza kupunguza muda huu kadri atakavyoona inafaa lakini kwa kushauriana na tume ya utumishi wa mahakama.
Well argued, as the AG is well qualified!
 
Nimepata habari kuwa Ndugu Ado Shaibu wa ACT-Wazalendo ametoa maelekezo kwa mwanasheria wake Bibi Fatma Karume kumfungulia mashtaka mahakamani mwanasheria mkuu wa Serikali Dr. Kilangi na Rais Magufuli kutokana na Rais kumteua Dr. Kilangi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati ambapo Dr. Kilangi hana sifa za kuwa mwanasheria mkuu.

Kwa mujibu wa Ibara ya 59 (2) ya katiba ya Tanzania, mtu anakuwa na sifa za kuwa mwanasheria mkuu wa serikali iwapo ana sifa zifuatazo;

(1) Ni mtumishi wa Umma mwenye sifa za kufanya kazi za wakili na amekuwa na sifa hii mfululizo kwa muda wa miaka 15.

(2) Ni wakili au mtu mwenye sifa za kuwa wakili na amekuwa na sifa hii mfululizo kwa muda wa miaka 15.

Swali ni je Dr. Kilangi ana sifa hizi? Kadri nijuavyo mimi ni kuwa Dr. Kilangi hana sifa hizi.

Kwanza, ukisoma wasifu (CV) ya Dr. Kilingi haioneshi mahala popote kuwa aliwahi kufanya kazi ya sheria katika utumishi wa umma ambayo inamfanya kuwa na sifa za kuwa wakili kama vile mwanasheria wa serikali, mwendesha mashtaka wa serikali au mwanasheria wa serikali za mitaa au kazi nyingine za sheria katika utumishi wa umma kama zilivyo tajwa na masharti ya kifungu cha 3 (2) cha sheria ya mawakili, Sura ya 341 au masharti ya Sheria ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (Kutimiza Majukumu), 2005 au Sheria ya huduma ya mashtaka ya taifa, 2008. Kutofanya kazi ya sheria katika utumishi wa umma moja kwa moja inamnyima Dr. Kilangi sifa ya kuwa na sifa hii kwa muda wa miaka 15 mfululizo. Mpaka hapo Dr. Kilangi ameshapoteza sifa ya kwanza ya kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Pili, kumbukumbu kutoka chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) zinaonesha kwamba Dr. Kilangi ni wakili mwenye Roll No. 2022 ambaye alipata uwakili tarehe 8 October 2011, hivyo bado Dr. Kilangi hajafikisha muda wa miaka 15 mfululizo tangia alipoapishwa kuwa wakili wa mahakama kuu na wakati anateuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali alikuwa bado hajafikisha miaka 15 mfululizo tangia amekuwa wakili.

Kutokana na maelezo haya ni wazi kabisa kuwa Dr. Kilangi hachomoki kwenye mtego huu labda tu kama ataweza kuchomokea kwenye sifa ya kwanza ya kufanya kazi ya sheria katika utumishi wa umma maana kwenye sifa hii sina ushahidi wa kutosha.

Kama huu ndo ukweli basi ni masikitiko yangu kwa taifa kumpoteza mwanasheria mkuu mbobezi katika sheria ya mafuta, gesi asilia na madini, mtu huyu tuna muitaji sana kulisaidia taifa katika sekta za mafuta, gesi asilia na madini, hivyo basi, ni imani yangu kuwa mhe. Rais atamteua kuwa mwanasheria kwenye nafasi nyingine katika sekta ya mafuta na gesi asilia au madini iwapo mahakama itaamua kuwa uteuzi wake kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ni batili.

Ushauri wangu kwa Mhe. Rais ni kuwa iwapo nafasi ya mwanasheria mkuu itabaki wazi basi kwa heshima na taadhima ninakushauri kuwa kwa mtizamo wangu watu wanao weza kuimudu nafasi ya mwanasheria mkuu wa serikali ni moja wapo katika ya watu (mawakili) watatu wafuatao;

(1) Francis Stolla (Rais mara 3 mfululizo wa TLS)

(2) Audax Kaendaguzi ( Mwandishi maarufu wa vitabu vya sheria na amicus curie wa mahakama ya rufaa)

(3) Dr. Onesmo Kyauke ( Mhadhiri wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam).

Sitataja au kueleza sifa za watu hawa maana Mhe Rais kwa kutumia vyombo vyake vya kimkakati ataweza kupata sifa za watu hawa.

Pia, Jaji Kiongozi, Dr. Feleshi anafaa kuwa mwanasheria mkuu lakini kwa wadhifa wake sio busara kumteua kuwa mwanasheria mkuu.

Ni hayo tu Mhe. Rais.

SHAHADA YA SHERIA (LL.B) PEKEE HAIMFANYI MTU KUWA NA SIFA ZA KUWA WAKILI.

Kuna wanasheria na wanasiasa hata raia wa kawaida wanaamini au kuaminishwa kuwa kupata shahada ya kwanza ya sheria (LL.B) pekee inamfanya mtu kuwa na "sifa za kuwa wakili" kwa minajiri ya kuteuliwa ya kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali. Watu wanaounga mkono hoja hii wanasema kuwa Dr. Kilangi alipata shahada ya kwanza ya sheria mwaka 2000 hivyo alikuwa na sifa za kuwa wakili kuanzia mwaka 2000, hii ikiwa na maana kwamba wakati anateuliwa kushika wadhifa wa mwanasheria mkuu tiyari alikuwa na zaidi ya miaka 15 akiwa na sifa za kuwa wakili. Wapinzani wa hoja hii wanasema kuwa Dr. Kilangi alipata sifa za kuwa wakili baada ya kufaulu bar examinations chini ya Baraza la Elimu ya sheria na kuwa wakili mwaka 2011 hivyo bado hajafikisha miaka 15 ya uwakili au ya kuwa na sifa za kuwa wakili. Maoni yangu kuhusu swala la shahada ya kwanza ya sheria kumpa mtu sifa za kuwa wakili ni kama ifuatavyo;

Ibara ya 59 (2) ya katiba imeweka masharti kuwa ili mtu ateulie kuwa mawanasheria mkuu wa serikali lazima awe "wakili" au awe na "sifa za kuwa wakili". Swala la kuwa "wakili" halina utata liko wazi mno na haliitaji mjadala kabisa na swala lenye utata ni mtu mwenye "sifa za kuwa wakili". Mtu mwenye shahada ya kwanza ya sheria hana kabisa "sifa za kuwa wakili" kwa sababu sheria mbili zinataja kwa uwazi mtu mwenye sifa za kuwa wakili. Sheria zimeweka aina tano (5) za watu wenye sifa za kuwa wakili kama ifuatavyo;

Kwanza, "mtu mwenye Post-Graduate Diploma in Legal Practice" ambayo imetolewa na Law School of Tanzania ana sifa za kuwa wakili, hii ni kwa mujibu wa section 12 (3) of the Law School of Tanzania Act, 2007 (sheria Na. 18 ya 2007). Na mtu kamwe hawezi kupata Post-Graduate Diploma in Legal Practice" ambayo imetolewa na Law School of Tanzania mpaka awe na shahada ya sheria au sifa zingine za kitaalum ambazo zinatambuliwa na Baraza la Elimu ya Sheria (Council for Legal Education), hii ni kwa mujibu wa section 11 (1) (a) and (b) of the Law School of Tanzania Act, 2007

Pili, mtu ambaye ana shahada ya sheria ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki au chuo kikuu chochote ambacho kinatambuliwa na Baraza la Elimu ya Sheria na awe amefauli "Bar examinations" inayosimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria , na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (i) and (b) (i) of the Advocate Act, Cap. 1.

Tatu, Mtu ambaye amekuwa wakili Zanziba, Kenya na Uganda kwa kipindi cha miaka 5 kabla ya siku ya kufanya maombi ya kuwa wakili, na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (i) and (b) (i) of the Advocate Act, Cap. 1.

Nne, mtu ambaye ni wakili wa mahaka zisizokuwa na mipaka ya mamlaka katika maswala ya jinai na madai katika nchi za jumuia ya madola au nchi nyingine zilizoteuliwa na waziri wa sheria kwa ajiri hiyo, na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (ii) of the Advocate Act, Cap. 1.

Tano, mtu ambaye ni solisita (solicitor) wa mahakama ya juu ya Uingereza (England), Northern Ireland, Jamhuri ya Ireland na Scotland (United Kingdom).

Hivyo basi, hitimisho langu ni kuwa mtu mwenye shahada ya sheria (LL.B) kamwe hawezi kuwa na sifa za kuwa wakili mpaka apate Post-Graduate Diploma in Legal Practice Kutoka Law School of Tanzania au afaulu mitihani inayosimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria (Council for Legal Education) au awe amekuwa wakili au solisita katika nchi za jumuia ya madola au awe amekuwa wakili katika Kenya, Zanzibar na Uganda kwa kipindi cha miaka mitano.

Mimi siyo mwanasheria ila kama kweli yote uliyoyasema hapa yako kwenye Katiba, na kwamba sifa za weledi wa Mwanasheria Mkuu huyu ziko kama ulivyozitaja, then nadhani huko mbele ya safari inabidi tujaribu kuangalia uwezekano wa kuwa tuna-ammend baadhi ya vifungu vya Katiba yetu, kwa hati ya dharula kupitia Bunge. Hii itasaidia kuwalinda watu kama huyu, kwamba tunamhitaji sana lakini bahati mbaya Katiba inasema otherwise!
 
Back
Top Bottom