Vicin
JF-Expert Member
- Jul 19, 2017
- 676
- 295
Habarini wadau.
Mimi ni mmojawapo wa waombaji wa vyuo mwaka huu, ila kutokea kipindi tumetuma maombi hadi kukaribia selection kutoka mawazo yanatawala kichwani ukizingatia na hali ya maisha ilivyo ongezea na kwamba tumeshasugua mno mtaani.
Dalili mojawapo ya stress ni kukosa usingizi, kuchelewa kupata usingizi, kulala kupita kawaida yako kama ulikuwa unaamka saa 12 asubuhi, unajikuta unaamka saa 2 asubuhi, usingizi kukatika usiku wa manane........
Namshukuru Mungu mimi nimepata chuo.
Ushauri wangu kwa ambao hawajapata na wanaomba second admission. Fanya application mapema, kuwa makini katika machaguo kwani vyuo vinachukua ufaulu wa juu kwa baadhi ya course kuliko kawaida, usione chuo kimeandika pointi zake ni kiasi flani ukajua ukiomba utakuwa umekidhi vigezo!!!!!! Matokeo ya mwaka huu kuna one kibao ndio maana wengi wenye two na one za mwishoni walioomba course zenye pointi kubwa wamekosa. Kwa mfano, ukiwa na one ya 5 udsm unaweza ukaomba llb (Law) au petroleum and gas ukatemwa, chagua course kwa umakini upate chuo kwanza, course utaenda kuhama kama pointi zinaruhusu na nafasi ipo.
Nasema hivyo kwasababu ukiwa una ufaulu mzuri halafu ukakosa chuo ndio mpaka mwakani tena, na je! unahisi mwakani watashusha pointi!
Ukibaki mtaani ni dhahiri utapotea usipokuwa makini.
Epuka hizo stress. Kama una pointi za kupata chuo make sure unaomba upate chuo kwanza.
Ukishakamilisha maombi ya chuo, kamwombe Mungu wako, kisha nenda kaangalie mpira, muvi........
Nawatakieni kila la kheri na jumapili yenye baraka tele. Mungu awajalie.