ACT-Tanzania yapata usajili wa kudumu!

ACT-Tanzania yapata usajili wa kudumu!

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
Chama kilichovunja rekodi kwa kupata usajili wa kudumu miezi michache mara baada ya usajili wa muda; ACT-TANZANIA leo ndio kimekabidhiwa cheti chake cha usajili wa kudumu rasmi na masajili wa vyama vya siasa mara baada ya kumalizika zoezi la usajili lililofanyika katika mikoa kumi iliyoteuliwa.

ACT-TANZANIA

cheti5.jpg

cheti,,,.jpg

cheti.jpg
Mwenyekiti akikabidhiwa cheti.

kilifanikiwa kumaliza zoezi la uhakiki mara baada ya kuruka vihunzi vingi toka kwa wahafidhina na watu wasiopenda siasa za ushindani. Katika zoezi letu tumekumbana na vikwazo vingi ikiwa pamoja na uchomekaji wa wanachama fake waliotumwa kwaajili ya kazi ya kujifanya wako tayari kuhakikiwa lakini kwa lengo la kutojitokeza siku ya kuhakikiwa, jambo ambalo wahafidhina na maadui zetu walikuwa hawajui ni kuwa chama chetu kinapendwa na wananchi hivyo wengi walijitokeza kiasi cha kuziba mapengo ya mamluki ambao kwa makusudi hawajajitokeza siku ya kuhakikiwa. Pamoja na hayo tunatambua wanachama wetu waaminifu waliotaka kujitokeza lakini sababu zilizo nje ya uwezo wao zilipelekea washindwe kujitokeza siku ya kuhakikiwa.

Karibu ACT-TANZANIA, wewe ndio mbadala wa CHADEMA na CCM.

Mungu ibariki Tanzania.

cheti.......jpg

Njano5.
Mwanachama.
0784845394
 
Naanza kutilia mashaka umakini wa Msajiri wa vyama vya Siasa Mhe. Judge Mtungi. Inawezekana vipi judge MAKINI asajiri acronym ya ACT kuwa chama cha Siasa Tanzania? Acronym ya ACT is an International registered trade mark ya Atermisinin Combination Therapy (ACT). Waswahili sisi tunaiita DAWA MSETO ya kutibu malaria. Huyu judge Mtungi anahitaji dose ya ACT atakuwa amepata cerebral malaria!
 
Ujio wa hiki chama hauna maana yoyote, kwani chama hili kilibuniwa mahsusi kujaribu kuzipunguza kura za CDM 2015, Kwa sasa habari ya mjini ni UKAWA.

Mpango mzima umedoda kabla hata haujaanza - Poleni MM1 & MM2 na MM3. (Missing in Action!!). UKAWA mpango mzima!!
 
hongereni sana, sasa mkaijenge demokrasia, msipambane na wapinzani wenzenu,pambaneni na adui ujinga,maradhi na umaskini
 
Ok,hivi kile ADC kilifia wapi,naona kama vinafanana majina.
 
Kwanini wanatumia rangi inayotumika sana kwenye misiba (purple)?
 
WanaJamvi hivi ADC ipo kweli!! naona Mwelekeo uleule wa WASALITI.
 
Naanza kutilia mashaka umakini wa Msajiri wa vyama vya Siasa Mhe. Judge Mtungi. Inawezekana vipi judge MAKINI asajiri acronym ya ACT kuwa chama cha Siasa Tanzania? Acronym ya ACT is an International registered trade mark ya Atermisinin Combination Therapy (ACT). Waswahili sisi tunaiita DAWA MSETO ya kutibu malaria. Huyu judge Mtungi anahitaji dose ya ACT atakuwa amepata cerebral malaria!

Wewe unaumwa. Hakuna abbreviation yenye maana moja duniani. Muhimu ni nini maana ya hiyo abbreviation.
 
Ujio wa CCJ ulitisha sana, lakini hiki chama cha CCJ kipo wapi?, labda Nape anajua. Aidha, huyo mwenyekiti ndo huyo huyo aliyeshiriki kuanzisha ADC, kwa hiyo hapo wanacheza shere.

wanapoteza muda wao bure sisi kwa sasa tunaangalia nini kitafuata kwenye katiba mpya.
 
Wewe unaumwa. Hakuna abbreviation yenye maana moja duniani. Muhimu ni nini maana ya hiyo abbreviation.

Wewe ndiyo unaumwa, unahitaji ACT tena yenye nembo ya jani iliyothibitishwa WHO. Kama ni hivyo hebu nenda kwa Mtungi usajiri chama kwa acronym ya CCM umwambie abbreviation yake ni Chama Cha Makini (CCM), uone kama atakisajiri?
 
Mi pia nimo huko kwa mission, jidanganyeni, mlikua traitors and i wil be
 
hawa ndio wapinzani wa kweli wenye hoja sio haya machumia tumbo
 
Back
Top Bottom