PreGE2025 Ado Shaibu ajitosa Ubunge Tunduru Kaskazini

PreGE2025 Ado Shaibu ajitosa Ubunge Tunduru Kaskazini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,820
Reaction score
15,049
ADO SHAIBU AJITOSA UBUNGE TUNDURU KASKAZINI

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa ubunge katika Jimbo la Tunduru Kaskazini kupitia ACT Wazalendo. Amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Jimbo hilo Ndugu Noel Chilemba katika Ofisi ya Jimbo leo tarehe 26 Aprili 2025.
WhatsApp Image 2025-04-26 at 12.58.20_2e901522.jpg

WhatsApp Image 2025-04-26 at 12.58.19_ae57c51f.jpg

WhatsApp Image 2025-04-26 at 12.58.20_d81dfd44.jpg
 
Omba omba kupewa Hela kama habadili mtizamo siku zote ataendelea kuwa ombaomba!

Kuingia kwenye uchaguzi huku anayeamua ushindi ni unayetakiwa kumpinga, hiyo ni tabia za omba omba!
 
Omba omba kupewa Hela kama habadili mtizamo siku zote ataendelea kuwa ombaomba!

Kuingia kwenye uchaguzi huku anayeamua ushindi ni unayetakiwa kumpinga, hiyo ni tabia za omba omba!
Lazima wataingizwa kama wabunge kadhaa wa upinzani,ili kuonyesha watu walichagua,kwa hali hiyo anaweza kuingia.
 
Omba omba kupewa Hela kama habadili mtizamo siku zote ataendelea kuwa ombaomba!

Kuingia kwenye uchaguzi huku anayeamua ushindi ni unayetakiwa kumpinga, hiyo ni tabia za omba omba!
Ahahahahaha! Kuna chama ombaomba zaidi ya Chadema duniani? Au ndio mambo ya "Nyani haoni kundule!!" Ahahahahaha!!
 
Ishajulikana. Na katika vitu anavitamani Zitto ni kuwa kiongozi wa upinzania bungeni.

Kwa CCM ya Sasa wao na ACT ni kulwa na doto lao ni moja dhidi ya CHADEMA.
Ndo iko hivyo,ZZK wala vyama vingine ukiacha CHADEMA, hawana kingine,wao ni maopotyunisti.
 
ACT sehemu zote wanazokubalika watashinda!! Ni ushindi nwa kimkakati kuifanya ACT kuwa Cha KIKUU Cha upinzani bungeni!!
 
Omba omba kupewa Hela kama habadili mtizamo siku zote ataendelea kuwa ombaomba!

Kuingia kwenye uchaguzi huku anayeamua ushindi ni unayetakiwa kumpinga, hiyo ni tabia za omba omba!
Makasiriko ya nini, unataka agombee tundu Lissu tuu wakigombea wengine mnawakashfu.
Heshimuni maamuzi ya wengine wewe endelea kufuata upepo.
 
Lazima wataingizwa kama wabunge kadhaa wa upinzani,ili kuonyesha watu walichagua,kwa hali hiyo anaweza kuingia.
Uko sahihi, kama walivyokomaa Covid 19 kubaki, hii zamu ya wengine.
 
ACT inaenda kunufaika kwa bifu la CHADEMA na CCM. Watapata wabunge na madiwani wawili watatu dunia izugwe kuwa uchaguzi ulikuwa huru na haki. Mind kuwa ACT ni washirika wa serikali kule Zanzibar, kwa hiyo CCM haitamtosa mshirika wake, itamuachia majimbo na kata kadhaa angalau ACT ipate ushindi wa asilimia kadhaa mzani ukae sawa, hii haitaji hata D moja ya darasa la nne kung'amua mchezo huo wa kisiasa. Kuna lile genge la G55 la chadema nalo wakifanikiwa kulisimika mulemule ndani ya chadema likagombea nalo linaweza kupata majimbo kadhaa na mwisho kabisa mshua wa no reform no election wanaweza wakamuachia baada ya uchaguzi kupita, hoja yake itakuwa imepungua makali kwa sababu uchaguzi utakuwa umepita na huko mbeleni kutakuwa na muda mrefu wa kufanya reforms akaambiwa haya sasa na tufanye hiyo reform
 
Dhana ya uwakilishi wa wananchi imekuwa ya ovyo sana, ni kuhusu mafao zaidi kuliko mwananchi, ndio maana wakifika bungeni sauti zao zinabadlika, wao ni kuimba kwaya, makofi na vigelegele kwa Serikali.
 
Back
Top Bottom