Addiction ya haya magazeti yaliyofungiwa inanitesa

Nkyambe

JF-Expert Member
Mar 18, 2017
277
250
Kila nisimamapo mbele ya newspaper stand kukodolea vichwa vya habari nakumbwa na nostalgia. Nahisi maumivu ya kukosa kitu fulani cha kulisha nafsi na akili yangu nilichokizoea huko nyuma. Vichwa vya habari vinavutia lakini yaliyomo ni ya mwelekeo mmoja. Kupamba na kupongeza tu bila ukosoaji wa kina. Bila uchambuzi wa ujasiri wa kuonyesha upande wa pili ambao serikali na watawala hawapendi watawaliwa wauone. Walianza na kuzuia bunge lisioneshwe mubashara, wakafanikiwa. Wananchi wamekosa kuwasikia wabunge wao wakijadili mustakabali wa maisha na maendeleo yao! Kisa: wapo wabunge wanaokosoa kwa uwazi na uthubutu uliotukuka mwenendo wa serikali pale inapofanya madudu. Baada ya kufanikiwa kulinyamazisha bunge wakahamia kwenye magazeti yenye uthubutu na ujasiri wa kukosoa kwa kina na unyambulifu. Yakafungiwa na mengine kufutwa kabisa kwa habari eti za uchochezi. Uchochezi ambao hakuna mahali sheria iliruhusiwa kuudadavua na kuutolea maamuzi iwapo kweli ulikuwa uchochezi! Leo tena nipo mbele ya muuza magazeti, nostalgia ikinitesa. Addiction (uraibu) ya magazeti jasiri ikinitesa: uko wapi RAIA Mwema? uko wapi Mwanahalisi? uko wapi Mawio? uko wapi Mseto? uko wapi Tanzania Daima? Mmetupwa kwenye kapu la sahau kwa kusema kwenu ya sirini bila kuogopa ili sisi tuweze kuujua upande ule adimu kuoneshwa na haya magazeti mengine. Nawalilia enyi mliotupwa kaburini, iweni na subira na saburi hadi siku ya kufunguliwa kwenu. Ili siku mkirudi mitaani niweze kupona hii withdrawal effect inayonitesa (alosto?).
 

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
649
1,000
Sijanunua gazeti muda mrefu kwa kweli na mimi naumwa ugonjwa kama wako
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom