ACT-Tanzania na Msingi wa Utu

ACT-Tanzania na Msingi wa Utu

Hahaha hiki nacho ni chama kumbe.....!!!!!!!!! Stupidity mnafikiri kuwa na utitiri wa vyama ndio democracy....
 
Machadema bana ha ha ha mbona povu linawatoka hivyo kwa chama kichanga kama ACT je CCM mtaiweza kweli hali yakuwa ACT inawameza taratibu?? Ha ha ha Kweli Chagadema cha babu majanga na DJ Marienge
 
Machadema bana ha ha ha mbona povu linawatoka hivyo kwa chama kichanga kama ACT je CCM mtaiweza kweli hali yakuwa ACT inawameza taratibu?? Ha ha ha Kweli Chagadema cha babu majanga na DJ Marienge
Mkuu Ally Kanah , hivi kuna nini cha kumfanya mtu atukane kwenye uzi huu? kwa kweli inasikitisha ila mimi siku hizi sina mengi ya kusema, ninachosisitiza kila siku ni kwamba "na tufanye tufanyalo, ila tujue tu kwamba mwisho wa ubaya aibu!"

Kadhalika nakusihi kama unakusudia "CHADEMA" Usiwaite "CHAGADEMA" vinginevyo labda kama unakusudia kitu kingine.Hata ukiona unafanyiwa ubaya, jitahidi kulipiza wema tu! japo ni kazi ngumu kufanya hivyo na inahitaji moyo thabiti ila wale wenye moyo na kifua ndio wanaoweza kuwa viongozi wema na bora, hivyo jilazimishe kujijenga katika tabia hiyo huenda baadae ukawa kiongozi mzuri na ukasaidia sana.
 
Baada ya msiba na propaganda za kipumbavu toka Lumumba, leo ACT wanakuja na propaganda ileile chini ya kuvuli cha UTU!!!!

Sijui Mh. Zitto anajisikiaje akiona kifo cha Mama'ke kinakuwa mtaji wa siasa na yeye anakaa kimya namna hii!!!??

Kwahiyo pia ACT mnataka kutuambia kwamba UTU ni kutumia vifo kama mtaji!? Mbona kabla ya kifo cha Mama yetu mlikuwa hamjaja na hizi drama uchwara za utu!!??
 
AciT-Tanzania kutegemea msiba ili muonekane ni chama mnajidanganya nyie mnajulikana ni Yuda Branch hamna hata tone la utu kama natania someni na kutafakari kazi zenu.
1.Masalia program
2.P7
3.Riporti ya uchunguzia
4.Waraka wa ki M1,M2 ndo utajua ushetani unavyoigiza una utu
 
Ndugu Mwisho wa ubaya aibu! haya!


Ndugu, Mi sielewi hapa hii Tz inaelekea wapi!? Watu wanakuja na maneno wasiyojua hata maana yake!!

Kama sikosei hili ni bandiko lao la kwanza kuhusu MISINGI ya chama, iweje waanze na msingi wa UTU ambao tangu mateso ya Mama yetu pale MOI hadi umauti ccm walikuwa wamevalia njuga, na Misingi ipo mingi lakini eti wamechagua UTU!!?

Wanatuhubiria UTU wakati huo huo wanakiuka UTU kwa Mama yetu!!? Au wanatufanya hamnazo!?
 
Naona betlehem anatumia id's zake zote mbili. Moja inaposti ingine inalike interchangeably.

Fun huh!
 
Naona betlehem anatumia id's zake zote mbili. Moja inaposti ingine inalike interchangeably.

Fun huh!

katika uzi huu, wewe ulichoona cha kujadili ni betlehem? ok sawa! maana waswahili husema akili ni nywele nyembamba........
Ila mwisho wa ubaya.......!
 
Ndugu, Mi sielewi hapa hii Tz inaelekea wapi!? Watu wanakuja na maneno wasiyojua hata maana yake!!

Kama sikosei hili ni bandiko lao la kwanza kuhusu MISINGI ya chama, iweje waanze na msingi wa UTU ambao tangu mateso ya Mama yetu pale MOI hadi umauti ccm walikuwa wamevalia njuga, na Misingi ipo mingi lakini eti wamechagua UTU!!?

Wanatuhubiria UTU wakati huo huo wanakiuka UTU kwa Mama yetu!!? Au wanatufanya hamnazo!?

mkuu kama hueleweki vizuri! unasema ACT-Tanzania ina misingi mingi, hebu tuambie iko mingapi!, itaje!, na utuambie wewe umeiona wapi?
 
Kama ACT ingalikuwa na watu makini,ingeshakataa support ya ccm.
Vinginevyo,tunashindwa kuwatofautisha!
 
Kama ACT ingalikuwa na watu makini,ingeshakataa support ya ccm.
Vinginevyo,tunashindwa kuwatofautisha!

huwa inasapotiwa na ccm!?na support hiyo inahusiana na misingi ya ACT-Tanzania, na hasa huu msingi wa utu unaojadiliwa hapa !?leo?
 
mkuu kama hueleweki vizuri! unasema ACT-Tanzania ina misingi mingi, hebu tuambie iko mingapi!, itaje!, na utuambie wewe umeiona wapi?


Ni wapi hunielewi!? Kwani hili group la wasariti lina msingi mmoja tu wa UTU!? Rejea mada kuu uliyopost, inasema "tutakuwa tunafafanua 'MISINGI' ya chama chetu kwa kadri tutakavyoweza". Au umesahau hata uliyoyaandika mwenyewe?
 
😛uke:😛uke:😛uke:

ACT = CCM's Left hand

Hivi CCM ni left party! na ACT-Tanzania ni left vile vile? kama ndio hivyo, vitakuwa vinafanana.Lakin hivi wewe unaipinga ccm kwa kuwa ni left? halaf kumbe vyama vya left ndio vyenye msingi wa utu!? ok sawa.
 
View attachment 162302
UTU WA MTU NI WA THAMANI ZAIDI YA CHOCHOTE KILE.

Ndugu watanzania wote kwa Ujumla, tunawasalimu kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi!

Ndugu watanzania wenzetu, pamoja na kuwa na vitu vingi sana duniani vyenye thamani kubwa sana; ni ukweli usiopingika kwamba hakuna kitu chenye thamani inayolingana wala inayokaribia kulingana na thamani ya 'Utu' wa Mtu.Mtu anapozaliwa mtu, anakuwa na thamani ya asili ambayo kwa namna yeyote ile ni lazima ifahamike, iheshimiwe, ilindwe kwa namna yeyote na kufanywa ionekane wakati wote katika jamii yetu.

Katika Misingi ya chama cha ACT-Tanzania, miongoni mwa misingi yake mikubwa ambayo chama kinaisimamia na kitaisimamia, kuilinda na kuitetea, ni pamoja na msingi wa Utu.

"ACT-Tanzania inaamini kuwa sera, mipango na shughuli zozote za kichama au za kiserikali zitakuwa hazina mafanikio ya kudumu kama hazitatambua, kuheshimu na kulinda utu wa kila Mtanzania. Ni kwa sababu hiyo tunu kuu itakayotuongoza katika utumishi wa umma ni kuheshimu, kutambua na kulinda utu wa kila mtu bila kujali tofauti zozote ambazo zinawatofautisha watu"

ACT-Tanzania tunatambua kuwa kuna tofauti nyingi zinazowatofautisha wanadamu.Kwa mfano kuna watu wengine masikini wengine matajiri, wengine wazima wengine walemavu.Vile vile tunafahamu vyema kwamba katika jamii yeyote ni lazima watu wawe na tofauti za kimtizamo; hivyo basi hata katika jamii yetu, tofauti za kimtizamo ni lazima.Hata hivyo ACT-Tanzania inaamini kwamba hakuna tofauti yeyote inayoweza kuhalalisha au kuwa ndio sababu ya kutotambua na kuheshimu utu wa mtu kama vile inavyopaswa.

ACT-Tanzania inaamini kwamba pamoja na tofauti za kisiasa miongoni mwa watu na vyama, ni lazima siasa hizo ziweke mbele msingi wa utu kama nguzo mama ya siasa za msingi, hivyo kuzifanya shughuli zote za kisiasa ziende katika misingi ya ustaarabu na ubinadamu na tofauti zibaki katika sera na itikadi.

Hata hivyo ACT-Tanzania inatambua juu ya uwepo wa idadi kubwa ya watu katika jamii zetu ambao kwa sababu za kisiasa wanaweza ama kupoteza utu wao au kuchezea na kutolinda wala kujali utu wa watu wengine , ili kupata maslahi fulani ya kisiasa.ACT-Tanzania inaamini kwamba jamii hujengwa, na hali hiyo inaweza kubadilishwa taratibu taratibu kwa chama, wanachama, wadau na watanzania wote waliostaarabika kutoa elimu kwa jamii zilizowazunguka kwa nadharia na vitendo na hilo ndilo ambalo chama cha ACT-Tanzania kinalifanya.

Mwisho, Kimsingi jamii inapaswa kufahamu kwamba thamani ya kitu chochote duniani hupatikana kutokana na uwepo wa watu,na watu huwa watu kwa sababu ya hadhi ya utu wao.Hivyo ni jukumu letu sote kuulinda na kuuhifadhi utu wetu na utu wa wawatanzania wenzetu kwa ujumla kwa maslahi ja jamii ya mwanadamu kwa ujumla.Tukiweza kufanya hivyo, itakuwa ni rahisi sasa kupata maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kujenga jamii ya watanzania wenye furaha kama kinavyodhamiria chama chetu.

Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa ajili ya Taifa la leo na kesho!
ACT-Tanzania tumedhamiria na bila shaka Mungu atatusaidia!



**********************************************
Tutakuwa tukiitolea ufafanuzi Misingi ya Chama cha ACT-Tanzania, mmoja baada ya mwingine kwa kadiri ya uwezo wetu na kwa kutumia mbinu zozote tutakazoweza hadi itakapoeleweka kwa watu wazima wote na wenye akili timamu kwani chama chochote kile bora hujengwa na misingi kwanza.Kwa kuwa kila mtu ana wajibu katika nchi yake; nawe utakuwa umefanya jambo la maana kwa kutuunga mkono kwa kuifundisha misingi hii katika jamii yako.


Naomba elimu kuhusu hichi chama, hivi wanzilishi wake wametokea sayari ya Mars au ni waswahili wenzetu? Sasa kama ni waswahili wenzetu wanajitofautisha vipi na viongozi wa vyama utitiri tulivyonavyo kwa sasa? Je wamewahi kuwa wanachama wa chama chochote cha kisiasa? Naomba kiongozi yeyote wa ACT-Tanzania anipe ufafanuzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom