Adhabu za Wanafunzi Juma Nature alituonya

The Tomorrow People

JF-Expert Member
Jul 11, 2013
2,662
2,745
Wanabodi habari,
Baada ya lile sakata la Mbeya Day mengi yameongelewa. Ingawa mateso ya wanafunzi ni yamuda mrefu, mara chache hatua zimechukuliwa.

Leo tujikumbushe wimbo wa Juma Nature-Kigetogeto, juu ya mateso ya wanafunzi...

"....Tunatahabika kusoma hatutaki tumeghairi, kwa maana haya maticha yanausongo sio siri,

Yasije yakatufumua watoto wa watu bure, tukajalipa kisasi tukaonekana majambazi,

......Vulugu asababishe aliye leta soo, shule tumekuja kusoma au kupewa adhabu za vyoo. Hata nibanwe vipi na haja sijisaidii ng'oo.

Mwalimu hawa wasalimu vijana ndio tutakubariki? Kama mtanashati mwenye mapene ya kigiriki acha stiki.

Sakata laisha mseto, ukitumaindi sana ndio vile kigeto geto.

Haiwezekani ulete masuala ya ubaguzi, hu wakati si wakuleteana makuzi wala upuuuzi, chonga lako usifuate ambalo si lako,

Wengine watu wa gheto wanaweza kukuminyia mkong'oto uone chungu ya mwaka wasela wako tuone taka...kwani si ujinga tunataka.

Sasa kusoma baaaas, si afadhali daftari niende kutungia vesi, maana nashangaa mwalimu akija kila swali naulizwa mimi tuuu kwani mi ndio nani wengine huwaoni.

Unatutafuta sababu usiongopee watu, biashara faida juu yenu mnatutuma sisi. Mmekatwa hamba miguuu?

Iweje una mtoto umtese kama mnyama au mwanga? Au unatafuta tufe tu ukusanye michango?

Stiki sio kuonya, kufunza ni kubuzwa tuuuu, au unaniambia nini unasemaje??

.....wenzetu kusoma starehe huku kwetu mauaji, hebu jijaribu wewe mwanafunzi akuchape fimbo, yaalaaaaa, utasema inaukweli hii nyimbo.

Wengine mnatusononesha hamjui kusomesha, wengine hatupandishi hata kama tuna kesha."

Juma Nature aliona mbali, na hii ndio hali halisi ya shule zetu. Hatua stahiki zichukuliwe.
 
Juzi nimepanda kwenye daladala na hao wanafunzi wa Mbeya day jamani ni shidaaa.....kwanza wanaenda shule saa 2 pili hawana adabu kabisaa tupo kwenye gari tumejaa watu wazima lakini wanavyoongeaaa sasaaa.....baadaye mwingine kachukua simu anawasiliana na kiboy friend chakee....yaaani mpaka wale watoto wanashuka ujenzii nliwaangalia nkashindwa hata kuwamalizaa
 
Juzi nimepanda kwenye daladala na hao wanafunzi wa Mbeya day jamani ni shidaaa.....kwanza wanaenda shule saa 2 pili hawana adabu kabisaa tupo kwenye gari tumejaa watu wazima lakini wanavyoongeaaa sasaaa.....baadaye mwingine kachukua simu anawasiliana na kiboy friend chakee....yaaani mpaka wale watoto wanashuka ujenzii nliwaangalia nkashindwa hata kuwamalizaa
Naona hata mkuu wa mkoa alisema hao washa pinda
 
Inafika kipindi mwalimu unakasirika unawaadhibu kwa hasira yanakukuta ya kina Msigwa kila mtu anakuona mbaya.....ila kiukweli wale wanafunzi wanakeraa yaani nliwaonea huruma sana wazazi wao....
Si mbaya kwa kuwa like tukio tulishabikia sana bila kuchunguza kwa undani, wacha tuvune mabua
 
1477327755943.png
Sir Nature moja ya wasanii nnaowakubali nchini mwetu hivi umewahi kusikia ile nyimbo ya dogo....totoidi?
 
Back
Top Bottom