Ndugu ukitaka unafuu wa ada unatakiwa kupasua sana ili uwe na nafasi nzuri ya kuingia vyuo vya serikali kama UDSM, UDOM, MZUMBE, SUA n.k. ambapo ushindani wa kuingia kuchukua fani kama za Geology, Petroleum and Gas, Civil huwa zinagombaniwa sana na wale waliofaulu sana ndo wanapata nafasi. mfano kwa programme ya Bachelor of Science in Petroleum Engineering ya UDSM - UD060 kwenye guidebook ya TCU, capacity yake ni wanafunzi 20 tu ila wanaoiomba kwa mwaka huwa ni wengi sana zaidi ya 5,000 hadi 10,000. kwa hiyo mwishoni wanaopata nafasi ni wale tu wenye points za juu sana mfano A=5, B+=4, B=3, C=2, D= 1 na E=0.5 na F=0 kwa Grading system mpya ya BRN. ila kwa wale wa Grading za zamani A=5, B=4, C=3, D=2, E= 1 na S=0.5 na F=0. utakuta mfano mtu ana PCM = P=A, C=A, M=B+ huyu applicant ana uwezo mkubwa sana wa kupata nafasi ya hii programme ya Petroleum au Civil ya UDSM au chuo chochote cha Serikali. ila ukipata ufaulu hafifu mfano PCM una P=D, C=D, M=C hapa nafasi yako ni finyu sana ukishindanishwa na wenzako kwa hiyo utakosa nafasi kwenye vyuo vya serikali ila kwa kuwa ndoto yako ni kuwa Engineer au Daktaria utajikuta nafasi zinazobakia ni kwenye vyuo vya binafsi kama St. Joseph na KIU zenye ada kubwa sana. NIwatie shime wadogo zetu wasome sana ili wapate nafasi kwenye vyuo vya serikali.