ACT- Tanzania: Taarifa kwa vyombo habari

ACT- Tanzania: Taarifa kwa vyombo habari

Abdull Kazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Posts
345
Reaction score
307
Kama mnavyo fahamu, Chama cha Wazalendo ACT-Tanzania kitafanya mkutano wake mkuu na uzinduzi wa chama mnamo tarehe 28 na 29 Machi 2015.

Katika mkutano Mkuu chama kitapitisha katiba mpya ya chama na kufanya uchaguzi wa nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Kiongozi wa chama, Mwenyekiti wa Chama, Makamu wenyeviti, Katibu Mkuu na Manaibu makatibu wakuu. Pia chama kitachagua wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu.

Katika Uzinduzi wa chama tarehe 29 Machi 2015 kuanzia saa tisa alasiri, viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wamealikwa.

ACT – Tanzania imemwalika Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti wa Taifa wa CUF kuzungumza kwa niaba ya vyama vya upinzani nchini kuhusu ' kwanini Tanzania bado ni nchi masikini na nini cha kufanya kuondoa umasikini'. Pia viongozi wote wa vyama vya siasa nchini, mabalozi wa nchi mbalimbali na wakuu wa asasi zisizo za kiserikali wamealikwa. Uzinduzi utaonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni na radio kadhaa hapa nchini.

Mheshimiwa Samia Nkrumah, Kiongozi wa Chama cha CPP cha Ghana na mtoto wa Rais wa kwanza wa Ghana Osagyefo Kwame Nkrumah amealikwa pamoja na Mheshimiwa Ababu Namwamba, Katibu Mkuu wa chama cha ODM cha Kenya na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Kenya. Vile vile ACT – Tanzania inatarajiwa kupata wageni kutoka vyama rafiki vya Ujerumani Die Linke na Umoja wa vyama vya mrengo wa kushoto Progressive Alliance.

Baada ya Uzinduzi ACT Tanzania itafanya mikutano ya hadhara nchi nzima kwa kuanzia na mikoa ya Arusha, Shinyanga, Tabora, Kigoma na Mbeya.

Tukiwa jijini Arusha ACT – Tanzania itahuisha Azimio la Arusha na kuelezea mwelekeo wa kisera wa chama katika kujenga Tanzania mpya yenye kufuata misingi Usawa, Uzalendo, Uwazi, Uwajibikaji, Demokrasia na Uadilifu.

Abdallah Khamis,
Afisa Habari

0777008686
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD]___________________________________________________________
P.O. Box 105043, House No. 203, Mpakani A Street, Kijiitonyama, Dar es salaam.
Tel: +255 22 277 1103, Mob: +255 763 463740 / 715 784670, Email: acttanzania@gmail.com
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
ACT-Wazalendo Kuandika historia Tanzania.

Hatimae Zimebaki siku Tatu Chama cha ACT-Wazalendo kifanyen uzinduzi wa chama,utakuwa uzinduzi wa kihistoria kutokana na wananchi wengi hasa wanyonge kuhamisika sana kuona chama chao kinaandika historia Mpya.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama pamoja na wanachana ,wapenzi na mashabiki wa chama wanaendelea kumiminika toka kila pembe ya Tanzania.

Mapokezi ni mazuri Mpaka sasa Zaidi ya viongozi na wanachama toka Mikoa 24 wameshatinga Jijini Dar es Salaam kwaajili ya kushiriki tukio hilo la Kihistori.

Pia Wageni Mbalimbali toka Nchi za Afrika,Amerika na Ulaya wanaendelea kuwasili kwaajili ya kushuhudia uzinduzi wa chama hapo tarehe 29-03-2015 ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Tuliahidi ,tumeweza na sasa tunasonga Mbele.

Karibu wote mshuhudie safari ya ukombozi ikianza rasmi.
 
mbona vyama rafiki ni kama vile vya chadema?
 
kulikuwa hakuna haja ya kutaja mmewaalika nan maana wanaweza wasifike hao mlio wataja
 
kulikuwa hakuna haja ya kutaja mmewaalika nan maana wanaweza wasifike hao mlio wataja

Wakati unafanya sanaa, by the way ukajamba itaunganishwa kwenye usanii husika.

Tunaendelea na kazi baachage bahangaike, bataishiaga kuvua migebuka
 
Sasa kama msemaji wa upinzani ni Mh lipumba. Mnasema mmealika na vyama vingine so wakaseme nn wakat jukumu hilo kapewa lip umba? Au tuje kula na kuondoka? Act achen kejeli bwanaa
 
Fahari ndio mama wa ujinga kutumia mamilioni kwa jambo kama hilo na kwa chama kichanga namna hiyo ni ufujaji mkubwa wa pesa

Ni sawa na kufunga harusi ya kifahari na ya gharama kubwa wakati maharusi hawana hata kibanda cha kuweka mbavu

Mkutano wa hiki chama utageuka kuwa kashfa kubwa ngoja tuwe na subra WAKATI SI MILELE
 
ACT-Wazalendo Kuandika historia Tanzania.

Hatimae Zimebaki siku Tatu Chama cha ACT-Wazalendo kifanyen uzinduzi wa chama,utakuwa uzinduzi wa kihistoria kutokana na wananchi wengi hasa wanyonge kuhamisika sana kuona chama chao kinaandika historia Mpya.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama pamoja na wanachana ,wapenzi na mashabiki wa chama wanaendelea kumiminika toka kila pembe ya Tanzania.

Mapokezi ni mazuri Mpaka sasa Zaidi ya viongozi na wanachama toka Mikoa 24 wameshatinga Jijini Dar es Salaam kwaajili ya kushiriki tukio hilo la Kihistori.

Pia Wageni Mbalimbali toka Nchi za Afrika,Amerika na Ulaya wanaendelea kuwasili kwaajili ya kushuhudia uzinduzi wa chama hapo tarehe 29-03-2015 ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Tuliahidi ,tumeweza na sasa tunasonga Mbele.

Karibu wote mshuhudie safari ya ukombozi ikianza rasmi.
Hiki kweli ni kishindo!
 
Nafasi ya :-

Kiongozi wa Chama ...Huyu ni supreme kwa mwenyekiti ??

Mwenyekiti ...Hiki ni cheo contravatial kwa kuwa Kadawi anakidai mahakamani ???

Otherwise it's seems ni gharama kubwa Sana zotatumika hasa kwa chama ambacho bado hakuna wanachama ...wa kutosha ....

Ukawa Wataathirika hapa ..?
 
Mbona ccm hawajalikwa... Na wengine Huwa wanawaalika...chama Tawala ..au WANAONA wanaonekana ...
 
Fahari ndio mama wa ujinga kutumia mamilioni kwa jambo kama hilo na kwa chama kichanga namna hiyo ni ufujaji mkubwa wa pesa

Ni sawa na kufunga harusi ya kifahari na ya gharama kubwa wakati maharusi hawana hata kibanda cha kuweka mbavu

Mkutano wa hiki chama utageuka kuwa kashfa kubwa ngoja tuwe na subra WAKATI SI MILELE

Marekebisho kidogo mkuu , hawana uwezo wa kufanya mkutano , ni kijiuzinduzi cha kizushi tu .
 
Eti sasa wanasonga mbele!!! Mnasonga mbele na usaliti wenu wa kutaka kuisambaratisha CHADEMA.

Fungua ukurasa mpya mkuu, wenzio hawana muda na chadema tena all they talk/write is about act. Ukiona mtu anamjadili mwanamke aliyemtimua (ni mfano tu) ujue bado anampenda
 
Wanaosifia ATC bila kuangalia kasoro ni vichwa maji, hata siku moja huwezi ukashabikia chama kinachoingia kuvuruga vyama pinzani kisa ngivu ya mtu mmoja, Zito anachofanya sasa hv kuwakomoa Chadema nakuruga mipango ya Ukawa hii haipo sawa kabisaaaaa...
 
Anaikomoaje CHADEMA?
Anavurugaje Mipango ya UKAWA? At least tuambieni na sisi tuelewe.
 
Back
Top Bottom