Hilo jambo mbona liko wazi sana kuwa ACT imeanzishwa kimkakati ili kuiokoa Sisiem.
Usalama wa Sisiem ulishawatonya 'mabosi' wao kuwa kwa hali Ukawa walivyowakalia kooni, hakuna jinsi lazima ianzishwe Sisiem B, ili kura za upinzani zigawanwe, ili Sisiem ipete kiulaini.
Hata kauli iliyotolewa na ZZK, ambaye ndiye kiongozi mkuu wa ACT kuwa mwanachama yeyote atakayeiunga mkono Ukawa, atafukuzwa uanachama wa chama hicho ni uthibitisho mwingine kuwa, Sisiem na ACT ni mtu na mdogo wake.
Mbona kiongozi huyo mkuu hajawahi kutamka kuwa mwanachama wa ACT atakayeiunga mkono Sisiem kuwa naye atatimuliwa uanachama?
Kwa hiyo ushahidi wa mazingira unaonyesha kuwa ACT imeanzishwa kimkakati ili kuzigawa kura za wapinzani baina ya Ukawa na ACT, ili Sisiem ishinde kiulaini.