ACT-Tanzania , Taarifa Mkononi mwako

ACT-Tanzania , Taarifa Mkononi mwako

kweli kabisa ndugu, usiwape namba yako kabisa maana ukiwapa namba yako ya simu watakuibia simu yako, halafu ukiwapa parua pepe watakuibia E-mail yako. Yaani ni hatari sana! usikubali kabisa mkuu!

nawapenda sana Act lakini kuna mambo yanantia shaka? Kwa nini mnashabikiwa sana na ccm? nyie ni chama cha upinzani kweli au mpo kuisadia ccm? halaf kwa nini viongozi wemu na baadhi ya mashabiki wenu ni wale waliofukuzwa chadema? viongozi wenu wataaminikaje wakati wana kashfa inayojulikana na watz karibia wote? ujingaaliyofanya Kitila umemwaibisha sana hata ya wasomi wenzake wamemshangaa na kutokuamini kitila anaweza kuwa so low.pmbona chama chemu hakionekani kimeanzishwa kwa nia njema? Mna kazi kubwa sana kujisafisha mbele ya umma. Hakuna kitu kibaya km kuanzisha chama ambacho viongozi wake tayari wana kashfa na hawaaminiki mbele ya umma. maana yake badala ya kuanza na sera mbadala mnaanza na kujisafisha!
 
Mimi sio mtaalamu sana wa mambo ya uhasibu lakini nilishawahi kuambiwa na mtaalam mmoja wa mambo ya fedha kwamba mara nyingi taarifa za mapato na matamizi ya taasisi, hutolewa katika vipindi vya robo mwaka, nushu mwaka, robo tatu na mwaka.Sasa sijui kama alichokuwa ameniambia kilikuwa ni ukweli au laa! nadhani wataalam wa mambo ya uhasibu wanaweza kutusaidia ujuzi katika eneo hili, ila kama ilikuwa ni ukweli na kama ACT-Tanzania watakuwa wanafuata utaratibu huo wa kitaalam (kama itakuwa kweli ndivyo unavyotakiwa uwe), basi bila shaka wanaweza wakatoa baada ya kufikisha robo mwaka! pengine tusubiri kidogo halafu tuone kama ACT- Tanzania itafanya hivyo au laa!

Au una taarifa tofauti na hiyo, juu ya muda ambao taasisi hutakiwa kutoa taarifa zake za mapato na matumizi ili tuweze ku-share ujuzi?


Financial statements hutayarishwa kila Mwezi.

Lakini kunapokuwa na phase muhimu kama ya mchakato wa kusajili chama, ACT itajipatia credit kubwa iwapo itaweka wazi mambo yake.

Kuna nyuzi zilianzishwa kuulizia mambo ya pesa za ACT zikafutwa sijui sheria gani za JF haziruhusu kuhoji masuala ya fedha za ACT?
 
Naomba nikiri wazi kwamba NINA AKILI TIMAMU ( maana imeshasemwa ndani Ya uzi huu kwamba ukipinga usaliti basi huna akili ) KWAMBA SIUNGI MKONO ACT , KWA VILE MALENGO YAKE YANAFAHAMIKA NA KUJULIKANA .
 
Ndugu watanzania wote, tunawasalimu kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi.

Katika kusimamia dhana ya uwazi na kuhakikisha kwamba kila anayependa kupata taarifa mbali mbali kuhusu chama cha ACT-Tanzania, anazipata kikamilifu, kwa haraka, kwa ufanisi na bila usumbufu mkubwa, tunawaomba watanzania wote wanaopenda kupata taarifa mbali mbali za chama cha ACT- Tanzania, watutumie barua pepe zao au namba zao za simu.

ACT-Tanzania tunatumia na tutaendelea kutumia mbinu mbali mbali ili kujitahidi kuwafikia watanzania wengi iwezekanavyo (ikiwezekana watu wazima wote na wenye akili timamu), kwa haraka, kwa ufanisi, bila usumbufu mkubwa na kwa kujaribu kutumia njia ambazo ni za gharama nafuu zaidi.

Miongoni mwa mbinu ambazo baadhi tumeanza kuzitumia na tutakuwa tunazitumia kuwafikia watanzania ukiacha mikutano ya hadhara, ni pamoja na hii ya kupitia simu zenu, barua pepe zenu, tovuti ambayo tutaifungua karibuni, vitabu, vipeperushi (brochures), mitandao ya kijamii na kadhalika.Tutakuwa tukiboresha mifumo yetu ya mawasiliano kila mara kulingana na uwezo wetu ili watanzania waweze kuyafaidi matunda ya chama chao wakati wote.

NB. Kwa sasa kuna vijitabu vidogo (Brochures) tunagawa vinavyoeleza mambo muhimu yanayohusiana na ACT-Tanzania kwa muhtasari.Kama mtu anahitaji "soft copy", atatutumia e-mail yake na kama anataka "Hard Copy" atasubiria kidogo hadi tutakapoingia mtaani kwake.

ACT-Tanzania.................Taifa kwanza leo na kesho!,
Mabadiliko na Uwazi.........Chukua Hatua!.

Tuwasiliane kwa acttanzania@yahoo.com au acttanzania@gmail.com.

Pumbatupu@traitors.com
 
kweli kabisa ndugu, usiwape namba yako kabisa maana ukiwapa namba yako ya simu watakuibia simu yako, halafu ukiwapa parua pepe watakuibia E-mail yako. Yaani ni hatari sana! usikubali kabisa mkuu!

mimi sio muumini wa ACT ila napenda kitu anachokifanya betlehem. Tunaweza kuona kama anacheza ila anafanya kitu cha maana sana. Mkuu unajenga wala hubomoi.
 
hizi taarifa za ATC huwa nazisikia hapa tu, Hamjapewa bajeti ya kuzunguka bado?
 
Asante sana ACT kwa kuja kitofauti,nawatabiria makubwa katika siasa za Tanzania,itikadi yenu na falsafa ya kusimama upande wa wanyonge hakika ni jawabu kwa matatizo ya watanzania.

sasa watanzania wataamka na ACT,watashinda na ACT na watalala na ACT katoka simu na computer zao.

Chapeni kazi,ccm na chadema wapo kwaajili ya maslahi yao na familia zao.
 
Hiki chama mlichemka mlipoanza kujenga msingi wa uhalali wenu kwa ku-attack Chadema.

I am not a politician but I know one when I see one. Wote ni wale wale wenye njaa tuu.

Baadala ya kujenga hoja mnakuja na nyimbo zile zile zilizochoka za kuattack personalities. My point is, Chadema might be weak and a failure in its agenda (by the way, I dont agree with many of their approach to politics). Lakini hiyo haiwahusu. Kikubwa kwenu ni kuhakikisha wananchi wanaelewa mnachosimamia. Kusimama jukwaani na kuanza kuwatukana CHADEMA naona ni ukosefu wa fikra. Na I suspect you are simply marceneries paid to spoil things.

Mimi Masanja naona hiki chama ni reactionary. Just losers kwenye vyama vingine. Basically you are trying to show Chadema na wengineo kwamba na nyinyi mna chama kwa hiyo hata kama waliwafukuza..you can as well establish your own party. No roots. No values..simply to confuse us poor wananchi.

I will be pleasantly surprised if you prove me wrong.

Masanja

Kwanza naomba radhi kwa kufchelewa mada muimu sana kwangu
 
Asante kwa taarifa mkuu
Waache misukule iropoke na kupiga maneno ya kashfa nsicho wanacho juwa wao
 
nawapenda sana Act lakini kuna mambo yanantia shaka? Kwa nini mnashabikiwa sana na ccm? nyie ni chama cha upinzani kweli au mpo kuisadia ccm? halaf kwa nini viongozi wemu na baadhi ya mashabiki wenu ni wale waliofukuzwa chadema? viongozi wenu wataaminikaje wakati wana kashfa inayojulikana na watz karibia wote? ujingaaliyofanya Kitila umemwaibisha sana hata ya wasomi wenzake wamemshangaa na kutokuamini kitila anaweza kuwa so low.pmbona chama chemu hakionekani kimeanzishwa kwa nia njema? Mna kazi kubwa sana kujisafisha mbele ya umma. Hakuna kitu kibaya km kuanzisha chama ambacho viongozi wake tayari wana kashfa na hawaaminiki mbele ya umma. maana yake badala ya kuanza na sera mbadala mnaanza na kujisafisha!

Kuna mtu kasema ACT na CCM ni ndugu wa damu!
 
Back
Top Bottom