ACT-Wazalendo kuvuna wabunge kutoka CCM na CHADEMA

ACT-Wazalendo kuvuna wabunge kutoka CCM na CHADEMA

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
56,943
Reaction score
46,442
Wanaukumbi.

Baada ya vumbi la uchaguzi mkuu kuanza kumtika tumeona kura za maoni zinazoendelea kupigwa kutoka Chadema na CCM kwenye kila jimbo.

Chadema wanachagua wagombea ili baadae watakapokubaliana na wenzao CUF, NCCR Mageuzi, NLD, itabidi baadhi ya Majimbo wapewe vyama hivyo ambavyo vipo kwenye umoja huo UKAWA.

Na hapo ndiyo utazuka mgogoro mkubwa wa baadhi ya wagombea ambao majimbo yao watapewa UKAWA, hapo ndipo ACT-Wazalendo watakapojipatia wagombea wanaokubalika na kuwasimamisha kama wagombea wa ACT-Wazalendo.

Vile wagombea wa CCM ambao watakatwa pia kuna uwezekano mkubwa wakakimbilia ACT-Wazalendo.

Hapo ndiyo kauli ya Zitto kuwa wagombea hamsini watahamia ACT-Wazalendo itatimia.

Huu ndiyo ukweli ingawa unauma kuusoma hii hali kwenye siasa uwa inatumika sana.

Wale wote waliofanyiwa fitna watatumia mbinu hii ambayo imewahi kutumiwa na Dr.W.Slaa wakati yupo CCM kabla ya kutimkia Chadema na kushinda ubunge.


========Updates========
10.8.2015


Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chadema, Chiku Abwao )akuongea na wafuasi wa ACT - Wazalendo baada ya kupitishwa na chama hicho kugombea ubunge Jimbo la Iringa Mjini.


By Geofrey Nyang’oro, Bakari Kiango, MwananchiDar/Iringa. Kada aliyewania ubunge kupitia Chadema katika Jimbo la Kalenga na kutemwa kwenye kura za maoni, Mwanahamisi Muyinga ameibuka mshindi wa kura hizo katika jimbo hilohilo kupitia chama cha ACT-Wazalendo.

Katika uchaguzi uliofanyika katika Kata ya Mlandege mwishoni mwa wiki iliyopita, Muyinga aliibuka mshindi kwa kupata kura 10 akifuatiwa na Daniel Mwangili aliyepata kura saba, huku Edward Mtakimwa na Kiduo Mgunga wakipata kura tatu kila mmoja.

Mbali na Muyinga, wengine waliotemwa Chadema na kushinda ACT ni aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kunduchi, Janeth Rithe na Dickson Ngh’illy aliyewahi kugombea Jimbo la Temeke mwaka 2010.

Katibu mwenezi wa Chadema Wilaya ya Butiama naye ahamia ACT-Wazalendo.
 
si mlisema bunge likiisha tu kuna wabunge hamsini wanakuja huko?

Wako wapi?

Na nyie act sijui etc... siasa hamziwezi
 
Scavengers
Siyo waokotezaji hata Slaa alivyokosa ubunge Karatu kupitia CCM alikimbila Chadema.

Wewe unadhani mtu kakipigania chama miaka yote leo hii umwambie itabidi akae pembeni Jimbo wanapewa NLD UKAWA atakubali?

Suburi uone vumbi litakavyotimka.
 
Kwa hiyo sio kuwa wanahamia Bali wanaenda baada ya kukosa nafasi huku? Kauli ya CEO ilikuwa wanahamia kwa ridhaa yao kwa kufurahishwa na sera kumbe sivyo!
 
Kwani mkuu Ritz ACT haina wanachama wanaofaa kuwa wagombea mpaka wawe na sifa kama ya KIONGOZI MKUU?
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo sio kuwa wanahamia Bali wanaenda baada ya kukosa nafasi huku? Kauli ya CEO ilikuwa wanahamia kwa ridhaa yao kwa kufurahishwa na sera kumbe sivyo!
Mkuu unakumbuka Dr.Slaa alivyohamia CCM? watatumia mtindo huo huo kama wa Dr.Slaa.
 
Act wanaenda kwa philosophy ya fisi, ya kuufatilia mkono wa binadamu kwa mategemeo kwamba utaanguka ili waule
 
Ritz na wewe umeshachukua kadi?
 
Last edited by a moderator:
Huo ndio mtego wa watu wajanja.Utafiti wako Upo vzr.
Hizi kura za maoni tayari zimeishaleta mgawanyiko mkubwa na UKAWA lazima waachiane majimbo, ACT-Wazalendo wamerusha kokoro lao wanasubiri kuanza kulivuta lazima watapata samaki kama siyo sangara hata sato na dagaa wanatosha.
 
Mara uwe msemaji wa ACT mara CCM. Sasa huo unafiki wako tukweleweje? Mambo ya UKAWA yaacheni. Hangaikieni mambo yenu ACT na CCM. Mwaka huu mmeshikwa pabaya na propaganda hizo haziwasaidii
 
Mwenyekiti amesema tutulie mambo yatakua mazur. Na Salam mmezipata juzi Mwanza
 
Hiyo ni subira za fisi kuvizi mkono wa binadam ukatike naye aokote, hatimaye anasindikiza mpaka mtu anafika aendako.
 
Hizi kura za maoni tayari zimeishaleta mgawanyiko mkubwa na UKAWA lazima waachiane majimbo, ACT-Wazalendo wamerusha kokoro lao wanasubiri kuanza kulivuta lazima watapata samaki kama siyo sangara hata sato na dagaa wanatosha.

Maalim thread yako inaivua nguo ACT na Zitto...Unatoa picha kuwa hawawezi kupata ''cream'' bali wao ni wa kusubiri makombo tu! Come on you can do better, ustaadh!
 
Tukiacha ushabiki wa kijinga na tukikubali kufungua akili sisi wapinzani tutagundua Ritz ameongea la kweli. Nna wasiwasi litatokea.
 
Last edited by a moderator:
ACT ni chama cha waswahili kwa ujumla kimekwisha!!!
 
Back
Top Bottom