GE2025 ACT Wazalendo yaahidi kufuta kigezo cha leseni kwa wavuvi

GE2025 ACT Wazalendo yaahidi kufuta kigezo cha leseni kwa wavuvi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Chama cha ACT Wazalendo kimeahidi kufuta leseni za wavuvi endapo wananchi watawachagua wagombea ubunge na udiwani kutoka katika chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Chama hicho kimekosoa utaratibu wa wavuvi kulipia leseni wakati huohuo wakikatwa tozo ya mafuta tofauti na ilivyo katika sekta ya kilimo ambapo wakulima hulipia tozo ya mafuta pekee wanapotumia matrekta.

Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe alisema hayo wakati wa mkutano wa kampeni wa chama hicho jimbo la Kigamboni uliofanyika Oktoba 02, 2025 jijini Dar es Salaam.

“Mkulima chombo chake cha kazi ni trekta lakini trekta halina leseni wakati mvuvi chombo chake ni boti na kina leseni, tunaposema taifa la wote maslahi ya wote maana yake haki iwe kwa wote mvuvi na mkulima”, alisema Zitto

Akimnadi Mwanaisha Mdeme ambaye ni mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chama chake, Zitto alisema mgombea huyo na wagombea wengine wa chama wanaotoka katika maeneo yenye uvuvi wataungana kuwatetea wavuvi nchini.

Aidha alikosoa utaratibu wa mvuvi kulipa leseni za wasaidizi wake wanapokuwa kwenye shughuli za uzalishaji wakati katika sekta nyingine za usafirishaji na kilimo mwenye leseni ni dereva pekee

“Watu wa malori tingo hana leseni lakini kwenye sekta ya uvuvi kila aliyepo ndani ya boti ya uvuvi anakatiwa leseni kwa sababu hamna mtu wa kuwasemea”, aliongeza Zitto

Naye mgombea ubunge katika jimbo hilo, Mwanaisha Mdeme aliwaomba wananchi kumtuma bungeni ili akatatue changamoto za miundombinu na huduma duni za kijamii zilizopo katika jimbo hilo.

“Asubuhi tunapokwenda kwenye shughuli zetu tunashuhudia wanafunzi wakitembea muda mrefu kwenda shule kwa sababu hakuna mabasi ya abiria kutokana na ubovu wa barabara”, alisema Mwanaisha
559442829_18119077237513179_2302767527343098656_n.jpg
558665255_18119077132513179_4159256400858272206_n.jpg
559539069_18119077141513179_3257529810251191323_n.jpg
 
Chama cha ACT Wazalendo kimeahidi kufuta utaratibu wa leseni kwa wavuvi endapo kitapata ridhaa ya wananchi kupitia wagombea wake wa ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa jana, Oktoba 2, 2025 na kiongozi mstaafu wa chama hicho, Zitto Kabwe, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Kigamboni jijini Dar es Salaam, alipokuwa akinadi mgombea ubunge wa chama hicho katika jimbo hilo, Mwanaisha Mdeme.

Zitto amesema utaratibu wa sasa unaowataka wavuvi kulipia leseni za boti na wasaidizi wao ni kandamizi na wa kibaguzi ikilinganishwa na sekta nyingine, hasa kilimo.

“Mkulima chombo chake cha kazi ni trekta, lakini trekta halina leseni. Mvuvi chombo chake ni boti, tena anatozwa leseni. Tunaposema taifa la wote, maslahi ya wote, maana yake haki iwe kwa wote, kwa mvuvi na mkulima,” amesema Zitto.

Mwanaisha Mdeme amewataka wananchi wa Kigamboni kumchagua ili akalete sauti yao bungeni na kushughulikia changamoto zinazolikabili jimbo hilo, ikiwemo barabara mbovu na huduma hafifu za kijamii.
 
Mgombea wao alieenguliwa na pingamizi la mwanasheria mkuu wa serikali ndio alikuwa kinara wa kuwachome nyavu zao wavuvi
 
Back
Top Bottom