ACT-Wazalendo kuvuna wabunge kutoka CCM na CHADEMA

ACT-Wazalendo kuvuna wabunge kutoka CCM na CHADEMA

Huu ndiyo ukweli mkuu pamoja kuwa unauuma.

UKAWA ni vyama vitano tu CUF, NCCR Mageuzi, Chadema, NLD.

Na moja ya ushirikiano wao ni kuachiana majimbo ya uchaguzi.

Hizi kura za maoni zinazoendelea Chadema majimbo mengine lazima wawape UKAWA.

eti UKAWA ina vyama vitano tu CUF, NCCR, CHADEMA na NLD, loh
 
Mimi nasubiri kuona majimbo ya uchaguzi watayopewa NLD.
 
Kwani UKAWA una vyama hivyo tu?

Vyama vyote vya UKAWA vinagawana majimbo ya uchaguzi, usipotoshe.

Unachochea kuni kama kawaida yako?

Sasa kapotosha nini Hapo? Au hujamuelewa? Hujui kama kuna majimbo ambayo kuna wanachama wa vyama vya ukawa wote wanakubalika? Sasa unadhani ataekatwa atakubali kisa kumpisha mwana ukawa mwenzake? Huyo ataekatwa hana option zaidi ya kwenda ACT ndio Ritz anachozungumzia hapa, nchi hii kubwa sana na ACT itavuna sana kwa style hiyo
 
Last edited by a moderator:
Hili ni jibu langu la kuondoa aibu,Nilipouliza jana inamaana ACT wanaohamia ni kutoka CDM na Nccr tu?
Naona mmeona nishai mkaona mje na huu mpango wa kuaminisha watu hata watu kutoka Ccm wanahamia Act
Yani nyumba moja watu wanahama vyumba tu,Na kujipongeza wamehamia nyumba mpya.
 
Nilidhani ACT ni chama kimejipambanua kuwa kina wanasiasa wa tofauti na tuliowazoea, na tofauti hiyo yatokana na UZALENDO!!!

Sasa hawa watakaokatwa ndio wazalendo? Na hawa waliopo sasa ndani ya chama wao hawana lao?

Kwa jinsi ACT inavyonadiwa kuwa ni chama makini, chama cha wenye akili kubwa, inashangaza wangoje kula matapishi ya wenye akili ndogo na wasio na uzalendo.

ACT jipangeni vizuri bado mmekaa kilaghai laghai tu
 
Hili ni jibu langu la kuondoa aibu,Nilipouliza jana inamaana ACT wanaohamia ni kutoka CDM na Nccr tu?
Naona mmeona nishai mkaona mje na huu mpango wa kuaminisha watu hata watu kutoka Ccm wanahamia Act
Yani nyumba moja watu wanahama vyumba tu,Na kujipongeza wamehamia nyumba mpya.
Umeona mkuu?

Chama cha upinzani kinachojengeka kwa kutafuta viongozi wa vyama vingine vya upinzani, badala ya kupunguza nguvu ya Chama tawala, ni tawi la chama tawala?
 
Ndio nini sasa. CHADEMA ni chama na UKAWA ni umoja, sasa kuachia ukawa ndio chama gani, kwani wao ni nje ya UKAWA?

Mkuu inawezekana mimi unielewi msome Dr.Slaa.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema endapo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vitashindwa kuafikiana katika kuachiana baadhi ya majimbo kabla ya Uchaguzi Mkuu, watawaeleza wananchi kwa kuwa ndiyo kiini cha kuanzishwa kwa umoja huo.

Dk Slaa alisema hayo jana kabla ya kumalizika kwa vikao vya wakuu wa Ukawa ambao wamekubaliana kusimamisha mgombea mmoja kuanzia ngazi ya urais, ubunge na udiwani na kwa siku mbili kuanzia juzi, walikuwa wakijadili ufanikishwaji wa azimio hilo.

Dk Slaa alisema hadi sasa wameshakubaliana kuachiana asilimia 95 ya majimbo yote na kwamba ana matumaini watafanikisha, lakini akaonya kuwa ikishindikana, hawatasita kuwaeleza wananchi.Mkoani Dar es Salaam, Ukawa imeshafikia muafaka katika majimbo mawili ya Kawe na Ubungo na kubakiza majimbo sita, wakati majimbo matano ya mikoa mingine bado yanaupasua kichwa umoja huo wa vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD.

Chanzo: Mwananchi
 
Sasa kapotosha nini Hapo? Au hujamuelewa? Hujui kama kuna majimbo ambayo kuna wanachama wa vyama vya ukawa wote wanakubalika? Sasa unadhani ataekatwa atakubali kisa kumpisha mwana ukawa mwenzake? Huyo ataekatwa hana option zaidi ya kwenda ACT ndio Ritz anachozungumzia hapa, nchi hii kubwa sana na ACT itavuna sana kwa style hiyo
Mkuu wangu unadhani hawaelewi basi tu hawataki kukubaliana na ukweli.
 
Last edited by a moderator:
Hili ni jibu langu la kuondoa aibu,Nilipouliza jana inamaana ACT wanaohamia ni kutoka CDM na Nccr tu?
Naona mmeona nishai mkaona mje na huu mpango wa kuaminisha watu hata watu kutoka Ccm wanahamia Act
Yani nyumba moja watu wanahama vyumba tu,Na kujipongeza wamehamia nyumba mpya.
Mkuu mbona wanahamia Chadema ni kutoka CCM tu kina Lembeli, Ester na wengine na sasa mnamuomba Lowassa ahamie Chadema huoni kama mnachukuwa makapi.
 
Siyo waokotezaji hata Slaa alivyokosa ubunge Karatu kupitia CCM alikimbila Chadema.

Wewe unadhani mtu kakipigania chama miaka yote leo hii umwambie itabidi akae pembeni Jimbo wanapewa NLD UKAWA atakubali?

Suburi uone vumbi litakavyotimka.

Wewe usipomtaja Dr. Slaa uwezi kulala, uliyotunga ni uongo mtupu, achana na Akili kama za Inzi kuchezea mali ghafi wakati mwenzie anazitumia kutengeneza asali.
 
Wangalienda kwa sababu ni waumini wa sera, itikadi, misingi ya chama na falsafa ya chama ningeliumia sana ila kwa sababu wanakwenda kwa kuwa wamekosa nafasi za ubunge itakuwa ni njaa zao na waje uko njia nyeupe. Kama nyinyi mlivyoondoka siyo mbaya ni haki yao kuhama ama kwa njaa zao au uzalendo wao.
 
Umepoteza dira weye

Ndio maana Wake wakasifiwa kwa ajili ya kuwaelekeza waume zao ili wasipoteze Hizo Dira.

We mimba changa inakusumbua mpk unaelekeza Waume za watu
Hali ya kuwa Nyonda wako Nicholas umemsahau anakufa na Gongo!.

Angalia Nicholas asije kukufania tu unajadili na midume mingine. Utanyea kwenye ndoo. Shauri yako.
 
Last edited by a moderator:
Kumekucha tena.
 
Wewe usipomtaja Dr. Slaa uwezi kulala, uliyotunga ni uongo mtupu, achana na Akili kama za Inzi kuchezea mali ghafi wakati mwenzie anazitumia kutengeneza asali.

SLAA amesalitiwa na Wakristo wenzake kwa kupenda Noti.

Walutheran na wakatoliki picha haziendi.
Km vile Bruce lee na b.olo young!

Teh teh teh
 
Machemli wa Ukerewe naye yupo njiani.
 
Wanaukumbi.

Baada ya vumbi la uchaguzi mkuu kuanza kumtika tumeona kura za maoni zinazoendelea kupigwa kutoka Chadema na CCM kwenye kila jimbo.

Chadema wanachagua wagombea ili baadae watakapokubaliana na wenzao CUF, NCCR Mageuzi, NLD, itabidi baadhi ya Majimbo wapewe vyama hivyo ambavyo vipo kwenye umoja huo UKAWA.

Na hapo ndiyo utazuka mgogoro mkubwa wa baadhi ya wagombea ambao majimbo yao watapewa UKAWA, hapo ndipo ACT-Wazalendo watakapojipatia wagombea wanaokubalika na kuwasimamisha kama wagombea wa ACT-Wazalendo.

Vile wagombea wa CCM ambao watakatwa pia kuna uwezekano mkubwa wakakimbilia ACT-Wazalendo.

Hapo ndiyo kauli ya Zitto kuwa wagombea hamsini watahamia ACT-Wazalendo itatimia.

Huu ndiyo ukweli ingawa unauma kuusoma hii hali kwenye siasa uwa inatumika sana.

Wale wote waliofanyiwa fitna watatumia mbinu hii ambayo imewahi kutumiwa na Dr.W.Slaa wakati yupo CCM kabla ya kutimkia Chadema na kushinda ubunge.

========Updates========
10.8.2015

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chadema, Chiku Abwao )akuongea na wafuasi wa ACT - Wazalendo baada ya kupitishwa na chama hicho kugombea ubunge Jimbo la Iringa Mjini.

By Geofrey Nyang’oro, Bakari Kiango, MwananchiDar/Iringa. Kada aliyewania ubunge kupitia Chadema katika Jimbo la Kalenga na kutemwa kwenye kura za maoni, Mwanahamisi Muyinga ameibuka mshindi wa kura hizo katika jimbo hilohilo kupitia chama cha ACT-Wazalendo.

Katika uchaguzi uliofanyika katika Kata ya Mlandege mwishoni mwa wiki iliyopita, Muyinga aliibuka mshindi kwa kupata kura 10 akifuatiwa na Daniel Mwangili aliyepata kura saba, huku Edward Mtakimwa na Kiduo Mgunga wakipata kura tatu kila mmoja.

Mbali na Muyinga, wengine waliotemwa Chadema na kushinda ACT ni aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kunduchi, Janeth Rithe na Dickson Ngh’illy aliyewahi kugombea Jimbo la Temeke mwaka 2010.
Wewe ndiyo msemaji wa Zitto na ACT siku hizi?
 
Back
Top Bottom