Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ameweka msimamo mzito kuhusu mchakato wa maridhiano nchini, akisisitiza kuwa chama hicho hakitashiriki katika mazungumzo yoyote ya "ulaghai" yanayolenga kufunika makosa yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza kwenye kikao cha viongozi wa chama cha ACT Wazalendo kilichofanyika Januari 8, 2026 Jimbo la Lindi Mjini katika ukumbi wa Gafu, Kata ya Makonde mkoani Lindi, Semu amesema maridhiano ya kweli lazima yasimame kwenye misingi ya haki, uadilifu, na kukiri kwa makosa yaliyofanywa dhidi ya raia.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa maridhiano ya dhati yanapaswa kuambatana na mageuzi ya kimuundo katika mifumo ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi ambayo imekuwa chanzo cha migogoro nchini. Amesema kuwa ACT Wazalendo itakuwa mstari wa mbele kudai maridhiano jumuishi yanayoheshimu utu wa kila Mtanzania badala ya kutumika kama chombo cha kuhalalisha dhuluma.
Semu alitumia fursa hiyo kutoa pole kwa wanachama na wakazi wa Lindi waliokumbwa na madhila wakati wa uchaguzi, akihimiza umoja na mshikamano katika kuendelea kupigania haki za raia