ACT-Tanzania: Challenges and Opportunities! (SEHEMU YA KWANZA)

ACT-Tanzania: Challenges and Opportunities! (SEHEMU YA KWANZA)

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,198
Reaction score
7,539
Wadau, baada ya kupotea kidogo, leo ningependa nilete kwenu mjadala kidogo kuhusu chama kilichosajiliwa hivi karibuni ACT-Tanzania.

Inafahamika wazi kwamba chama cha ACT-Tanzania ni chama cha 23 kusajiliwa kama sio cha 22.Kama vilivyo vyama vingine(ikiwa kweli vinaamini hivyo), ACT-Tanzania nayo inaamini na inapigania kuwa chama cha kwanza kwa kukubalika zaidi na hivyo kuiongoza nchi na kutekeleza falsafa, itikadi na sera zake.Sasa swali la kujiuliza tu ni ikiwa ni jambo lipi hasa litakalokifanya chama cha ACT-Tanzania kufikia lengo hilo kama vyama zaidi ya 20 vilivyotangulia kwa miaka nenda rudi vimeshindwa kufikia lengo? na je ni nini cha ziada ambacho ACT-Tanzania inacho tofauti na watangulizi wao ? maswali haya pamoja na mengine; yanabakia kuwa mambo ya mjadala.

Kwa leo mimi ningependa tu kugusia kidogo changamoto na fursa zinazoikabili ACT-Tanzania angalau (02) tu kwa uchache wake.

1. Uchanga wa Chama:
  • Changamoto,

i) Kwa sasa ACT-Tanzania ndicho chama kichanga kuliko vyote; hivyo kama ni mtoto, tunaweza kusema ni 'kichanga'.Sasa changamoto ni kwamba ni kwa vipi ACT-Tanzania inaweza kukimbia kutoka chini mwisho hadi kufika juu mwanzo na kasi hiyo kitaitoa wapi!.

ii) Pili Vyama vyote vya upinzani vilivyotangulia kuanzia kuanzishwa kwa sera ya vyama vingi hadi leo, havijaweza kufikia lengo la kuunda serikali.Sasa changamoto ni kwamba ni kwa vipi ACT-Tanzania itaweza kufikia lengo ikiwa wa kabla yao kwa miaka nenda rudi wamekwama, na ni kwa vipi hasa ACT-Tanzania itaweza kukabiliana na changamoto zilizowashinda watangulizi wake.

  • Fursa,
i) Angalau ACT-Tanzania kutokana na uchanga wake, bado haijafanya jambo lolote ovu; hivyo haina kashifa yeyote ya ukosefu wa maadili au ufisadi, hivyo kama fursa hii italindwa na kutumika vizuri inaweza kusaidia sana.
iii) Angalau ukiangalia misingi ya ACT-Tanzania;Unagundua kwamba inaitofautisha kabisa ACT-Tanzania dhidi ya vyama vyote vilivyotangulia kabla yake.Sasa kazi kubwa ni ikiwa chama kitaweza kutembea katika misingi hiyo.

ii) Angalau ACT-Tanzania inaonekana kuwa na watu wengi wenye utaalam na upeo mzuri juu ya masuala ya siasa pamoja na dhamira ya dhati.Kwa hiyo kama watajituma na kushawishi watu wengine wenye Uzalendo wa kweli,vipaji na uoni kuwaunga mkono, hiyo itaweza kukisaidia sana chama hiki kichanga kuliko vyote kupiga hatua.

2:Imani.
Katika hali ya kawaida, ili chama kiweze kusonga mbele kwenda juu na pengine hadi kufikia kushika nafasi ya kwanza (yaani kushika dola) ni lazima kiaminiwe na imani haiji yeyewe tu bali hujengwa na imani thabiti ni ile inayojengwa kwa matendo na si maneno matupu.

  • Changamoto
i) Watanzania wengi walishawahi kuumwa na nyoka tena pengine zaidi ya mara moja, na bado wanajua nyoka walio wauma wako mitaani,sasa wakiona majani wanaogopa maskini!.Hata ukimuhakikishia mtu wa namna hiyo kuwa anachokiona 'ni jani' bado tu atabaki na wasi wasi kwamba ni nyoka na akigusishwa mguuni bila kuona lazima ataruka tu!

ii) Watanzania ni wale wale, kwa hiyo wafuasi watakaoiunga mkono ACT-Tanzania na pengine kugombea na kupata uongozi wa chama ni watanzania hawa hawa ambao ni 'Heterogenious' . Sasa upo uwezekano wa watu ambao hawakuwa waadilifu kwenye vyama vingine, kuingia ACT, Kwa dhumuni lile lile la kufanya uharibifu nchini na hivyo kuifanya ACT-Tanzania nayo isiaminike na wasioiami wawe na uhalali wa kufanya hivyo.

  • Fursa;

i) Uchanga wa chama wenyewe ni fursa; Waswahili husema samaki mkunje angali mbichi. Kama chama cha ACT-Tanzania kitatengeneza kanuni na mifumo thabiti na kuisimamia kuanzia mwanzo kwa nguvu moja na kuhakikisha kwamba wasimamizi wa misingi na kanuni hizo nao ni waadilifu na wasafi, basi hiyo inaweza ikakisaidia chama hiki kichanga kuliko vyote nchini.

ii) Chama cha ACT-Tanzania bado hakijawa na makando kando; kwa hiyo kikianza kuonesha kwa matendo tokea mwanzo kwamba kinatenda kinayoyasema; basi walioumwa na nyoka kidogo kidogo wataanza kuona tofauti ya nyoka na majani 'Objectively'. Kwa kuwa mazoea hujenga tabia, kwa kuanza na kujizoeza kutembea katika yale ambayo chama kinayasema; itajenga tabia ya chama, na tabia ya namna hiyo inakuwa ni tabia 'Possitive' ambayo kimsingi ndiyo inayotakiwa.

Kwa leo niishie hapa na nitaendelea kueleza changamoto na fursa nyingine kwa kadiri Mungu atakavyotujaalia.Tumuombe Mungu atupe afya njema na atuongezee ujuzi elimu na maarifa ili tuweze kuelimishana, kujadiliana na kuijenga nchi yetu kwa maslahi ya watu wetu kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

...

i) Angalau ACT-Tanzania kutokana na uchanga wake, bado haijafanya jambo lolote ovu; hivyo haina kashifa yeyote ya ukosefu wa maadili au ufisadi, hivyo kama fursa hii italindwa na kutumika vizuri inaweza kusaidia sana.
...

Kashfa namba moja duniani ni kuwa puppet. Hawa wapuuzi wanazunguka huko na huko kwa niaba ya mabwana zao kushawishi wananchi kukataa mabadiliko yaliyoasisiwa na wananchi wenyewe. Taarifa za mitandao zinaonesha hivyo.
 
Unataks tujadili nini salsa kuwa nio kichanga au nini acheni uto to mnabore......huna cha kuandika soma vya wenzako
 
Kashfa namba moja duniani ni kuwa puppet. Hawa wapuuzi wanazunguka huko na huko kwa niaba ya mabwana zao kushawishi wananchi kukataa mabadiliko yaliyoasisiwa na wananchi wenyewe. Taarifa za mitandao zinaonesha hivyo.
Nilishawahi kuleta uzi mzima hapa nikihoji hivi ni nani mwananchi hasa! Hakuna aliejibu zaidi ya wachangiaji wengi kusema nao wanashangaa! sasa nawe nakuuliza tena kabla ya kuanza kuishughulikia hoja yako kwa undani; kwa uelewa wako wewe mwananchi ni nani hasa? je wewe ni mwananchi? je mimi ni mwananchi? je wana ACT-Tanzania ni wananchi? je wana CUF wananchi? je Mkuu wa wilaya ni mwananchi? je polisi ni mwananchi? Mwananchi ni nani hasa? na ukijibu swali hili; ikiwa una nia njema. nasi tutaendelea kuifanyia kazi hoja yako na kuona ukweli na mantiki yake
 
Mamlaka na madaraka yote yatatoka kwa wananchi, sio kwa mkuu wa wilaya, Rais, mbunge, ACT-Tz, CCM, Chadema, NCCR-Mageuzi, Bunge, au pengine popote. Katiba ya nchi (na Rasimu ya Warioba ukitaka) imeeleza mwananchi ni nani.
 
Unaamini kwamba nilichukuuliza ndicho ulichojibu na huna shaka yeyote juu ya hilo?Kama ndio, basi turudi kwenye mada ya msingi iliyoko kwenye uzi maana hilo la katiba ya na Rasimu ya Warioba halihusiani na mjadala huu ila kama werwe unadhani linahusiana! basi una uhuru. Hiyo ndiyo demokrasia na kwa kuwa vichwa vya wanadamu havifanani; basi hali za namna hii kutokea ni kawaida sana.
 
Chama cha hovyo sana hiki ,kinatangaza uchaguzi bila Kuwa na katiba ,sijui kimepata wapi muundo was uongozi wakati katiba yao haijapitishwa.

Chama wamekaa watu wanne Morogoro na kujipa cheo cha kamati kuu.......chama cha aina gani hiki?
 
Mkuu betlehem, nilitarajia kuwa ungetuwekea MALENGO na MWELEKEO wa ACT ... Naamini Watanzania wengi wanataka radical changes ktk kila Nyanja ya uendeshaji wa nchi hii... perhaps AZIMIO la arusha lingeweza kuwapaisha sana ....
 
Niviongozi wapi wenye uzoefu au sifa zao ni zipi?
Pili;hicho chama kwanini kimeamua kufuata vyama vingine vingi hapa nchini kwakutuletea jina la chama kwa kiingereza,hivi nia ya chama hiki ni wanachama wa aina gani?ni watanzania wangapi wa naelewa maana ya jina la chama hiki?
 
Hawa Act-tanzania washambakweli yani kila cku mpo humu JF tu mnazugazuga sasa sijui ndo tutawapigia kura humu JF mi nahsi nyie ni sacos mpya jiiteni tu Act-tanzania sacos hili liko bomba zaidi..!!
 
Chama cha hovyo sana hiki ,kinatangaza uchaguzi bila Kuwa na katiba ,sijui kimepata wapi muundo was uongozi wakati katiba yao haijapitishwa.

Chama wamekaa watu wanne Morogoro na kujipa cheo cha kamati kuu.......chama cha aina gani hiki?
Alaah! hebu ifafanue vizuri hii ndugu yangu! maana inaonekana una uelewa mzuri wa kile unachokiongea.kwa hiyo kimsingi kitakuwa kimesajiliwa bila katiba vile vile au?au kitakuwa kina katiba lakini kwa kuwa wewe hujaiona; basi kimsingi itakuwa haipo? kwani mkuu kwa kawaida katiba za vyama vya siasa hupatikana je kitaalam na uhalali wake wa kisheria na kisiasa hupatikana je na wakati gani, na ni wakati gani hasa inatakiwa ianze kutumika kitaalam? maana inaonekana wewe ni mzuri sana kwenye mambo haya!

Kisha baada ya hapo, turudi kwenye mada ya msingi hapo juu kama una la kuchangia maana nimeona kwenye comment yako ya awali umependekeza kwamba; ni bora kama mtu hana cha kuchangia akaacha na kusoma michango ya wenzake, wazo ambalo kimsingi ni zuri na mimi nilikubaliana nalo..
 
Unaamini kwamba nilichukuuliza ndicho ulichojibu na huna shaka yeyote juu ya hilo?Kama ndio, basi turudi kwenye mada ya msingi iliyoko kwenye uzi maana hilo la katiba ya na Rasimu ya Warioba halihusiani na mjadala huu ila kama werwe unadhani linahusiana! basi una uhuru. Hiyo ndiyo demokrasia na kwa kuwa vichwa vya wanadamu havifanani; basi hali za namna hii kutokea ni kawaida sana.

Kaka umeuliza mwananchi ni nani na bahati nzuri Katiba imetoa maana ya neno "mwananchi" kwamba ni yule ambaye (kwa umoja wao) madaraka na mamlaka ya uendeshaji wa nchi hutoka kwao na hukabidhi mamlaka haya kwa wachache (watawala) ili waendeshe nchi kwa niaba yao (wananchi).

Ni ajabu kwamba hawa ACT-Tz wanashirikiana na baadhi ya watawala kutaka kupindua maoni ya wananchi juu ya uendeshaji wa nchi yao. Chama cha aina hii huwezi kusema eti "hakina kashfa". Kama nilivyosema, usaliti (kushiriki kupindua maoni ya wananchi) ni kashfa mbaya zaidi pengine kuzidi hata ufisadi na uchafu mwingine.
 
kadi yako ni namba ngapi ? Je mmetengeneza katiba ? Na inasemekana mnawapigia magoti baadhi ya WASALITI ili waje kugombea uongozi , kwanini hamtoi fomu ili kila anayetaka aje mwenyewe kuchukua ?
 
Siwezi jibishana na MTU asiyetaka kujielimisha,soma alichoandika juzi aliyejiita mwenezi was ACT wakati anatangaza ratiba ya uchaguzi we nu Mara baada ya kikao cha masaki.....
 
Chama cha hovyo sana hiki ,kinatangaza uchaguzi bila Kuwa na katiba ,sijui kimepata wapi muundo was uongozi wakati katiba yao haijapitishwa.

Chama wamekaa watu wanne Morogoro na kujipa cheo cha kamati kuu.......chama cha aina gani hiki?
naomba ushaidi juu ya chama kutangaza uchaguzi kabla ya katiba.akili ya kufugwa inamatatizo.uchaguzi utafanyika baada ya rasimu ya katiba kupitishwa.acheni propaganda za kitoto.
 
Changamoto kubwa kama kweli wanataka kushika dola wajiandae na fitina, majungu, kuhongwa, kupigwa na kuumizwa na chama dola, kwani hakitaki ushindani bali kuzuga wazungu ili watoe misaada kwa kisingizio cha democrasia pana.
Pia wajue wanaingia kwenye nchi ya watu wasio na elimu ya uraia ya kutosha. Kwa mazingira ambayo wananchi wanawapa uongozi chama kinachohonga wapiga kura, kuwatisha na kutumia dola kubaki madarakani wajue nguvu ya ushawishi wa hoja itakuwa na shuluba nzito. Ila kama kinapata support toka chama dola kama mazingira yanavyoonyesha basi viongozi wake watakuwa matajiri na watatumika wakati maalum tu kama backup ya chama tawala. Nadhani ndaniya mwaka lengo litafahamika.
 
Siwezi jibishana na MTU asiyetaka kujielimisha,soma alichoandika juzi aliyejiita mwenezi was ACT wakati anatangaza ratiba ya uchaguzi we nu Mara baada ya kikao cha masaki.....

wewe ndo urudi kusoma pengine umehadithiwa.shirikisha ubongo rudi kwenye ule uzi wa mwenezi
 
Kashfa namba moja duniani ni kuwa puppet. Hawa wapuuzi wanazunguka huko na huko kwa niaba ya mabwana zao kushawishi wananchi kukataa mabadiliko yaliyoasisiwa na wananchi wenyewe. Taarifa za mitandao zinaonesha hivyo.

Akili ya kuambiwa changanya na yako.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
Hawa Act-tanzania washambakweli yani kila cku mpo humu JF tu mnazugazuga sasa sijui ndo tutawapigia kura humu JF mi nahsi nyie ni sacos mpya jiiteni tu Act-tanzania sacos hili liko bomba zaidi..!!

Ulizani JF ni ya Chadema sio?

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
Mkuu betlehem, nilitarajia kuwa ungetuwekea MALENGO na MWELEKEO wa ACT ... Naamini Watanzania wengi wanataka radical changes ktk kila Nyanja ya uendeshaji wa nchi hii... perhaps AZIMIO la arusha lingeweza kuwapaisha sana ....
mkuu RockSpider jana kuna uzi humu ambao ulikuwa na document yenye misingi ya ACT-Tanzania.Nimejaribu kuihamisha document peke yake naona inainisumbua ila unaweza kuifuata huko.Rejea;
ACT-Tanzania (Alliance for Change and Transparency): Taarifa kwa Umma.

Mimi nimeipitia misingi hiyo kwa umakini sana na nilichokiona ni kwamba kwa kiasi kikubwa inaakisi azimio la Arusha lililoboreshwa ili kukidhi mazingira ya sasa. Sasa bado ambacho mimi nakiona kwamba kinabakia kuwa suala la mjada na kazi ngumu kiutekelezaji; ni kama ACT-Tanzania yenyewe itaweza kutembea katika misingi hiyo bila kukengeuka ila kimsingi misingi yenyewe ni mizuri angalau ki nadharia kwa kuanzia.Zaidi zaidi unaweza kuipitia na tukaijadili na kuikosoa kila tutakapoona inafaa au vinginevyo kuiunga mkono.

Zaidi zaidi wale wanaokosoa vitu bila hata kuviona au kuviona bila kuvisoma, au kuvisoma na kisha ku-divert mada wapo jana, leo na kesho na tatizo ni mambo kama matatu hivi, ambayo ni;

I, ukosefu wa elimu ya uraia kwa baadhi,

2. kukubali kutumika bila kujali anayemtumia muhusika na anatumika kufanya nini,na
3. Kile ambacho mtaani wanakiita "Kujitoa fahamu".

N.B Inawezekana kuna na mengine ambayo siyajui lakini wengine wanaweza kuyajua.

Kuna baadhi ya watu wana tatizo moja au yote miongoni mwa makundi hayo hapo juu na watu hao wataendelea kuwepo tu.La msingi ni kuwavumilia na kuwaelewesha tu kwa kadiri itakavyowezekana.
 
Back
Top Bottom