Admission za vyuo mwaka huu ni chanzo cha stress. Caveat emptor.

Vicin

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
676
295
Habarini wadau.
Mimi ni mmojawapo wa waombaji wa vyuo mwaka huu, ila kutokea kipindi tumetuma maombi hadi kukaribia selection kutoka mawazo yanatawala kichwani ukizingatia na hali ya maisha ilivyo ongezea na kwamba tumeshasugua mno mtaani.
Dalili mojawapo ya stress ni kukosa usingizi, kuchelewa kupata usingizi, kulala kupita kawaida yako kama ulikuwa unaamka saa 12 asubuhi, unajikuta unaamka saa 2 asubuhi, usingizi kukatika usiku wa manane........
Namshukuru Mungu mimi nimepata chuo.

Ushauri wangu kwa ambao hawajapata na wanaomba second admission. Fanya application mapema, kuwa makini katika machaguo kwani vyuo vinachukua ufaulu wa juu kwa baadhi ya course kuliko kawaida, usione chuo kimeandika pointi zake ni kiasi flani ukajua ukiomba utakuwa umekidhi vigezo!!!!!! Matokeo ya mwaka huu kuna one kibao ndio maana wengi wenye two na one za mwishoni walioomba course zenye pointi kubwa wamekosa. Kwa mfano, ukiwa na one ya 5 udsm unaweza ukaomba llb (Law) au petroleum and gas ukatemwa, chagua course kwa umakini upate chuo kwanza, course utaenda kuhama kama pointi zinaruhusu na nafasi ipo.
Nasema hivyo kwasababu ukiwa una ufaulu mzuri halafu ukakosa chuo ndio mpaka mwakani tena, na je! unahisi mwakani watashusha pointi!
Ukibaki mtaani ni dhahiri utapotea usipokuwa makini.
Epuka hizo stress. Kama una pointi za kupata chuo make sure unaomba upate chuo kwanza.
Ukishakamilisha maombi ya chuo, kamwombe Mungu wako, kisha nenda kaangalie mpira, muvi........
Nawatakieni kila la kheri na jumapili yenye baraka tele. Mungu awajalie.
 
Ndio yale ya kusoma course yoyote ilimradi tu hata kama sio anachokipenda....ila ndio Tz na elimu yetu
 
Aisee poleni wadogo zangu kumbe mambo yamekua magumu namna hiyo
Asante.
Mambo magumu, mtu unawaza chuo, na hujui mkopo kama utapata. Maana hali ilivyo mtaani saivi hakueleweki ada na maisha ya chuo tatizo lingine.
 
Ndio muone umuhimu wa Central Admission System.....Ile System ilikuwa nzuri sana maana unakuwa na uhakika wa Course uliyoomba kupata ila Chuo ni tofauti...

Huu usumbufu walioufanya lazima watairudisha CAS
 
Ikumbukwe kwamba
kama umemaliza form six kuna wenzako wenye div 3 wanatamani wapate chuo hata ingekuwa ni barchelor of cocroach, we una vigezo vya kwenda chuo ila unasema unaangalia unachopenda, sijui professional, sijui nataka kuwa flani,
kama umetoka diploma kumbuka kuwa kuna watu wenye GPA ya 2.9 wanatamani wapate mpenyo ila system imebana. Usiangalie unataka kuwa nani, angalia wamekufanya uwe nani,,, course ambazo zinaandaa watu kuajiriwa ila kuna watu wengi waliopo mtaani, asilimia kubwa zimekaza, course ambazo zinakuandaa kujiajiri ndio afadhali kidogo.
 
Pole Sana Ndugu Zangu Mimi Namshukuru Mungu Nimepata Chuo Kwa Course Nilizozipa Chaguo La Kwanza Ila Wanachukua Ufaulu Mkubwa Sana
 
Ndio muone umuhimu wa Central Admission System.....Ile System ilikuwa nzuri sana maana unakuwa na uhakika wa Course uliyoomba kupata ila Chuo ni tofauti...

Huu usumbufu walioufanya lazima watairudisha CAS
Mimi nilikosa kwa mfumo huo huo wa CAS na nilikua na ufauru mzuri tu je unahisi ule mfumo nntauona mzuri? lkn mwaka huu nimepata UDSM NA SUA,nanawajua wengi sana walokosa mwaka Jana na mwaka huu wamepata,apo inshu sio mfumo bali ni ufauru kuwa mkubwa ulopelekea competition kuwa kubwa,japo hakuna kinachokosa kasoro kwa mfumo huu wa sasa wakiweza kudhibiti hii inshu ya multiple selection basi utazidi kuwa bora,
 
Kwakwel mungu asaidue maana hata ss tuliopata bado safar ni ndefu!!!! Aya mambo ya kukonfirm kwakwel hayatup huhakika
Ukiconfirm vyuo viwili ndio shida. Tumia busara uconfirm kimoja. Upate na mwenzako apate.
 
Back
Top Bottom