Zanzibar 2020 ACT Wazalendo wapewa somo zito, CCM haiko tayari kutenda haki katika chaguzi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
ACT walidhani kuwa maadam wamo katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa huko Zanzibar, basi labda CCM wangeanza kuwatreat fairly.
Lakini wakasahau kuwa CCM kimeshakuwa chama cha dhulma, kama kiliwadhulumu mara ya kwanza, mara ya pili, mara ya tatu n. k kitaendekea kuwadhulumu mpaka itokee nguvu ya kukomesha dhulma hiyo.

Sasa juzi wameshiriki uchaguzi huko Konde, wamefanyiwa michezo ileile ya kihuni.

Huko Kigoma pia wakishiriki uchaguzi, wakalialia kufanyiwa michezo ya ajabu kabla ya baadae kutoa ripoti ya kujikosha.

Hawa jamaa wa ACT kiukweli kabisa kukubali kwao kushiriki kwenye ile serikali ya Zanzibar kulinyong'onyesha mapambano ya wananchi kudai katiba mpya yenye tume huru za chaguzi ndani yake.

Kiufupi kilichofanyika katika makubaliano yale ni tamaa tu ya madaraka ya baadhi ya watu, na pia inasemwa kuwa kuna watu walihakiishiwa kuwa kwenye payroll ya Serikali ili wabariki dhulma ile, na sote tunaona wametulia tuli!

Watanganyika na Wazanzibar bila kuungana na kudai katiba mpya hawa CCM wataendelea kufanya uhuni wao uleule

Hizi Chaguzi za marudio zituonyeshe tu uchaguzi wa 2025 utakuwaje kama hakuna mabadiliko yoyote ya msingi katika hizi tume.

 
Ndio sasa wanashituka

Screenshot_20210719-075127_Twitter.jpg
 
CCM likija suala la maslahi yao hawana urafiki na mtu, usijichanganye kabisa, namsubiri Zitto aje na tamko sijui atasemaje safari hii, na asipoangalia iko siku ataishiwa maneno aanze kulia tu.
 
Ukijumlisha kura za mgombea wa CHADEMA na ACT zinazidi zile za CCM hapo bado za vyama vingine.

CHADEMA waliishajiapiza kutoshiriki uchaguzi lakini huu wa Konde wameshiriki ingawa kijanja kwa kujidai kuwa mgazi ya chini wamekaidi maagizo ya ngazi ya Taifa, CHADEMA waliishafanya tathmini kuwa wakiingia uchaguzi watagawa kura hivyo ACT hawawezi kushinda. Lengo lilikuwa kuzuia ACT wasishinde.

Kura zimepigwa 5000 lakini CCN imeshinda kwa kura zisizofika 2000.

Unafiki ni tatizo kubwa miongoni mwa wapinzani, na kinachoangaliwa ni maslahi binafsi.
 
Back
Top Bottom