ACT-Wazalendo mnapata wapi pesa za kuendesha chama?

ACT-Wazalendo mnapata wapi pesa za kuendesha chama?

kwa kweli tunahitaji tuwekwe wazi,naamini wazalendo wataonesha uzalendo wao kutupa majibu ya hili.
 
Mimi naupenda huo uzalendo, lakini kama kweli ninyi ni wazalendo, wekeni hapa chanzo chenu cha mapato. Naona chama chenu kilianza zamani kidogo lakini hakikupata kufanya mambo hadi siku kiongozi wenu mkuu alipochukua kadi na kupewa uongozi ndipo tukaanza kuona harakati. Je, ZZK ndiye ACT? Je, mna ujasiri wa kutueleza mnapata wapi mapato yenu kwa ghafla namna hiyo? Kwa nini tuwaamini?

Chanzo cha mapato ya chama chochote ni michango ya wapenzi, wanachama na watu wenye imani na itikadi,msimamo na mwelekeo wa chama. Wote waliopo kwenye vyama wanajua hilo.

ACT kwa wakati wake kitatoa taarifa juu ya michango na mapato ya chama, msingi wa ACT ni UADILIFU NA UWAZI. Chama kitakaguliwa na wakaguzi watakaoteuliwa na CAG, na tofauti na vyama vingine aACT haihitaji ITONYWE KWANZA JUU YA UKAGUZI WA CAG, ACT itajipeleka yenyewe kwa CAG na taarifa yake itawekwa wazi.Ndio tofauti ya ACT na vyama vingine.

Nje ya hilo, mbona watu wenye vyama vyao mna hamu sana na mapato na matumizi ya ACT wakati ata hamjui mapato na matumizi ya vyama vyenu??si mlipaswa muwe na uchungu zaidi na pesa za chama chenu kabla ya kufuatilia za ACT?vip mna uchungu na mapato na matumizi ya ACT kuliko ya chama chenu cha Chadema??siasa za kukosa hoja.Watanzania wamechoka siasa za aina hii.
 
"Nenda ukamuulize Mzee Mtei chadema ilianza haina ruzuku fedha za ziara walitowa wapi" -@Zitto kabwe
 
Wakati kunavyama vina miaka zaidi ya 10 vimeshindwa kufanya mikutano hata mkoa mzima.

Nyie hamna wabunge wala madiwani wanaokichangia chama.

Kama Zitto aliweza kutangaza mali alizonazo na amezipata vipi, kwanini ameshindwa kutueleza pesa za kuendesha chama zinapatikana wapi?

Wadhamini wa chama ni akinanani.

Kama mtanzania nahitaji majibu?

Alafu bila kusahau,huko nyuma Mwl.Kaijage alishatuambia kuwa ili kuakisi jina la chama watakuwa wakiweka wazi taarifa mbalimbali hasa za fedha (na Uzi upo humu).Lakini mpaka leo kimya na wala hakuna dalili ya kufanya hivyo.

Ni wazi hawawezi kufanya hivyo asilani.
 
Wakati kunavyama vina miaka zaidi ya 10 vimeshindwa kufanya mikutano hata mkoa mzima.

Nyie hamna wabunge wala madiwani wanaokichangia chama.

Kama Zitto aliweza kutangaza mali alizonazo na amezipata vipi, kwanini ameshindwa kutueleza pesa za kuendesha chama zinapatikana wapi?

Wadhamini wa chama ni akinanani.

Kama mtanzania nahitaji majibu?

Ni mikakati tu mkuu,
 
Haa haa inawezekana zile 700 milioni walizoomba kwa lowasa ndo zinafanya kazi.
 
mtoa mada ameuliza swali la msingi sana cha ajabu majibu hakuna ya maana watu wajibu upuuzi mtupu
 
Mkuu wangu hata kujibu hayo machache ni credit, si viongozi wengi wana ujasiri wa kuface hadhira na kujibu maswali yao. Pia kiongozi makini kama ZZK hawezzi kukurupuka kujibu maswali ambayo anahitaji muda kuyatafakari na kutafutia majibu yake, lakini ukumbuke kuwa yapo maswali mengine hayana majibu.

Nakuhimiza ndugu, fuatilia kwa karibu mikutano ya ACT na soma vyema sera na katiba ya ACT kisha fananisha na vyama vingine utagundua kuwa kuna tofauti kubwa sana. Juzi nimeshangaa sana kwa Mbowe kusema hatokubali JK kujiongezea muda wa kuongoza, wakati katika katiba yao ya chama hakuna ukomo wa uongozi...........

Hujajibu swali kuhusu Mbowe katiba ya CHADEMA so katiba ya nchi JK angeongeza muda kivipi wakati katiba haijarekebishwa kama ingekuwa mtihani ungefeli
 
Kwani si wamesema Lowasa akikatwa jina CCM aende ACT-Utapeli.
 
Alafu bila kusahau,huko nyuma Mwl.Kaijage alishatuambia kuwa ili kuakisi jina la chama watakuwa wakiweka wazi taarifa mbalimbali hasa za fedha (na Uzi upo humu).Lakini mpaka leo kimya na wala hakuna dalili ya kufanya hivyo.

Ni wazi hawawezi kufanya hivyo asilani.

Nadhani wataweka baada ya kumaliza mikutano yao....ngoja tuwasubiri
 
mimi mwenyewe nachangia hiki chama kila siku siku kwani nyie zile milioni 300 mnapelaka wapi? haadi mnatuchangisha michango ya mikutano kila siku tumieni mali vizuri
 
chanzo cha mapato ya chama chochote ni michango ya wapenzi, wanachama na watu wenye imani na itikadi,msimamo na mwelekeo wa chama. Wote waliopo kwenye vyama wanajua hilo.

Act kwa wakati wake kitatoa taarifa juu ya michango na mapato ya chama, msingi wa act ni uadilifu na uwazi. Chama kitakaguliwa na wakaguzi watakaoteuliwa na cag, na tofauti na vyama vingine aact haihitaji itonywe kwanza juu ya ukaguzi wa cag, act itajipeleka yenyewe kwa cag na taarifa yake itawekwa wazi.ndio tofauti ya act na vyama vingine.

Nje ya hilo, mbona watu wenye vyama vyao mna hamu sana na mapato na matumizi ya act wakati ata hamjui mapato na matumizi ya vyama vyenu??si mlipaswa muwe na uchungu zaidi na pesa za chama chenu kabla ya kufuatilia za act?vip mna uchungu na mapato na matumizi ya act kuliko ya chama chenu cha chadema??siasa za kukosa hoja.watanzania wamechoka siasa za aina hii.
ila hizi sarakasi hazikuwepo wakati wa limbu
 
mimi mwenyewe nachangia hiki chama kila siku siku kwani nyie zile milioni 300 mnapelaka wapi? Haadi mnatuchangisha michango ya mikutano kila siku tumieni mali vizuri
jibu swali acha kuuliza maswali juu ya maswalii
 
Back
Top Bottom