Rashda Zunde
JF-Expert Member
- May 28, 2022
- 297
- 285
Chama cha ACT-Wazalendo kinaonesha wazi kutowathamini wanawake na kukosa imani nao katika nafasi za juu za uongozi. Hali hii imejidhihirisha baada ya kumtangaza Luhaga Mpina kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho kwa Uchaguzi Mkuu wa 2025, licha ya kuwepo kwa Dorothy Semu ambaye tayari alikuwa amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa tiketi hiyo hiyo.
Uamuzi wa kumpitisha mwanasiasa aliyejiunga na ACT kwa ghafla kutoka CCM, na kumweka mbele ya mwanamke aliyekulia ndani ya chama hicho na kujitoa kwa hali ya juu, ni kielelezo tosha cha mfumo dume unaotamalaki ndani ya ACT-Wazalendo. Ni hatua inayoashiria kuwa mwanamke, hata awe na historia ya uaminifu na mapambano ya kweli ndani ya chama, bado hatapewa nafasi ya kuaminiwa kuongoza taifa.
Dorothy Semu amekuwa miongoni mwa viongozi waliolijenga ACT-Wazalendo kwa nguvu na kujitoa kwa hali na mali. Moja ya vielelezo vya kujitoa kwake ni tukio la Aprili 24, 2025, alipokwenda Mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi inayomkabili Tundu Lissu. Akiwa mstari wa mbele kuonesha mshikamano na chama chake, Dorothy alikumbana na kejeli, dhihaka na hata vitisho nje ya mahakama hiyo – lakini hakurudi nyuma. Alisimama imara kwa ajili ya chama alichokipigania kwa miaka mingi.
Lakini pamoja na kujitoa huku kwa dhati, ACT-Wazalendo imeamua kumtupilia mbali na kumwekea mbele mwanamume mpya aliyejiunga kwa ghafla. Huu ni uthibitisho kuwa wanawake hawana nafasi ya kweli ndani ya ACT-Wazalendo – chama kinachojinasibu kuwa cha mabadiliko, lakini bado kinahifadhi mizizi ya ubaguzi wa kijinsia.