ACT-Tanzania: Challenges and Opportunities! (SEHEMU YA KWANZA)

ACT-Tanzania: Challenges and Opportunities! (SEHEMU YA KWANZA)

KFC,soma maelezo ya mwenezi was ACT ya juzi hapa jukwaani alitangaza ratiba ya uchaguzi ndipo baadae akasema katiba inafanyiwa kazi name jopo lililoundwa hivyo likikamilusha kamati kuu itapitia....wakati uchaguzi unaendelea
 
Kaka umeuliza mwananchi ni nani na bahati nzuri Katiba imetoa maana ya neno "mwananchi" kwamba ni yule ambaye (kwa umoja wao) madaraka na mamlaka ya uendeshaji wa nchi hutoka kwao na hukabidhi mamlaka haya kwa wachache (watawala) ili waendeshe nchi kwa niaba yao (wananchi).

Ni ajabu kwamba hawa ACT-Tz wanashirikiana na baadhi ya watawala kutaka kupindua maoni ya wananchi juu ya uendeshaji wa nchi yao. Chama cha aina hii huwezi kusema eti "hakina kashfa". Kama nilivyosema, usaliti (kushiriki kupindua maoni ya wananchi) ni kashfa mbaya zaidi pengine kuzidi hata ufisadi na uchafu mwingine.
Basi mkuu umeeleweka.Mimi nimekuelewa na vile vile ni matumaini yangu kwamba wadau wote watakuwa wamekuelewa kwamba kimsingi ACT-Tanzania kwa sasa imepata kashfa ya "Mapinduzi" eeeh! "Kujaribu kupindua maoni ya wananchi" kama unavyosema na chanzo cha taarifa hiyo ni wewe mwenyewe.Vile vile unatuambia kwama jaribio hilo la mapinduzi, ni jaribio baya zaidi na hivyo ndio kashfa kubwa zaidi kuliko kashfa nyingine zilizowahi kutokea nchini na hivyo chama Hicho ndicho kibaya kuliko vyote na hivyo hakina fursa yeyote ya kufanya vizuri.

Ok! umeeleweka ndugu yangu.
 
Kuna tatizo kubwa sana la watanzania walio wengi hasa vijana,kuzomea vitu mbali mbali,kutokupenda kusumbua akiri kwa kutafakari na kujipa imani kwamba kila kitu ni propaganda.
Nina wakumbusha kuwa kwa aina ya siasa za vyama vya upinzani za miaka20,AcT,ikija vyema tutaona vyama kama chadema vikijifia kwasababu ya kutokukubali kukosolewa na kujisahihisha.ACT inaweza kuchora mstari wa ukomo wa siasa zisizo na agenda.,kama itatumia fursa na changamoto za vyama vilivyopo.
 
naomba ushaidi juu ya chama kutangaza uchaguzi kabla ya katiba.akili ya kufugwa inamatatizo.uchaguzi utafanyika baada ya rasimu ya katiba kupitishwa.acheni propaganda za kitoto.

By Haki sawa
Hiki chama ni cha hovyo sana, yaani uchaguzi wa vitongoji mpaka taifa unatangazwa kabla ya katiba kupitishwa, hivi huo muundo wa uongozi mmeutoa wapi wakati hamna katiba?

mwenezi ambaye ni verified hapa......

Kwa faida ya muuliza swali na umma kwa ujumla: tunapenda kulitolea ufafanuzi tena na tena jambo hili.Tunapenda kufafanua tena kwa wale ambao hawakuona ufafanuzi wetu wa awali kwamba ACT-Tanzania ina katiba (rasimu) ambayo ndiyo chama kimeitumia kupata usajili.Rasimu hii inaelekeza mambo yote ya msingi ikiwemo misingi, itikadi na falsafa ya chama.Vile vile inaelekeza muundo mzima wa chama.Hata hivyo chama kilishatoa ufafanuzi kwamba Kamati kuu ya muda iliunda jopo la kudurusu (revise) rasimu hiyo kwa kuwa wawanachama na wadau wengine waliona kuna makosa katika baadhi ya sehemu kwenye rasimu hiyo ikiwemo makosa ya kiuchapaji na kisarufi.Hivyo basi kama chama kilivyotoa ratiba hapo juu; imeelezwa ni nini kinaendelea na bila shaka rasimu yenye mabadiliko itakapokabidhiwa katika kikao kilichokuwa kimeunda jopo la marejeo ya katiba hiyo na kikao kukubali kwamba marekebisho yaliyofanywa ni sahihi; jamii nzima inaweza kupatiwa tena rasimu hiyo pengine hata kabla ya mkutano mkuu ili wadau wengine nao waweze kutoa ushauri na maoni yao.

Vile vile wote tufahamu kwama ACT-Tanzania ni bado ni mtoto wa siku kumi (10), sasa mtoto anakuwa taratibu.Chama kinashauri kwamba ni bora wadau kutoa ushauri na kukosoa kila inapostahili ili chama kiweze kuwa bora badala ya kulalamika tu.
 
ni watanzania wangapi wa naelewa maana ya jina la chama hiki?
Tuanze na wewe kwanza; je! wewe unajua maana yake? kama unajua, ushawahi kuwaelimisha wangapi ili nao wajue, na kama hujawahi kuelimisha yeyote, elimu hiyo unakaa nayo ya nini na kwa faida ya nani na mpaka lini? na kama hujui maana yake; je ushawahi kuwauliza wanaojua wakujuze? kama hujawahi kuuliza, je umeemua kubaki hivyo hivyo bila kujua? kama uliuliza; je! uliowauliza wote hawajakuambia! kama wamekuambia unacholalamika nini?

Au wewe unajua maana yake, ila wapo wasio jua? na kama ndio hivyo, wewe umejua je kwamba wapo wasiojua na ni kina nani? je! ujuavyo wewe dawa ya mtu asiyejua kitu ni nini?

Hebu tusaidie maana inaonekana wewe una mawazo mazuri sema tu hujayatoa bado.
 
Kwa uandishi huu na elimu yako uliyonayo inashangaza kuwa unataka kufisadi time kwa kujadili chama cha mamluki na wanafiki,please niambie hoja gani Zitto aliyowahi kuianzisha na akaisimamia hadi mwisho??! Mabilioni ya Uswisi- filamu imeishia wapi??!

Mgodi wa Buzwagi??!! Zitto alijengewa shule na kupewa mabati jimboni kwake na kampuni ile ile!!! Akaingizwa kwenye kamati ya Bomani na wakaongeza 1% ya mrahaba!!

Sakata la nishati na mitambo ya Buzwagi??!! Zitto alishauri Tanesco inunue mitambo ile ili hali mmiliki alikuwa ni Rostam Aziz na Zitto na Rostam na January Ma-rope ni chanda na dole!!

Huyu Zitto ni Mlaghai tu na kibaraka wa wenye pesa na madaraka anayejificha katika siasa kwa kujifanya mzalendo kumbe wapi!!!

Kitila Mkumbo nae ni mamluki tu kwani ipo wazi huwezi kupewa idara kuu ya Elimu ya juu na Serikali ya CCM kama wewe ni mpinzani wa kweli,rejea wadhifa wa Kitila pale DUCE then njoo kwa kina Luhanga na Bana pale UDSM then endelea IFM,TIA,AIA etc

Na umamluki wake unathibitika kwa kula njama dhidi ya CHADEMA ili hali akiwa ni mshauri wa CHADEMA!! KWA nini hakutumia nafasi yake ya ushauri kueleza hayo mapungufu bila kuandaa njama za kupindua??!!

Naamini wameanzisha CHAMA kipya kama mradi mpya tu kuelekea 2015 ili kugawa kura za CHADEMA!! Kwa kuwa kuingia CCM ingethibitika rasmi habari za Zitto kuwa ndoano yao na ingeibuka pasipo samaki ni hasara kwa CCM kwa pesa na mbinu zao,wakaamua kwenda kuiepeleka ndoano yao kuvua sehemu mpya!!

Lengo ni lile lile la kufanya kazi ya CCM huku wakipewa fursa za kukuzwa kisiasa na CCM na mathalani sasa ACT inatajwa takes bungeni hata na Pinda na masipika ili kutoa airtime kwa mradi wao na lengo naona sasa ni kugawa kura za kanda ya Ziwa!!

ACT ni TLP mpya kwa kuwaleta wakina Mrema wapya kutoka kanda mpya kuiba kura kwani Mrema kashaisha na Kanda ya kaskazini CCM ni totally defeated kasoro Tanga!!
 
By Haki sawa
Hiki chama ni cha hovyo sana, yaani uchaguzi wa vitongoji mpaka taifa unatangazwa kabla ya katiba kupitishwa, hivi huo muundo wa uongozi mmeutoa wapi wakati hamna katiba?

mwenezi ambaye ni verified hapa......

Kwa faida ya muuliza swali na umma kwa ujumla: tunapenda kulitolea ufafanuzi tena na tena jambo hili.Tunapenda kufafanua tena kwa wale ambao hawakuona ufafanuzi wetu wa awali kwamba ACT-Tanzania ina katiba (rasimu) ambayo ndiyo chama kimeitumia kupata usajili.Rasimu hii inaelekeza mambo yote ya msingi ikiwemo misingi, itikadi na falsafa ya chama.Vile vile inaelekeza muundo mzima wa chama.Hata hivyo chama kilishatoa ufafanuzi kwamba Kamati kuu ya muda iliunda jopo la kudurusu (revise) rasimu hiyo kwa kuwa wawanachama na wadau wengine waliona kuna makosa katika baadhi ya sehemu kwenye rasimu hiyo ikiwemo makosa ya kiuchapaji na kisarufi.Hivyo basi kama chama kilivyotoa ratiba hapo juu; imeelezwa ni nini kinaendelea na bila shaka rasimu yenye mabadiliko itakapokabidhiwa katika kikao kilichokuwa kimeunda jopo la marejeo ya katiba hiyo na kikao kukubali kwamba marekebisho yaliyofanywa ni sahihi; jamii nzima inaweza kupatiwa tena rasimu hiyo pengine hata kabla ya mkutano mkuu ili wadau wengine nao waweze kutoa ushauri na maoni yao.

Vile vile wote tufahamu kwama ACT-Tanzania ni bado ni mtoto wa siku kumi (10), sasa mtoto anakuwa taratibu.Chama kinashauri kwamba ni bora wadau kutoa ushauri na kukosoa kila inapostahili ili chama kiweze kuwa bora badala ya kulalamika tu.

Kwani ndugu Haki sawa , kwa mujibu wa ratiba hiyo iliyotolewa; mkutano mkuu maalum wa katiba unakaa lini na uchaguzi wa chama ni lini?ni kipi kinachoanza kabla ya kipi? je! ni sahihi hicho kinachoanza kuanza kabla ya mwenzake? kama ndio ni kwa sababu gani na kama sio ni kwa sababu gani?

Wewe haki sawa inaonekana una uelewa mzuri kweli na unaweza kutoa elimu nzuri sana kwa maslahi ya watu wengi.Hebu fafanua kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Kwa uandishi huu na elimu yako uliyonayo inashangaza kuwa unataka kufisadi time kwa kujadili chama cha mamluki na wanafiki,please niambie hoja gani Zitto aliyowahi kuianzisha na akaisimamia hadi mwisho??! Mabilioni ya Uswisi- filamu imeishia wapi??!

!
1. Ndugu yangu; umesoma mada vizuri na kuielewa kabla ya kuchangia? Hebu kama huna uhakika juu ya hili soma tena na tena.

2.Kwenye mjadala huu, kuna mahali katajwa zitto? kama sio, wewe zitto unamuingiza je hapa?

3. Zitto ni mwanachama wa chama gani na wewe umejua je?na unaweza kuleta ushahidi wa uanachama wake?

4.Ujuavyo wewe; chama cha siasa ni nini?

5. Unafiki ni nini na ni kwa vipi ACT-Tanzania ni chama cha wanafiki (vielelezo vya uthibitisho vitakuwa na nguvu zaidi) na ni kivivi hii inahusiana na mada ilioko mbele yetu?

6. Mamluki ni watu wa namna gani na ni vipi ACT-Tanzania ni chama cha mamluki na wewe umejua je!na hili linahusiana vipi na mada iliyopo mbele yetu?

7. Ufisadi ni nini na ACT-Tanzania wamefisidi nini na ushahidi wako ni nini?

Mkuu nimekuuliza maswali mengi sana na bado nilikuwa natamani kukuhoji zaidi ila ngoja tu niishie hapo kwanza.Unaweza kujibu yote, baadhi, moja au ukaayaacha yote kama utaona hayakufai.Ndio demokrasia hiyo ndugu yangu!
7
 
Kwani ndugu Haki sawa , kwa mujibu wa ratiba hiyo iliyotolewa; mkutano mkuu maalum wa katiba unakaa lini na uchaguzi wa chama ni lini?ni kipi kinachoanza kabla ya kipi? je! ni sahihi hicho kinachoanza kuanza kabla ya mwenzake? kama ndio ni kwa sababu gani na kama sio ni kwa sababu gani?

Wewe haki sawa inaonekana una uelewa mzuri kweli na unaweza kutoa elimu nzuri sana kwa maslahi ya watu wengi.Hebu fafanua kidogo.

kwenye ye uzi nimekutumia tayari wamebadilisha ile original version na huu ndio ujanja ujanja wa ACT unapoonekana ....uzuri nilishaucopy Uzi original .....aibu yenu enyi wajanja wajanja .....
 
kwenye ye uzi nimekutumia tayari wamebadilisha ile original version na huu ndio ujanja ujanja wa ACT unapoonekana ....uzuri nilishaucopy Uzi original .....aibu yenu enyi wajanja wajanja .....
mkuu sikuelewi unajadili nini hasa! ngoja mimi nikuache sasa pengine wadau wenzangu watakuwa wanakuelewa unajadili nini.
 
  • Thanks
Reactions: kdc
Unaposema kama watu wake watakuwa waadilifu, hivi hujui kuwa viongozi wa ACT ni walewale wasaliti wa taifa wanaotumiwa na ccm kukwamisha harakati za wananchi kujikomboa kutoka mikononi mwa mafisadi ccm, namaanisha walisati waliasi Chadema ambao ni Zitto kabwe, Dr asiyejielewa Kitila Mkumbo, Samsoni Mwigamba, na vidudu mtu vingine ambavyo vilifukuzwa kitambo kwa usaliti, fedha wanazotumia ni kodi zetu wanazoiba mafisadi ambazo zingetumika kwenye maendeleo, siku zote wanaopita katika maovu hawafanikiwi kamwe, kwani wafanyayo ni laana mbele za Mungu.
 
1. Ndugu yangu; umesoma mada vizuri na kuielewa kabla ya kuchangia? Hebu kama huna uhakika juu ya hili soma tena na tena.

2.Kwenye mjadala huu, kuna mahali katajwa zitto? kama sio, wewe zitto unamuingiza je hapa?

3. Zitto ni mwanachama wa chama gani na wewe umejua je?na unaweza kuleta ushahidi wa uanachama wake?

4.Ujuavyo wewe; chama cha siasa ni nini?

5. Unafiki ni nini na ni kwa vipi ACT-Tanzania ni chama cha wanafiki (vielelezo vya uthibitisho vitakuwa na nguvu zaidi) na ni kivivi hii inahusiana na mada ilioko mbele yetu?

6. Mamluki ni watu wa namna gani na ni vipi ACT-Tanzania ni chama cha mamluki na wewe umejua je!na hili linahusiana vipi na mada iliyopo mbele yetu?

7. Ufisadi ni nini na ACT-Tanzania wamefisidi nini na ushahidi wako ni nini?

Mkuu nimekuuliza maswali mengi sana na bado nilikuwa natamani kukuhoji zaidi ila ngoja tu niishie hapo kwanza.Unaweza kujibu yote, baadhi, moja au ukaayaacha yote kama utaona hayakufai.Ndio demokrasia hiyo ndugu yangu!
7

Mkuu sitohangaika na maswali ya kizandiki ila ipo wazi huwezi kitenganisha ACT na Zitto,Kitila na Mwigamba!! Mwanzo wote walikana n'a kuapa ni CHADEMA ila leo Mwigamba na Kitila rasmi ni ACT n'a wamesema watamualika Zitto agombee uenyekiti na Zitto hajawahi kukana kuhusishwa n'a ACT zaidi anasema subiri kesi iishe!!

Katika hili sitojibu maswali yako ya kizandiki kwani ipo Wazi huwezi kujadili udhaifu n'a uimara wa nyumba pasipo kumtaja pia mmiliki wa nyumba,mkandarasi n'a ikiwezekana mdhamini!!

Uzuri id ya Betlem na uandishi wako nutambua tangu enzi za fukuto la hao jamaa wa ACT ndani ya CHADEMA,kwa hiyo tuswali twako havina tija pasipo kuwa n'a endorsement kuu ya waanzisha ACT n'a wadhamini wao n'a pia thé motive behind!!
 
Unaposema kama watu wake watakuwa waadilifu, hivi hujui kuwa viongozi wa ACT ni walewale wasaliti wa taifa wanaotumiwa na ccm kukwamisha harakati za wananchi kujikomboa kutoka mikononi mwa mafisadi ccm, namaanisha walisati waliasi Chadema ambao ni Zitto kabwe, Dr asiyejielewa Kitila Mkumbo, Samsoni Mwigamba, na vidudu mtu vingine ambavyo vilifukuzwa kitambo kwa usaliti, fedha wanazotumia ni kodi zetu wanazoiba mafisadi ambazo zingetumika kwenye maendeleo, siku zote wanaopita katika maovu hawafanikiwi kamwe, kwani wafanyayo ni laana mbele za Mungu.
Kwani kwa sasa ujuavyo wewe ; kwa sasa viongozi wa ACT-Tanzania ni akina nani? Ujuavyo wewe, mtu akkifukuzwa au kutoka chadema kimsingi ni msaliti wa nchi?Kwani usaliti ni nini? Katika mchango wako ulioutoa hapa; unachotaka kutuambia ni kwamba kwa mujibu wa uzi; ACT-Tanzania wana challenges lakini hawana opportunities!? au unataka kusema nini maana nimepitia mchango wako najaribu kuuoanisha na mada ni kama mimi sijaona muunganiko na mada yenyewe! au hujaelewa mada?
 
Mkuu sitohangaika na maswali ya kizandiki ila ipo wazi huwezi kitenganisha ACT na Zitto,Kitila na Mwigamba!! Mwanzo wote walikana n'a kuapa ni CHADEMA ila leo Mwigamba na Kitila rasmi ni ACT n'a wamesema watamualika Zitto agombee uenyekiti na Zitto hajawahi kukana kuhusishwa n'a ACT zaidi anasema subiri kesi iishe!!
!
1. Kwani kaka uzandiki ni nini na maswali yangu yanakuwa ya kizandiki kivipi? Je! ni maswali yote saba ni ya kizandiki? kama sio nijubu basi angalau hata mawili ambayo si ya kizandiki ila kama yote saba ya kizandiki; basi no comment!

2.Unasema Mwigamba Zitto na Dr.Kitila, waliapa kuwa ni chadema, sasa wako ACT-Tanzania.Napenda kukufahamisha tu (maana inaonekana huna habari) kwamba Dr.Kitila na Mwigamba walifukuzwa CHADEMA na kwa sababu hiyo wakapoteza uanachama wa chadema.Sasa kwa mujibu wa sheria za Tanzania, ni sawa tu mtu yeyote kujiunga na chama chochote atakacho; sasa sijajua hoja yako ni nini hasa! kuhusu kwamba walifukuzwa kwa sababu gani; hivi hilo bado ni suala ambalo halifahamiki mpaka sasa? je! uonavyo wewe! mjadala katika uzi huu kwa sasa unamuhusu Mwigamba na Dr.Kitila? Hivi inamaana hufahamu kwamba Zitto mpaka leo bado ni mwanachama wa chama gani au unafanya makusudi?

3.Unaposema hatuwezi kuwatenganisha watatu hao; hatuwezi kuwatenganisha kwenye nini sasa na hoja hiyo inahusiana vipi na uzi huu wa "Challenges& opportunities walizonazo ACT-Tanzania? hiyo inakuwa ni challenge au ni opputunity ili turudi kwa mada ya msingi?

4. Hivi kitaalam; ni kosa kwa mtu mmoja, au chama kuwashawishi watu wengine kujiunga na chama husika bila kujali vyama vyao na vyadhifa zao? kama sio! hoja yako ni nini sasa?
 
Unaposema kama watu wake watakuwa waadilifu, hivi hujui kuwa viongozi wa ACT ni walewale wasaliti wa taifa wanaotumiwa na ccm kukwamisha harakati za wananchi kujikomboa kutoka mikononi mwa mafisadi ccm, namaanisha walisati waliasi Chadema ambao ni Zitto kabwe, Dr asiyejielewa Kitila Mkumbo, Samsoni Mwigamba, na vidudu mtu vingine ambavyo vilifukuzwa kitambo kwa usaliti, fedha wanazotumia ni kodi zetu wanazoiba mafisadi ambazo zingetumika kwenye maendeleo, siku zote wanaopita katika maovu hawafanikiwi kamwe, kwani wafanyayo ni laana mbele za Mungu.

yaani kuna comment nyingine kuicha kama ilivyo itakua jf haijakusaidia we mchangiaji ......,...,.hebu nikuulize kitu 1 ivi chadema ni taifa?
 
Wana nafasi nzuri iwapo watafanya siasa za kujenga hoja na wananchi wakubali kuunga mkono hoja zenye mashiko. Pia nadhani iwapo watajenga hoja chama tawala huenda kikaona aibu na kukubali kuachia madaraka kwani hakitakuwa na hofu ya future yao hata kwa makosa waliyoyafanya kwani nadhani kuna uwezekano wa chama hiki kuleta muafaka wa kitaifa tofauti na sasa kwa kile kinachoendelea kati ya ccm na cdm.
 
Kinasimama nafasi nzuri ya kuleta muafaka wa kitaifa iwapo kitajenga hoja na kuachana na siasa za majitaka zilizoasisiwa na ccm baada ya kupata ushindani halisi toka cdm. Ccm huku bara hawakuwahi kupata changamoto halisi hasa huku bara hvyo baada ya kubanwa na cdm vilivyo ndio tukaanza kuona vitimbi na siasa za kukamiana kwani kuachia madaraka kirahisi ni ngumu kutokana na ukongwe wake. Ila kwasasa wangalau ccm wameanza kulainika ila sio kwa cdm kwani aina ya siasa za cdm ni hatari haswa kutokana na maisha ya viongozi wa ccm waliokuwa wamelewa madaraka na kuliingiza taifa kwenye mikataba mibovu, wanajua wataishia jela hvyo bora wakiachie chama kingine ambacho wangalau wataleta muafaka na kuganga yajayo.
 
yaani kuna comment nyingine kuicha kama ilivyo itakua jf haijakusaidia we mchangiaji ......,...,.hebu nikuulize kitu 1 ivi chadema ni taifa?
ni kweli mkuu; ukiona mtu anakosea na ukamsahihisha unakuwa umeufahamu wajibu wako na kuutekeleza.
 
Back
Top Bottom