Adhabu ya "Summary Dismissal" kwa kutokuonekana kazini haiwahusu viongozi?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,801
71,225
Tunafahamu kuwa watumishi wote wa Umma ambao ni Viongozi na wapo Madarakani kwa kupigiwa kura (kupitia uchaguzi) waajiri wao na mabosi wao ni sie Wapiga kura wananchi wa nchi hii.

Sheria za kazi na mahusiano kazini zinatamka kuwa Mtumishi asipohudhuria zaidi ya siku 3 mfululizo na bila taarifa yeyote kifuatacho ni kufukuzwa kazi moja kwa moja naMwajiri wake!

Sasa inakuwaje kuna viongozi wanakosekana kazini zaidi ya mwezi na hakuna taarifa nasi kama waajiri tuko kimya kiasi eti mtumishi huyo anarudi toka mafichoni kisha anamfokea mwajiri kwa kuulizauliza aliko?

Au sheria hiyo haiwahusu viongozi wa kuchaguliwa? Kwamba anaweza kuchaguliwa 2025 kisha akaondoka kuishi Ukraine kulima ngano na kurudi 2029 karibu na uchaguzi na tusiulize? Au tukiuliza tunaambiwa tutashughulikiwa huku tukifokewa?
 
Hii nchi ngumu sana Kaka, kuna siku itatokea top officials wote hawapo na hakuna kitakachotokea, mark my word.
 
Ukiijua nafasi yako hutouliza hayo maswali Mkuu.

Wewe ni Mwananchi, wenye mamlaka ni wao kwahyo inabidi uwe mpole tu maana hauna la kuwafanya watawala.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Mbona ipo hivo,wabunge zaidi ya asilimia 80 huishi dar na majimbo ni kazi tu
 
Hali ipi bwana kipara?

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app

Tunafahamu kuwa watumishi wote wa Umma ambao ni Viongozi na wapo Madarakani kwa kupigiwa kura (kupitia uchaguzi) waajiri wao na mabosi wao ni sie Wapiga kura wananchi wa nchi hii.
Sheria za kazi na mahusiano kazini zinatamka kuwa Mtumishi asipohudhuria zaidi ya siku 3 mfululizo na bila taarifa yeyote kifuatacho ni kufukuzwa kazi moja kwa moja naMwajiri wake!
Sasa inakuwaje kuna viongozi wanakosekana kazini zaidi ya mwezi na hakuna taarifa nasi kama waajiri tuko kimya kiasi eti mtumishi huyo anarudi toka mafichoni kisha anamfokea mwajiri kwa kuulizauliza aliko?
Au sheria hiyo haiwahusu viongozi wa kuchaguliwa? Kwamba anaweza kuchaguliwa 2025 kisha akaondoka kuishi Ukraine kulima ngano na kurudi 2029 karibu na uchaguzi na tusiulize? Au tukiuliza tunaambiwa tutashughulikiwa huku tukifokewa?

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Hii hali ya nchi kuhamisha mijadala ya maana inayogusa jamii zetu na kuanza kuhangaika na mtu mmoja ambaye wenyewe walitoa ufafanuzi,CCM wanatumia akili sana kudeal na watu wa nchi hii aliletwa makonda watu woote wakaimba makonda!
 
Kwanza turekebishe idadi ya siku ambazo mfanyakazi anaweza kufukuzwa asipoonekana kazini ni siku tano(5) na sio tatu,
Kwamba VP alikua wapi serikali ilikua na taarifa sio kwamba hakuwepo bila taarifa la hasha, taarifa kwa viongozi wake walijua yuko wapi hivyo suala la summary dismissal halimuhusu kiongozi wetu
 
Viongozi wake? Au mwajiri!
 
Back
Top Bottom