Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,578
- 28,700
Nilijua mshakufa, kumbe bado mpo??
mimi najua neno moja 2 kuwa hili nigege la wasaka madaraka 2 basiNdugu watanzania wote kwa Ujumla, tunawasalimu kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi!
Ndugu watanzania wenzetu, pamoja na kuwa na vitu vingi sana duniani vyenye thamani kubwa sana; ni ukweli usiopingika kwamba hakuna kitu chenye thamani inayolingana wala inayokaribia kulingana na thamani ya 'Utu' wa Mtu.Mtu anapozaliwa mtu, anakuwa na thamani ya asili ambayo kwa namna yeyote ile ni lazima ifahamike, iheshimiwe, ilindwe kwa namna yeyote na kufanywa ionekane wakati wote katika jamii yetu.
Katika Misingi ya chama cha ACT-Tanzania, miongoni mwa misingi yake mikubwa ambayo chama kinaisimamia na kitaisimamia, kuilinda na kuitetea, ni pamoja na msingi wa Utu.
"ACT-Tanzania inaamini kuwa sera, mipango na shughuli zozote za kichama au za kiserikali zitakuwa hazina mafanikio ya kudumu kama hazitatambua, kuheshimu na kulinda utu wa kila Mtanzania. Ni kwa sababu hiyo tunu kuu itakayotuongoza katika utumishi wa umma ni kuheshimu, kutambua na kulinda utu wa kila mtu bila kujali tofauti zozote ambazo zinawatofautisha watu"
ACT-Tanzania tunatambua kuwa kuna tofauti nyingi zinazowatofautisha wanadamu.Kwa mfano kuna watu wengine masikini wengine matajiri, wengine wazima wengine walemavu.Vile vile tunafahamu vyema kwamba katika jamii yeyote ni lazima watu wawe na tofauti za kimtizamo; hivyo basi hata katika jamii yetu, tofauti za kimtizamo ni lazima.Hata hivyo ACT-Tanzania inaamini kwamba hakuna tofauti yeyote inayoweza kuhalalisha au kuwa ndio sababu ya kutotambua na kuheshimu utu wa mtu kama vile inavyopaswa.
ACT-Tanzania inaamini kwamba pamoja na tofauti za kisiasa miongoni mwa watu na vyama, ni lazima siasa hizo ziweke mbele msingi wa utu kama nguzo mama ya siasa za msingi, hivyo kuzifanya shughuli zote za kisiasa ziende katika misingi ya ustaarabu na ubinadamu na tofauti zibaki katika sera na itikadi.
Hata hivyo ACT-Tanzania inatambua juu ya uwepo wa idadi kubwa ya watu katika jamii zetu ambao kwa sababu za kisiasa wanaweza ama kupoteza utu wao au kuchezea na kutolinda wala kujali utu wa watu wengine , ili kupata maslahi fulani ya kisiasa.ACT-Tanzania inaamini kwamba jamii hujengwa, na hali hiyo inaweza kubadilishwa taratibu taratibu kwa chama, wanachama, wadau na watanzania wote waliostaarabika kutoa elimu kwa jamii zilizowazunguka kwa nadharia na vitendo na hilo ndilo ambalo chama cha ACT-Tanzania kinalifanya.
Mwisho, Kimsingi jamii inapaswa kufahamu kwamba thamani ya kitu chochote duniani hupatikana kutokana na uwepo wa watu,na watu huwa watu kwa sababu ya hadhi ya utu wao.Hivyo ni jukumu letu sote kuulinda na kuuhifadhi utu wetu na utu wa wawatanzania wenzetu kwa ujumla kwa maslahi ja jamii ya mwanadamu kwa ujumla.Tukiweza kufanya hivyo, itakuwa ni rahisi sasa kupata maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kujenga jamii ya watanzania wenye furaha kama kinavyodhamiria chama chetu.
Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa ajili ya Taifa la leo na kesho!
ACT-Tanzania tumedhamiria na bila shaka Mungu atatusaidia!
**********************************************Tutakuwa tukiitolea ufafanuzi Misingi ya Chama cha ACT-Tanzania, mmoja baada ya mwingine kwa kadiri ya uwezo wetu na kwa kutumia mbinu zozote tutakazoweza hadi itakapoeleweka kwa watu wazima wote na wenye akili timamu kwani chama chochote kile bora hujengwa na misingi kwanza.Kwa kuwa kila mtu ana wajibu katika nchi yake; nawe utakuwa umefanya jambo la maana kwa kutuunga mkono kwa kuifundisha misingi hii katika jamii yako.
Nilijua mshakufa, kumbe bado mpo??
pengine ndio maana kinasimamia misingi ikiwemo huu wa Utu.mimi najua neno moja 2 kuwa hili nigege la wasaka madaraka 2 basi
ulikuwa unamaanisha neno utu wanrifaa propaganda za kijinga walizokuwa wanafanya watu kwa msiba uliotokea kama ni hivyo kweli watakuwa mabogasi....................
betlehem nimependa unavyowajibu hawa wahuni wa ufipa nendanao taratibu wataelewa somo.ungependa wafe eh! ok! watakufa tu hamna shida.wala usiwe na wasiwasi,wewe Endelea kuomba tu mkuu! kuna siku maombi yatakubaliwa.
Ndugu,
Kwa faida yako na faida ya Watanzania wote,
Ufafanuzi ufuatao unaweza kufaa kwa kila mwenye kutaka kufahamu.
Tunapenda kukufahamisha kwamba elimu hutolewa kokote kwa njia yeyote, la msingi ni kuhakikisha inafikia watu.Ni bora kokote unapoona elimu nzuri ukaichukua, ukaifanyia kazi na kuwafikishia wenzako na unapoona elimu mbaya kokote kuiacha na kukemea.Kadhalika unapoona jambo lolote jema mahali popote, ni bora ukalichukua na kuwafikishia wenzako na ukiona baya basi ukaliacha na kulikemea. Kwa kufanya hivyo utakuwa umetimiza wajibu wako kama binadamu, mzalendo na mtu unayeijenga nchi yako.Kinyume chake utakuwa umeamua kutokuwajibika kana kwamba hauna wajibu katika jamii yako.
Kuhusu aina ya mawasiliano ambayo Chama kinatumia kuwafikia wananchi, zipo nyingi kulingana na mazingira na uwezekano kwa wakati husika na aina ya watu wanaolengwa.Tunaweza kukutajia baadhi na kama nawe au mtanzania yeyote atakuwa na njia ya ziada nzuri inayoweza kutusaidia kuifundisha misingi ya chama chetu na kuwafikia watu wengi zaidi na wakaielewa; basi litakuwa ni jambo jema na la kushukuriwa.
Chama kinawasiliana na mtanzania mmoja mmoja kupitia mkakati maalum.Kama bado wewe hujafikiwa; ni suala la muda tu utafikiwa.Chama kitaanza kufanya mikutano ya hadhara karibuni.Kama eneo lako litakuwa ni miongoni mwa maeneo ambayo yatafikiwa, unashauriwa kuhudhuria na kuwashauri wenzako kuhudhuria vile vile.Kadhalika chama kimeanza kusambaza vitabu vidogo vinavyoeleleza na kufafanua mambo ya msingi yanayo husu chama.Kama hujafanikiwa kupata, basi utapata karibuni na ukifanikiwa kukipata kijitabu hicho, kisome kwa makini na ukiweza mpatie na mwenzako.
Kama mtu yeyote ana ushauri juu ya njia nzuri zaidi tunazoweza kuzitumia ili kuwafikia watanzania wote kwa wepesi zaidi, gharama nafuu zaidi, kwa haraka zaidi, kwa ufanisi zaidi na wakatuelewa zaidi ; basi litakuwa ni jambo jema sana.
Ikumbukwe kuwa ujenzi wa nchi yetu hii, ni jukumu letu sote, hivyo tushirikianeni ili kuifanya Tanzania kuwa eneo bora zaidi la kuishi na kuwafanya wananchi wake wawe na furaha zaidi.
Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa taifa la leo na kesho!
Kule duru za siasa tumeongelea jinsi ambavyo chama hiki kinaanza kwa matatizo.https://www.jamiiforums.com/great-t...a-cha-act-mpini-wa-ccm-kumaliza-upinzani.htmlNdugu watanzania wote kwa Ujumla, tunawasalimu kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi!
Ndugu watanzania wenzetu, pamoja na kuwa na vitu vingi sana duniani vyenye thamani kubwa sana; ni ukweli usiopingika kwamba hakuna kitu chenye thamani inayolingana wala inayokaribia kulingana na thamani ya 'Utu' wa Mtu.Mtu anapozaliwa mtu, anakuwa na thamani ya asili ambayo kwa namna yeyote ile ni lazima ifahamike, iheshimiwe, ilindwe kwa namna yeyote na kufanywa ionekane wakati wote katika jamii yetu.
Katika Misingi ya chama cha ACT-Tanzania, miongoni mwa misingi yake mikubwa ambayo chama kinaisimamia na kitaisimamia, kuilinda na kuitetea, ni pamoja na msingi wa Utu.
"ACT-Tanzania inaamini kuwa sera, mipango na shughuli zozote za kichama au za kiserikali zitakuwa hazina mafanikio ya kudumu kama hazitatambua, kuheshimu na kulinda utu wa kila Mtanzania. Ni kwa sababu hiyo tunu kuu itakayotuongoza katika utumishi wa umma ni kuheshimu, kutambua na kulinda utu wa kila mtu bila kujali tofauti zozote ambazo zinawatofautisha watu"
ACT-Tanzania tunatambua kuwa kuna tofauti nyingi zinazowatofautisha wanadamu.Kwa mfano kuna watu wengine masikini wengine matajiri, wengine wazima wengine walemavu.Vile vile tunafahamu vyema kwamba katika jamii yeyote ni lazima watu wawe na tofauti za kimtizamo; hivyo basi hata katika jamii yetu, tofauti za kimtizamo ni lazima.Hata hivyo ACT-Tanzania inaamini kwamba hakuna tofauti yeyote inayoweza kuhalalisha au kuwa ndio sababu ya kutotambua na kuheshimu utu wa mtu kama vile inavyopaswa.
ACT-Tanzania inaamini kwamba pamoja na tofauti za kisiasa miongoni mwa watu na vyama, ni lazima siasa hizo ziweke mbele msingi wa utu kama nguzo mama ya siasa za msingi, hivyo kuzifanya shughuli zote za kisiasa ziende katika misingi ya ustaarabu na ubinadamu na tofauti zibaki katika sera na itikadi.
Hata hivyo ACT-Tanzania inatambua juu ya uwepo wa idadi kubwa ya watu katika jamii zetu ambao kwa sababu za kisiasa wanaweza ama kupoteza utu wao au kuchezea na kutolinda wala kujali utu wa watu wengine , ili kupata maslahi fulani ya kisiasa.ACT-Tanzania inaamini kwamba jamii hujengwa, na hali hiyo inaweza kubadilishwa taratibu taratibu kwa chama, wanachama, wadau na watanzania wote waliostaarabika kutoa elimu kwa jamii zilizowazunguka kwa nadharia na vitendo na hilo ndilo ambalo chama cha ACT-Tanzania kinalifanya.
Mwisho, Kimsingi jamii inapaswa kufahamu kwamba thamani ya kitu chochote duniani hupatikana kutokana na uwepo wa watu,na watu huwa watu kwa sababu ya hadhi ya utu wao.Hivyo ni jukumu letu sote kuulinda na kuuhifadhi utu wetu na utu wa wawatanzania wenzetu kwa ujumla kwa maslahi ja jamii ya mwanadamu kwa ujumla.Tukiweza kufanya hivyo, itakuwa ni rahisi sasa kupata maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kujenga jamii ya watanzania wenye furaha kama kinavyodhamiria chama chetu.
Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa ajili ya Taifa la leo na kesho!
ACT-Tanzania tumedhamiria na bila shaka Mungu atatusaidia!
**********************************************Tutakuwa tukiitolea ufafanuzi Misingi ya Chama cha ACT-Tanzania, mmoja baada ya mwingine kwa kadiri ya uwezo wetu na kwa kutumia mbinu zozote tutakazoweza hadi itakapoeleweka kwa watu wazima wote na wenye akili timamu kwani chama chochote kile bora hujengwa na misingi kwanza.Kwa kuwa kila mtu ana wajibu katika nchi yake; nawe utakuwa umefanya jambo la maana kwa kutuunga mkono kwa kuifundisha misingi hii katika jamii yako.
Ndugu, Mi sielewi hapa hii Tz inaelekea wapi!? Watu wanakuja na maneno wasiyojua hata maana yake!!
Kama sikosei hili ni bandiko lao la kwanza kuhusu MISINGI ya chama, iweje waanze na msingi wa UTU ambao tangu mateso ya Mama yetu pale MOI hadi umauti ccm walikuwa wamevalia njuga, na Misingi ipo mingi lakini eti wamechagua UTU!!?
Wanatuhubiria UTU wakati huo huo wanakiuka UTU kwa Mama yetu!!? Au wanatufanya hamnazo!?
betlehem nimependa unavyowajibu hawa wahuni wa ufipa nendanao taratibu wataelewa somo.
Jana hamkuonekana kwenye maziko Kigoma
Nyie mtakuwa kama kile chama cha sijui CCK au sijui CCJ.
Mtakufa karibuni tu.
Nguruvi3Kule duru za siasa tumeongelea jinsi ambavyo chama hiki kinaanza kwa matatizo.https://www.jamiiforums.com/great-t...a-cha-act-mpini-wa-ccm-kumaliza-upinzani.html
Ukisoma kwa juu juu sana, unaweza kudhani hawa jamaa wanaanza kueneza sera au taratibu zao.Hapo mwisho anasema ''Tutakuwa tukitolea ufafanuzi misingi ya chama....' ili kuwafumba watu macho kwa kile walichodhamiria.
Sina tatizo na maoni yao au misimamo yao. Wana haki ya kueleza na kujieleza katika jamii na hilo si kosa.
Tatizo ninaloliona kwa ACT ni wao kusema ni wa WAZI wakati amabapo wanawafanya Watanzania wapuuzi na mazuzu.
Hapa ndipo ninaposimamia.
Mada yote hiyo haizungumzii misingi ya ACT, kinachozungumziwa ni tukio la msiba la 'mwanachama' wa ACT na tofauti za kisiasa zilizojitokeza miongoni mwa mfiwa na wanasiasa wa chama chake. Hapo ndipo nasema hakukuwa na sababu za kuzunguka na kuwafanya watu wajinga.
ACT wangeweza kusema Zitto kafiwa na mama yake na viongozi kadhaa hawakuhudhria. Straight foward na hilo lisingekuwa tatizo kwasababu wanatoa maoni yao na wana haki hiyo.
Walichokifanya si uwazi, ni kutaka kutufanya mazuzu. Hiki chama nimesema kimeanza na matatizo makubwa ya kuwa na kitu kinachoitwa 'PR'. Mahusiano katika jamii ni jambo muhimu sana. Haionekani kama wana hicho kitu katika chama chao.
ACT katika wakati huu ingejiepusha sana na mizozo au sintofahamu ikizingatiwa kuwa viongozi wake wamebeba mafurushi machafu migongoni mwao. Wana bifu na sehemu ya jamii na ili kuondoa sintofahamu na kutoa nafasi kwa chama kujieneza, ACT wanapaswa kujikita katika siasa na si migongano isiyo na tija.
ACT wanapokuwa na mambo rahisi au majitaka namna hii, hata siku watakapoeleza jambo la maana litatiliwa shaka kwasababu hawasimami katika misingi na kauli mbiu ya chama chao, UWAZI
Ningewaelewa kama mngetoka na ku-criticise CDM moja kwa moja. Pengine tungekuwa tunawaunga mkono kwa mambo mawili, moja,uwazi wenu na pili mada yenu. Huo ndio ukomavu.
Hizi siasa za Waraka zime prove kuwa failure kubwa, hamuonekani kujifunza.
Please go back to the drawing board. Mnafanya siasa za mwaka 1905. Kinjekitile anaonekana smart zaidi yenu.
UWAZI wenu upo wapi? Mtaendelea na siasa za kujificha ficha hadi lini? kwanini mnazidhulumu nafsi zenu kuongea, mkibana punzi na kuongelea matumboni?
Ndio kaka, hujawasoma in between the lines, si umesikia wakisema chadema hawana utu, sijui hawakwenda kumwona mgonjwa sijui hawakwenda msibani, na hawa jamaa wakaja na bandiko lao hapa eti kujionesha kwamba wao wana msingi wa utu! Utu gani huo? Wangekuwa na utu wangemdhalilisha Mbowe kiasi kile kwenye waraka wao wa siri? Kiongozi wao Zitto angemtukana mwenyekeiti wake?
mkuu mbona leo hujanitukana aiseee!?
chama cha mitandao ya jamii, sound nyingi kuliko utekelezaji... hata bendera sijawahi ona, huwa nakiona jf tu...
Jana hamkuonekana kwenye maziko Kigoma
bandiko halijataja chama chochote cha siasa zaidi ya ACT-TANZANIA,, ni ujahili si kama wazimu kuingiza mambo ya misiba na mambo ya vyama vingine katika bandiko ambalo maudhui yake hayahusiani na mambo hayo...pamoja na hayo,,kama kuna vyma havitambui "utu" wa mtu hilo ni tatizo la hivyo vyama na si tatizo la misingi ya ACT-TANZANIA ambayo kila mwana ACT inabidi aape kuiilinda.