mkuu hili suala la kuwa ccm nimelikana siku nyingi sana, kwanza ungejua ninavyoichukia ccm wala usingeandika haya humu. nimejiunga humu takriban miaka 5 sasa. angalia nimeanza kuchangia lini? hapo mwanzo nilikuwa msomaji tu, kuchangia kwangu kulianza rasmi baada ya wapinzani tuliokuwa tunawategemea kuanza kuleta mizengwe. Kufukuzwa kwa zitto kwa sababu tu alitaka kugombea uenyekiti wa chama kuliniudhi sana. unapozungumza chadema unawazungumza watu muhimu zaidi wawili. Zitto na Slaa. Hao ndo walioiuza chadema mitaani. lakini akina mbowe wamemfukuza Zitto as if alikuwa sio chochote. na wala hakupewa hata nafasi ya kujitetea kwenye vikao halali. waliokuta chadema imekomaa kama akina godless lema, tobo lisu waliotoka NCCR na TLP na kwengineko ndo wakawa na thamani kubwa kuliko wengine. kwa taarifa yako hiyo ndo sababu ya mimi kuandika humu. na kwa sasa naichukia zaidi chadema hii ya akina mbowe kuliko hata ccm.
kuachilia mbali kuwa kwa yeyote atakayekuja sitaathirika sana; lakinini pia uwezekano wa Magufuli kushinda ni 90%. lowasa na ukawa nawpa 10% tu.
sizungumzii percentage ya kura watakazopata nazungumzia probability. uelewe hilo.
na nakushauri uanze kujifanyia cancelling sasa hivi maaa usije ukafa na pressure bure.
Natamani nikumbuke ili nikukumbushe october baada ya uchaguzi.