HUko kwa CAG mimi simo maana nakuwa Sielewi Chama cha Siasa kisichotumia KODI za WANANCHI inakuwaje kikaguliwe na CAG.
*Kibanga, Vyama vya siasa havitakiwi kuwa mali ya mtu, vinatakiwa kuwa mali ya umma.Hivyo ni lazima mambo yake yote yafanyike katika utaratibu unaoeleweka na wa wazi.
Ndugu Kibanga, wakati wote tumekuwa tukilalamika kwamba kuna fedha chafu zinaingizwa kwenye mzunguko kupitia vyama vya siasa na leo hii watu (ukiwemo wewe) unalalamika kwamba ACT-Tanzania (kwa mfano), inafadhiliwa na wafadhili (ambao hujawataja lakini unaonekana unaamini kwamba hawakutakiwa kukifadhili).Sasa CAG Anataka akague ili ajue chama kinapata wapi fedha zake, fedha hizo ni halali au si halali, na chama kinazitumia je fedha hizo; nyie nyie (ukiwemo wewe) mnaolalamika kuingia kwa fedha chafu ndani ya vyama; mnajenga hoja kwamba visikaguliwe maana havina ruzuku ya serikali wakati wenzenu wanasema vyamo vyote maadam ni vyama vya umma vikaguliwe.
Wakati wengine wanasema ni lazima vyama vyote (iwe vinapokea au havipokei ruzuku) ni lazima viwe na wahasibu wenye weledi unaokubalika yaani CPA, Wale wale wanaolalamika wanasema ya nini wakati vyama husika havipokei ruzuku.Halafu vikiachwa; watu wale wale wanalalamika kwamba vyama husika vinaendeshwa kihuni.Hivi watu wa dizaini hii tukiwategema ni nini hatima yetu kama taifa?
Turudi kwenye hoja yangu amabyo ni kuwa nimetoa tu angalizo, Kuwa HAKUJAWAHI kutokea CHAMA kipya KIKAFANYA VIZURI kushinda Hivyo Vilivyoanza NA MAGEUZI ,Miaaka 90.
*Hii nitakujibu kwenye post ya peke yake maana nataka nikukumbushe mijadala yetu mimi na wewe siku chache zilizopita.
Na ukwlei ni kuwa, baada ya Uchaguzi wa 2015 ndio itakuwa mwisho wa ACT maana kwa sasa wafadhili wao wanakihitaji kwa kuwa kimekuja nkupambana na Vyama Vingine vyote, ila baada ya 2015 kutakuwa hakuna tena mapambano na Mfadhili atajitoa.
*Hivi kibanga;Unaposema mfadhili wa ACT-Tanzania,ili hoja yako iwe na maana, unatakiwa ueleze kwamba mfadhili huyo ni nani, wewe umemjuaje, unavielelezo gani na unaweza je kututhibitishia kwamba vielelezo vyako ni vya ukweli kabla ya ya kuipa manani hoja yako na kuendelea kuijadili.Kinyume chake ni kwamba utakuwa umeamua kujadili vitu ambavyo ni objective kwa kutumia emotions! na mwendo huo utakupoteza kabisa na kuishia kuushangaza ulimwengu.
Kwa ujumla mpaka sasa hujaeleza kwamba unachoongelea wewe ni changamoto au fursa au vyote maana ndio hoja iliyoko mbele yetu.Ukitaka ueleweke; usichangie tu ilimradi bali soma kwanza mada uielewe na kisha uhakikishe kwamba michango yako katika hitimisho; inaenda kuonesha muonganikano na mada iliyoko mezani.