ACT-Tanzania, Mapato na matumzi ya chama

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
643
Reaction score
1,603
Ndugu watanzania wote kwa ujumla, kokote mlipo tunawasalimu kwa salamu inayo ashiria mabadiliko na uwazi.

Ndugu watanzania, miongoni mwa maswali ambayo watanzania walikuwa wameuliza kuhusiana na chama cha ACT-Tanzania, ni pamoja na kutaka kujua kwamba chama kilitumia kiasi gani cha fedha katika zoezi la usajili na uhakiki wa wanachama waanzilishi zaidi ya 2000, na mpaka sasa chama kimetumia kiasi gani cha fedha, kimebaki na kiasi gani cha fedha na kimepata wapi fedha hizo.

Swali hili kimsingi ni muhimu sana kwa kuwa linagusa moja kwa moja moja ya msingi mmojawapo mkubwa wa chama, yaani "msingi wa uwazi"; ambapo chama kinaamini kwamba ni lazima kifanye shughuli zake kwa uwazi wa hali ya juu.Vile vile chama kinatambua kuwa miongoni mwa maeneo yanayofaa kupimia uadilifu wa watu ni katika eneo hili la mapato na matumizi.

Kwa kuwa ACT-Tanzania inajipambanua katika misingi ya uwazi √

Kwa kuwa ACT-Tanzania ni chama cha siasa cha mfano nchini √

Kwa kuwa taasisi yoyote ya umma ina wajibu wa kuweka wazi mapato na matumizi yake kwa kuwa yanatokana na umma wenyewe √

Kwa kuwa wanachama wanajitahidi kuchangia chama kwa moyo safi pamoja na kuwa na kipato duni √

Na kwa kuwa ACT- Tanzania imekuja kumaliza mazingaombwe ya kisiasa nchini √

ACT- Tanzania inapenda kuwafahamisha watanzania wote kwamba, kwa kuanzia itakuwa ikitoa taarifa zake za mapato na matumizi kwa umma, kila baada ya kipindi cha robo mwaka (miezi mnne) kwa kuanzia.Chama kinatamani ikiwezekana kiwe kinatoa taarifa zake kila mwezi lakini kwa kipindi hiki cha kuanzia, hakitaweza kufanya hivyo kwa kuwa zoezi hilo linahitaji gharama kubwa na chama bado hakijawa na chanzo cha mapato cha kuaminika.Kama ambavyo watanzania wengi wamekishauri chama kuwa kila kinapotoa taarifa muhimu, kisitegemee mitandao ya kijamii pekee bali kutumia mbinu zote za mawasiliano ili kuwafikia watanzania wote, ni dhahiri kwamba zoezi hilo linahitaji gharama kidogo.

Chama kinawaomba watanzania wahesabu miezi minne toka chama kilipopata usajili wa kudumu na hapo wasipopata taarifa ya fedha, basi watakuwa na haki ya kuhoji.Ni jambo lisolokuwa na wasi wasi kwamba taarifa itakapotoka kila mtu atajua ACT-Tanzania inapata wapi mapato yake, imepata kiasi gani, imetumia kiasi gani, imetumia kwenye nini, na imebaki na nini.

Ni matumaini yetu kwamba kila mtanzania mzalendo atakuwa ametuelewa vyema.

Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa ajili ya taifa letu leo na kesho!

Tuwasiliane kwa acttanzania@yahoo.com au acttanzania@gmail.com
 
Hivi ni watanzania wangapi wamo jamii forum? Mbona taarifa zenu naziona hapa tu au hiki chama ni cha jf?
 
Ni mwanzo mzuri lakini nina wasiwasi na sustainability yake! Kiukweli hakuna chama cho chote duniani kilicho na utaratibu huo! Hivyo nawapongeza kwa kuwa wa kwanza!

Tahadhari msije mkawa kama DECI kwa kuvutia wananchi wengi halafu mkaja sepa gizani baadaye!
 
Hivi ni watanzania wangapi wamo jamii forum? Mbona taarifa zenu naziona hapa tu au hiki chama ni cha jf?

Hii mijamaa imesajili chama kupambana na CHADEMA kwenye mitandao na media,so pathetic!!!
 
Huwa hakuna kazi ngumu kidogo,kama ni ngumu ni ngumu na kama ni rahisi ni rahisi tu.
 
"Chama kinatamani ikiwezekana kiwe kinatoa taarifa zake kila mwezi lakini kwa kipindi hiki cha kuanzia, hakitaweza kufanya hivyo kwa kuwa zoezi hilo linahitaji gharama kubwa na chama bado hakijawa na chanzo cha mapato cha kuaminika"

Hapo kwenye RED, kwani hazina ya serikali kuu chini ya Mwigulu imekwenda wapi? Vipi zile za mgawo wa Escrow account hazijafika huko?

Tiba
 
Kiongozi ni vizuri ukaanza kueleza mapato peke yake maana ndio yanatia shaka kwa sasa maana wengi tunaamini mmepewa hela na CCM na TISS. Then baada ya hiyo miezi 4 ndio utupe taarifa kamili ya mapato na matumizi. Je hela ya kupanga nyumba za ofisi, magari ya chama, ulisema mmeagiza bendera na kadi zaidi ya milioni nk, je mlichangiwa na nani hizo fedha?
 
Ha ha ha hiki ni kichekesho kikubwa, JF ndio mkutano mkuu wa chama hiki..!!? Ama kweli kabla hujafa utaona mambo mengi ya ajabu na hayatakwisha..!!!
 
Ndugu watanzania wote kwa ujumla, kokote mlipo tunawasalimu kwa salamu inayo ashiria mabadiliko na uwazi.

Ndugu watanzania, miongoni mwa maswali ambayo watanzania walikuwa wameuliza kuhusiana na chama cha ACT-Tanzania, ni pamoja na kutaka kujua kwamba chama kilitumia kiasi gani cha fedha katika zoezi la usajili na uhakiki wa wanachama waanzilishi zaidi ya 2000, na mpaka sasa chama kimetumia kiasi gani cha fedha, kimebaki na kiasi gani cha fedha na kimepata wapi fedha hizo.

Swali hili kimsingi ni muhimu sana kwa kuwa linagusa moja kwa moja moja ya msingi mmojawapo mkubwa wa chama, yaani "msingi wa uwazi"; ambapo chama kinaamini kwamba ni lazima kifanye shughuli zake kwa uwazi wa hali ya juu.Vile vile chama kinatambua kuwa miongoni mwa maeneo yanayofaa kupimia uadilifu wa watu ni katika eneo hili la mapato na matumizi.

Kwa kuwa ACT-Tanzania inajipambanua katika misingi ya uwazi √

Kwa kuwa ACT-Tanzania ni chama cha siasa cha mfano nchini √

Kwa kuwa taasisi yoyote ya umma ina wajibu wa kuweka wazi mapato na matumizi yake kwa kuwa yanatokana na umma wenyewe √

Kwa kuwa wanachama wanajitahidi kuchangia chama kwa moyo safi pamoja na kuwa na kipato duni √

Na kwa kuwa ACT- Tanzania imekuja kumaliza mazingaombwe ya kisiasa nchini √

ACT- Tanzania inapenda kuwafahamisha watanzania wote kwamba, kwa kuanzia itakuwa ikitoa taarifa zake za mapato na matumizi kwa umma, kila baada ya kipindi cha robo mwaka (miezi mnne) kwa kuanzia.Chama kinatamani ikiwezekana kiwe kinatoa taarifa zake kila mwezi lakini kwa kipindi hiki cha kuanzia, hakitaweza kufanya hivyo kwa kuwa zoezi hilo linahitaji gharama kubwa na chama bado hakijawa na chanzo cha mapato cha kuaminika.Kama ambavyo watanzania wengi wamekishauri chama kuwa kila kinapotoa taarifa muhimu, kisitegemee mitandao ya kijamii pekee bali kutumia mbinu zote za mawasiliano ili kuwafikia watanzania wote, ni dhahiri kwamba zoezi hilo linahitaji gharama kidogo.

Chama kinawaomba watanzania wahesabu miezi minne toka chama kilipopata usajili wa kudumu na hapo wasipopata taarifa ya fedha, basi watakuwa na haki ya kuhoji.Ni jambo lisolokuwa na wasi wasi kwamba taarifa itakapotoka kila mtu atajua ACT-Tanzania inapata wapi mapato yake, imepata kiasi gani, imetumia kiasi gani, imetumia kwenye nini, na imebaki na nini.

Ni matumaini yetu kwamba kila mtanzania mzalendo atakuwa ametuelewa vyema.

Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa ajili ya taifa letu leo na kesho!

Tuwasiliane kwa acttanzania@yahoo.com au acttanzania@gmail.com

Politican Finance is not candy and milk to show each and everyone, friends and enemies your EXPENDITURE...

This shows us THE LEADERSHIP is larking ETHICS...

Nchi GANI duniani hhata CHAMA MKIPENDACHO cha KIKOMUNISTI cha CHINA kinasambaza hayo MATUMIZI...

c.c ACT-Tanzania Uenezi
 
Kama kweli mmedhamiria kujenga taifa la kesho.Mnazungumziaje RUSHWA iliyokithiri katika taasis za serikali na binafsi...Ukizingatia kuwa ni chanzo kikubwa cha kurudisha maendeleo na udidimizaji wa haki za msingi za binadamu???.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom