ACT-Tanzania na Msingi wa Utu

ACT-Tanzania na Msingi wa Utu

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
643
Reaction score
1,603
Utu wa mtu ni zaidi.jpg
UTU WA MTU NI WA THAMANI ZAIDI YA CHOCHOTE KILE.

Ndugu watanzania wote kwa Ujumla, tunawasalimu kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi!

Ndugu watanzania wenzetu, pamoja na kuwa na vitu vingi sana duniani vyenye thamani kubwa sana; ni ukweli usiopingika kwamba hakuna kitu chenye thamani inayolingana wala inayokaribia kulingana na thamani ya 'Utu' wa Mtu.Mtu anapozaliwa mtu, anakuwa na thamani ya asili ambayo kwa namna yeyote ile ni lazima ifahamike, iheshimiwe, ilindwe kwa namna yeyote na kufanywa ionekane wakati wote katika jamii yetu.

Katika Misingi ya chama cha ACT-Tanzania, miongoni mwa misingi yake mikubwa ambayo chama kinaisimamia na kitaisimamia, kuilinda na kuitetea, ni pamoja na msingi wa Utu.

"ACT-Tanzania inaamini kuwa sera, mipango na shughuli zozote za kichama au za kiserikali zitakuwa hazina mafanikio ya kudumu kama hazitatambua, kuheshimu na kulinda utu wa kila Mtanzania. Ni kwa sababu hiyo tunu kuu itakayotuongoza katika utumishi wa umma ni kuheshimu, kutambua na kulinda utu wa kila mtu bila kujali tofauti zozote ambazo zinawatofautisha watu"

ACT-Tanzania tunatambua kuwa kuna tofauti nyingi zinazowatofautisha wanadamu.Kwa mfano kuna watu wengine masikini wengine matajiri, wengine wazima wengine walemavu.Vile vile tunafahamu vyema kwamba katika jamii yeyote ni lazima watu wawe na tofauti za kimtizamo; hivyo basi hata katika jamii yetu, tofauti za kimtizamo ni lazima.Hata hivyo ACT-Tanzania inaamini kwamba hakuna tofauti yeyote inayoweza kuhalalisha au kuwa ndio sababu ya kutotambua na kuheshimu utu wa mtu kama vile inavyopaswa.

ACT-Tanzania inaamini kwamba pamoja na tofauti za kisiasa miongoni mwa watu na vyama, ni lazima siasa hizo ziweke mbele msingi wa utu kama nguzo mama ya siasa za msingi, hivyo kuzifanya shughuli zote za kisiasa ziende katika misingi ya ustaarabu na ubinadamu na tofauti zibaki katika sera na itikadi.

Hata hivyo ACT-Tanzania inatambua juu ya uwepo wa idadi kubwa ya watu katika jamii zetu ambao kwa sababu za kisiasa wanaweza ama kupoteza utu wao au kuchezea na kutolinda wala kujali utu wa watu wengine , ili kupata maslahi fulani ya kisiasa.ACT-Tanzania inaamini kwamba jamii hujengwa, na hali hiyo inaweza kubadilishwa taratibu taratibu kwa chama, wanachama, wadau na watanzania wote waliostaarabika kutoa elimu kwa jamii zilizowazunguka kwa nadharia na vitendo na hilo ndilo ambalo chama cha ACT-Tanzania kinalifanya.

Mwisho, Kimsingi jamii inapaswa kufahamu kwamba thamani ya kitu chochote duniani hupatikana kutokana na uwepo wa watu,na watu huwa watu kwa sababu ya hadhi ya utu wao.Hivyo ni jukumu letu sote kuulinda na kuuhifadhi utu wetu na utu wa wawatanzania wenzetu kwa ujumla kwa maslahi ja jamii ya mwanadamu kwa ujumla.Tukiweza kufanya hivyo, itakuwa ni rahisi sasa kupata maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kujenga jamii ya watanzania wenye furaha kama kinavyodhamiria chama chetu.

Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa ajili ya Taifa la leo na kesho!
ACT-Tanzania tumedhamiria na bila shaka Mungu atatusaidia!



**********************************************
Tutakuwa tukiitolea ufafanuzi Misingi ya Chama cha ACT-Tanzania, mmoja baada ya mwingine kwa kadiri ya uwezo wetu na kwa kutumia mbinu zozote tutakazoweza hadi itakapoeleweka kwa watu wazima wote na wenye akili timamu kwani chama chochote kile bora hujengwa na misingi kwanza.Kwa kuwa kila mtu ana wajibu katika nchi yake; nawe utakuwa umefanya jambo la maana kwa kutuunga mkono kwa kuifundisha misingi hii katika jamii yako.

 
RIP CCJ .......ACT kumbe bado mpo mpo.......:A S 13:
 
Haka ka chama ndo kameingia chaka kabsaaa! bora mngekafanya kachama ka warina asali angalau kangesaundi!
thread ndeeefu, povu lenyewe uharo mtupu, bt mna roho ngumu..
 
Yaani mnafafnua msingi ya chama jamii forums? Kwa nini msifanye mikutano ya wazi mkawaambia wananchama wenu hayo mambo yenu km mnao? Nyie ACT na CCM mnataka kutumia msiba kujiongezea point lakini sio jambo zuri hata kidogo!
 
CCM wana tendency ya kukutumia na kukutupa, wewe kama unadhani watakupa nafasi ya kuota mapembe naomba usahau

ndio akili kubwa hawa bana na ndio thread ya akili kubwa
 
Yaani mnafafnua msingi ya chama jamii forums? Kwa nini msifanye mikutano ya wazi mkawaambia wananchama wenu hayo mambo yenu km mnao? Nyie ACT na CCM mnataka kutumia msiba kujiongezea point lakini sio jambo zuri hata kidogo!
ulikuwa unamaanisha neno utu wanrifaa propaganda za kijinga walizokuwa wanafanya watu kwa msiba uliotokea kama ni hivyo kweli watakuwa mabogasi....................
 
Sidhani kama watu wapo kwenye mood ya kusikiliza sera za chama kipya wakati huu wa utungwaji wa katiba mpya. Ujio wa chama hiki umekuwa na timing mbovu.
 
Nilichogundua cdm wanaiogopa sana act kuliko wanavyoiogopa ccm
 
Duh, hawa wamesha jichanganya shenz type. Yaani chama kimejikita katika misngi ya kidhanifu hivi. Wataweza kupanga chochote kweli?
 
Act mko kwenye kikao Mwandiga saizi? maana naona timu ya wote waliofukuzwa Chadema mmejaa Kigoma kwa sasa.

Mbona kwenye msiba wa raia wasiokuwa na hatia uliofanywa na washirika wenu ccm pale Arusha hamkurundikana kama mlivyolundikana saizi Kigoma????

Tafakarini sana.
 
chama cha mitandao ya jamii, sound nyingi kuliko utekelezaji... hata bendera sijawahi ona, huwa nakiona jf tu...
 
Yaani mnafafnua msingi ya chama jamii forums? Kwa nini msifanye mikutano ya wazi mkawaambia wananchama wenu hayo mambo yenu km mnao? Nyie ACT na CCM mnataka kutumia msiba kujiongezea point lakini sio jambo zuri hata kidogo!

Ndugu,
Kwa faida yako na faida ya Watanzania wote,
Ufafanuzi ufuatao unaweza kufaa kwa kila mwenye kutaka kufahamu.

Tunapenda kukufahamisha kwamba elimu hutolewa kokote kwa njia yeyote, la msingi ni kuhakikisha inafikia watu.Ni bora kokote unapoona elimu nzuri ukaichukua, ukaifanyia kazi na kuwafikishia wenzako na unapoona elimu mbaya kokote kuiacha na kukemea.Kadhalika unapoona jambo lolote jema mahali popote, ni bora ukalichukua na kuwafikishia wenzako na ukiona baya basi ukaliacha na kulikemea. Kwa kufanya hivyo utakuwa umetimiza wajibu wako kama binadamu, mzalendo na mtu unayeijenga nchi yako.Kinyume chake utakuwa umeamua kutokuwajibika kana kwamba hauna wajibu katika jamii yako.

Kuhusu aina ya mawasiliano ambayo Chama kinatumia kuwafikia wananchi, zipo nyingi kulingana na mazingira na uwezekano kwa wakati husika na aina ya watu wanaolengwa.Tunaweza kukutajia baadhi na kama nawe au mtanzania yeyote atakuwa na njia ya ziada nzuri inayoweza kutusaidia kuifundisha misingi ya chama chetu na kuwafikia watu wengi zaidi na wakaielewa; basi litakuwa ni jambo jema na la kushukuriwa.

Chama kinawasiliana na mtanzania mmoja mmoja kupitia mkakati maalum.Kama bado wewe hujafikiwa; ni suala la muda tu utafikiwa.Chama kitaanza kufanya mikutano ya hadhara karibuni.Kama eneo lako litakuwa ni miongoni mwa maeneo ambayo yatafikiwa, unashauriwa kuhudhuria na kuwashauri wenzako kuhudhuria vile vile.Kadhalika chama kimeanza kusambaza vitabu vidogo vinavyoeleleza na kufafanua mambo ya msingi yanayo husu chama.Kama hujafanikiwa kupata, basi utapata karibuni na ukifanikiwa kukipata kijitabu hicho, kisome kwa makini na ukiweza mpatie na mwenzako.

Kama mtu yeyote ana ushauri juu ya njia nzuri zaidi tunazoweza kuzitumia ili kuwafikia watanzania wote kwa wepesi zaidi, gharama nafuu zaidi, kwa haraka zaidi, kwa ufanisi zaidi na wakatuelewa zaidi ; basi litakuwa ni jambo jema sana.

Ikumbukwe kuwa ujenzi wa nchi yetu hii, ni jukumu letu sote, hivyo tushirikianeni ili kuifanya Tanzania kuwa eneo bora zaidi la kuishi na kuwafanya wananchi wake wawe na furaha zaidi.

Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa taifa la leo na kesho!

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom