ACT-Tanzania na Msingi wa Utu

ACT-Tanzania na Msingi wa Utu

Hiki chama kina wanachama wawili tu, Kitila na Mwigamba hata mwenezi anaogopa kuandika jina lake.
 
Haka ni ka chama kanakosubiri kuzikwa kigoma kwa mara nyingine
 
ebu kuwa objective ndg,I know you are better than this.
 
Hiki chama kina wanachama wawili tu, Kitila na Mwigamba hata mwenezi anaogopa kuandika jina lake.

Na sasa cha ajabu zaidi ni kwamba pamoja na kuwa na wanachama wawili tu, kimepata usajili wa kudumu!? au pengine hii ni kwa sababu ya misingi yake! lakini kwani sheria inasema kwamba chama kikiwa na misingi mizuri, kisajiliwe hata kama kina wanachama wawili?
 
Mbona huu ni msingi mkuu wa NCCR? That means hamna jipya!!
 
Na sasa cha ajabu zaidi ni kwamba pamoja na kuwa na wanachama wawili tu, kimepata usajili wa kudumu!? au pengine hii ni kwa sababu ya misingi yake! lakini kwani sheria inasema kwamba chama kikiwa na misingi mizuri, kisajiliwe hata kama kina wanachama wawili?

Kwani msingi mzuri wa chama unatokana na kuuandika au kuufafanua jamii forum? Mbona CCM kina misingi mizuri sana, hata huo utu umeelezwa vizuri sana? It is one thing to have good plans on paper, but it is completely another to implement those good plans! Tatizo sio kwamba misingi mizuri haipo,hta kidogo! tatizo ni kwamba hatuitekelezi misingi hiyo. Sasa nyie wasaliti unaweza kujustify vipi misingi mizuri km haijaonekana in practice? Ni kipi mlichokifanya kuonesha kwamba nyie mnatekeleza misingi mizuri ya utu? Kwani nani anashindwa kunadika kwenye katiba yake kwamba chama au NGO yangu itazingatia misingi ya utu? Mbona katiba ya tanzania inazungumzia vizuri sana haki za binadamu lakini hazitekelezwi? Acheni blah blah nyie wasaliti!
 
haka ka chama kanawatoa povu sana mpaka mnaoana ndoa ya bila anwani wakati wapumbav.u nyie mnatapika maji taka na nyie ni buku 7 chadema makario nyie
 
Kama mwenezi alivyofafanua wakati inaonekana mwenezi na wewe ni mtu mmoja maana mawazo na akili zenu zinafanana...

hatufafanani mawazo wala akili,,,sema mawazo na akili zetu zinazingatia misingi mikuu ya chama chetu,,hivyo wanaACT popote tunaonekana ni mapacha.....vyama amabvyo havina misingi au hawaisimamii wanachama na viongozi wake kila mtu na rwake...

 
Wana ACT mnasemaje kuhusu kauli hii ya mwanachama wa ACT
ACT-Tanzania.
Ni kweli ACT- Tanzania inapambana na vyama vya upinzani.
Habari zenu wanajamii wa Tanzania?

Kuna hisia nyingi na za msingi zinazosambaa zikidhaniwa kuwa ni propaganda za msingi na mbinu za kisiasa au mbinu za kishabiki ingawa hazina viwango halisi.

Kumezoeleka wapinzani Tanzania kuzushiana majina na tuhuma feki na za kubuni ili tu wanaozusha hizo propaganda wapate upenyo wa kupigiwa makofi katika majukwaa ya kisiasa.

Kwa leo ngoja nianze kuwajibu wale wanaogopa na kuanza kujificha nyuma ya vivuli vya kigoda kwa kauli wadhaniazo ni propaganda au ushabiki wenye manufaa kwa vyama vyao kinyume cha ACT-Tanzania.

Hii sentenso ya kuwa ACT-Tanzania inapambana na vyama vya upinzani badala ya kupambana na ccm inatajwa sana japo, hawathibitishi ni wapi na lini mpambano huo umetangazwa, ila wanataja kama hisia zao tu kwa hofu ya kupitwa katika mbio ili kesho waepuke aibu ya kushindwa vibaya.

Ni kweli ACT-Tanzania ikiwa ni chama cha siasa kipya chenye malengo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na mengineyo hakiwezi kuyatimiza bila kutwaa dola, na ACT-Tanzania hakiwezi kutwaa dola toka mikono ya ccm bila kuwapora nguvu wapinzani waliotangulia na kufahamika mbele yake kwanza.

Kwa Tanzania sasa miongoni wa vyama vya siasa takribani 23 ACT-Tanzania ni chama kidogo kuliko vyote kwa maana ya upya wake na kutokuwa na mbunge, diwani wala kiongozi wa serikali za mitaa, hivyo kinashika nafasi ya chini kwa ukongwe wa vyama vilivyopo Tanzania.

Doctrine ya ushindani inakutaka uanze kushindana na mshindani unaelekeana nae au unaelingana nae uwezo, uzito na nguvu, kisha uwaze kushindana na wanaokuzidi uwezo ujaribu bahati yako labda utashinda.

Ni kama mashindano ya mbio mnapoanza mbio za kilomita 5 na mkiwa watu 5, mkiwa ndani ya km ya kwanza wenzio wamekutangulia, ukitaka kuwa mbele ya wenzako ni lazima upambane na mtu wa nne ili uweze kumvuka, kisha upambane na wa 3 kisha wa 2, kisha wa kwanza ushindane nae na hatimaye umshinde uwe mbele yao wote.

Kuwapita wote itategemea mwendo kasi wako, ikiwa wewe ni mvivu usiyeitazama nafasi ya kwanza basi utaishia kupambana na huyo wa size yako mpaka mwisho, na ikiwa unatazama nafasi ya kwanza ni lazima utapiga juhudi na kuifikia kwa malengo uliyojipangia.

Wakati wengine walianza kwamwendokasi kana kwamba wanakimbia mbio za kilomita 100 na sasa wanachoka ndipo unawavuka na kuichekelea nafasi ya kwanza.

ACT -Tanzania iko katika nafasi ya 23 kwa sasa, huku CCM ikiwa nafasi ya 1, CUF na CHADEMA wakifuatia, NCCR, TLP, UDP, ADC na vyama vingine vilivyoshiriki chaguzi mbali mbali viko mbele ya ACT -Tanzania.

Katika malengo ya ACT-Tanzania ya kiuchumi, kisiasa na kijamii tuliyoyanuwia hayawezi kutimia bila kushika dola,na mwenye aloshika dola ni CCM ambaye yuko mbele kilomita kadhaa, kutoka ccm mpaka chama chenye nafasi ya 22 sio mbali kiasi hicho ni kilomita kadhaa tu.

Pamoja na kuwa CCM haiko mbali na tulipo hatuwezi kupambana na asili ya ushindani, ni lazima tuanze kupamabana na aliye mbele yetu yaani chama chenye nafasi ya 22, 21.........3...2....kisha tupambane kuhitimisha kuindoa CCM ili tushike dola kusudi kuu liwe kutimiza lengo la uwepo wetu kama chama, yaani kutimiza malengo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa na mengineyo.

Wala msishangae mkiona tunawapita wote kwa kipindi kifupi na kumfikia CCM kwani nimeeleza kuwa inategemeana na mwendo kasi wa washindani, hivyo tegemeeni kuona tukiwabwaga mapema ili tuweze kumbwaga ccm, hatuwezi kuimwaga ccm kabla ya kuwamwaga wapinzani wenzetu walioshindwa kwa miaka zaidi ya 20 sasa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.

Hivyo wanaosambaza sentenso za kiuoga za kuwa ACT-Tanzania inapambana na upinzani wala hawakosei ni lazima tupambane nao ili tuwavuke tuweze kupambana kikamilifu na kumuondoa mtawala mkuu ccm ambaye sababu za kumuondoa zinajulikana ni zile zile zinazohubiriwa na wapinzani wote kila siku, lakini nia za kumuondoa ndizo hutofautiana miongoni mwetu, wapo wapinzani wajuzi sana kubwata na kubwatuka majukwaani kana kwamba wana nia hiyo ili hali ni wawinda upenyo tu wa kutimiza malengo yao binafsi.

Tuko tofauti kiitikadi, kifalsafa za vyama vyetu na hata majina ya vyama ni tofauti, na ndio sababu kila chama kinafanya siasa za kuwataka wananchi wakiunge mkono, wanaCHADEMA wanaoshangaa kuanzishwa kwa chama kipya, kwa nini hawashangai chadema kutoiunga mkono NCCR ambayo ilikuwa na nguvu sana miaka hiyo? (nimewataja chadema kwa sababu hawa wamekuwa mabingwa wa hizi propaganda)ili hali wao wakisahau huwa hawaamini katika upinzani bali wanaamini katika chadema tu kwa maana ya jina la chama, rejea kauli za mwenyekiti wa chadema mbowe 2010 aliposema hawezi shirikiana na tuvyama twa hovyo hovyo, kumbuka alipokataa kuunda kambi ya upinzani ya kushirikisha wapinzani wote, kumbuka juzi alivyowabagua tena TLP,UDP n.k.

TUNAPAMBANA NA KILA CHAMA KILICHOPO ILI WANAVYAMA WAO WATUUNGE MKONO ILI TUIONDOE CCM KIRAHISI MAANA VYAMA VYAO VIMESHINDWA KUIONDOA TANGU MWAKA 1992 MPAKA SASA WANAWAYAWAYA.
Tutapambana sio kwa matusi, bali kwa hoja, tutashindana kuwavuta watu sio kwa kashfa bali sera na falsafa yetu, tutawashughulikia wapinzani wetu sio kwa tindikali bali kwa kuwabomoa kwa hoja, hatimaye tutafika lengo.

Nyakarungu 2014
Mwana ACT-Tanzania, Mwanachama Mwandamizi.
+255 755 023 503
diplomatictable@gmail.com

 
Wana ACT mnasemaje kuhusu kauli hii ya mwanachama wa ACT

Mimi kwa maoni yangu nadhani alichokiandika kwa kiasi kikubwa kina mantiki. Vinginevyo pengine tungechambua ni wapi kapoteza mantiki katika andiko lake.
 
Nafikiri hii hoja bado ni valid ila utekelezaji wake unaweza kuathiriwa na jamii yenyewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom