Adha za udomo zege

mjanja wa kijiji

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
1,469
4,081
kipindi cha balehe nakumbuka nilikuwa bingwa wa kutoa ushauri wa jinsi ya kutongoza madem kwa vijana wenzangu lakini wasichojua mimi nilikuwa muoga kwa madem hata kunguru ana afadhali, basi kuna binti mmoja mtaani nilitokea kumpenda sana lakini kumwambia ndio ikawa shida halafu binti mwenyewe alikuwa geti kali.
Nikawa nawaeleza washikaji kwamba nataka nimtokee huyo binti, jamaa wakajua sitashindwa kitu iwapo wao nimeweza kuwaunganishia na madem kwangu itakuwa kama kumsukuma mlevi vile. kulikuwa na jamaa mmoja alikuwa na kiherehere sana kila siku alikuwa ananisisitiza kuchonga nae huyo binti, nami sikutaka kuwaangusha makamanda wangu. Nikapanga siku ya kwenda wakati nimemtonya jamaa mmoja anizindikize nikashangaa kundi lote wanafuata nyuma.
tukafika eneo la tukio yule kiherehere akaenda kumuita wakati mimi nimesimama kwenye kona namsubiri ila hofu niliyokuwa nayo ni vigumu kuelezea, kulikuwa na joto lakini nilikuwa natetemeka kama ni vile nipo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro zikapita dakika kadhaa jamaa wala demu hatokei huku wapambe wakisubiri kwa hamu kuona kocha wao nitakavyomaliza mechi, baada kama dakika ishirini jamaa akaja nilishtuka sana mapigo ya moyo yakaenda mbio sana, alipofika karibu na mimi akasema baba wa yule binti yupo hivyo ťusubiri labda ataondoka mda si mrefu, moyoni nikajisemea laiti ungejua hali nayo hapa huo upuuzi usingeongea pale pale nikachomoka na kupita njia nyingine hata wale wapambe sikuwaaga.
 

We mtu umejua kunichekesha kwa kweli

Maendeleo hayana chama
 
Back
Top Bottom