Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
Usiposumbua bongo waweza kudhani ACT kama chama chenye nia ya kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya mtanzania kimezaliwa katika wakati mbaya sana, naam katika wakati ambao vyama vikubwa na venye nguvu vya upinzani vikidhamiria kusimamisha mgombea mmoja katika ngazi zote na dhamira yao hiyo kuhitimishwa kwa makubaliano yaliyotiwa muhuri mbele ya wanaoitwa wafuasi na wanachama wa vyama hivyo katika viwanja vya jangwani.
Kwa wenye kusumbua bongo, wasiongozwa na ushabiki isipokuwa kweli, yaani werevu katu hawafikiri kama hichi chama kimezaliwa katika wakati mbaya, badala yake wataona kuwa chama hiki kimekuja katika wakati muafaka, wakati ambao kiukweli tunahitaji mbadala wa CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani na CCM kama chama tawala. Niko na sababu zifuatazo zilizonipelekea kuamini kuwa huu si wakati mbaya kwa ACT na ya kwamba kinakwenda kupenya kati ya CCM na UKAWA.
MOSI: FALSAFA NA ITIKADI YA ACT.
Falsafa na itikadi ya ACT vyote kwa pamoja vinajenga mahusiano ya moja kwa moja kati ya chama na wananchi wote bila kujali tafauti zao za umri, jinsia, kabila, dini, nk. Chama kimeundwa kwa kufuata misingi ya demokrasia jamii. Uzalendo, usawa, uadilifu, uwazi, uwajibikaji, demokrasia rasilimali, hifadhi ya jamii, utu, umoja wa Afrika na kujitegemea, weledi na bidii katika kazi ni misingi kumi ya ACT itakayo iwezesha chama hiki kupenya kati ya CCM na UKAWA.
Misingi hii ambayo inagusa maisha ya mtanzania wa mjini na kijijini haionekani au hautumiki katika vyama vinavyounda UKAWA na CCM. Kama ikienezwa vizuri na ikieleweka vijijini na mjini watanzania wataenda kuichagua ACT badala ya UKAWA au CCM kama inavyotegemewa. Huku ndio kupenya kwenyewe kwa ACT kati ya UKAWA na CCM.
PILI: HIVI WATANZANIA WANAHITAJI MUUNGANO TU WA UPINZANI?
Huku nikizingatia mashirikiano yaliokwisha kufanyika huko nyuma kwa vyama vyetu hivi vya upinzani, tangu mwaka 1995 kila chama kimekuwa kikipigana kivyake katika vita ya kuitoa CCM ikulu. Viongozi wa vyama vya CUF, CHADEMA na NCCR huenda wamejua kuwa watanzania wanataka kuona upinzani ulioungana, lakini wameshindwa kujua ni muungano upi wa upinzani ambao watanzania wanauhitaji.
Watanzania hawahitaji muungano wa vyama vya upinzani ambavyo tafauti yao na CCM ni majina tu. Wanahitaji muungano ambao ukipewa dhamana ya kusimamia rasilimali za nchi hii pamoja na katiba yetu ya nchi basi kutakuwa hakuna majuto kama ilivyo sasa chini ya CCM.
Hivi CUF itaishauri nini CHADEMA juu ya ung'ang'anizi wa kiti cha urais ikiwa Lipumba kila uchaguzi yeye ndiye huwa mwenyekiti wa CUF? Hivi Mbowe atamshauri nini Mbatia juu matumizi mabaya ya fedha za umma ukiwa CHADEMA mahesabu yake ni pasua kichwa? Hivi Mbatia atamshauri nini Slaa juu ubabe ikiwa yeye mwenyewe anaiongoza NCCR kama kampuni yake?
Vyama hivi ndio vinaunda huo UKAWA, na ndio vinajinasibisha na ukombozi ikiwa vitendo vyao havina tafauti na chama cha majambazi(CCM). Watanzania hawatakuwa tayari kuitoa CCM madarakani na kuingiza UKAWA, badala yake watakuwa radhi kuipa dola ACT na huko ndio kupenya kwenyewe.
Akihojiwa katika kipindi cha BARAGUMU chanell Ten katibu mkuu wetu alisema chama chetu kiko tayari kushirikiana na chama chochote ili mradi chama hicho kwa kiasi fulani kifanane na ACT katika itikadi na namna wa uendeshaji wa chama wenye kuzingatia uwajibikaji na uwazi. Kwa kauli hii na nikizingatia na uendeshwaji wa vyama vinavyounda UKAWA sitarajii hata kidogo kwa ACT kujiunga na UKAWA labda tu vyama hivyo vibadilike na kufanana na ACT. Kama havitabadilika ACT haina budi kupenya kati yao na CCM.
View attachment 197696
TATU: KUNING'INIA KWA CHADEMA.
Siasa za huku bara ziko tafauti kabisa na siasa za Zanzibar, tangu mfumo wa vyama vingi urudishwe CUF imeandelea kuwa chama kikuu cha upinzani upande wa Zanzibar wakati huku bara kofia hiyo imekuwa ikihama toka chama kimoja na kwenda kingine. Kwanini hivyo bara na kwanini hivyo Zanzibar? Si mada yangu kwa leo ila historia kwa upande wa Zanzibar ndio kila kitu.
NCCR ndio kilikuwa chama cha upinzani chenye nguvu huku bara tangu kilipoanzishwa na hata baada ya uchaguzi mkuu mwaka 1995(ingawa hakijawahi kuongoza bungeni), mwaka 2000 hadi tukielekea uchaguzi mwaka 2010 kofia hiyo ilikuwa inashikiliwa na CUF na kuanzia 2010 hadi sasa kofia hiyo inashikiliwa na CHADEMA.
Kuna jambo hakuna mwenye kulibishia hapa kuwa kila kofia hii ilipohama ilikiacha chama iliyoishikilia kikiwa dhaifu katika mambo inayoyapigania, misimamo na kupungukiwa na idadi kubwa ya wanachama na wafuasi. NCCR ilipoishiwa nguvu huku bara pia ilipokonywa mashabiki na wanachama wake wengi, kimsingi ilianza kupokonywa mashabiki na wanachama na chama cha CUF kabla hata kupokonywa rasmi kofia ya chama kikubwa cha upinzani upande wa bara katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000. Pia CUF ilianza kupokonywa mashabiki na wanachama wake na CHADEMA kabla ya chama hicho kupokonywa rasmi kofia ya chama kikuu cha upinzani mwaka 2010. Si wanachama na mashabiki wa kawaida vyama hivi vilikuwa vinapoteza lakini pia hata baadhi ya viongozi wake na wanachama waandamizi. Bahati mbaya watanzania wanaojishughulisha na ushabiki wa vyama ni walewale sababu ongezeko lao ni dogo sana. Hii ina maanisha nini?
Hii ina maanisha kuwa wanachama na mashabiki wa NCCR waliokipa nguvu chama hicho mwaka 1995, ndio hao hao walioipa nguvu CUF mwaka 2000, ndio hao hao walioipa nguvu CHADEMA mwaka 2010 na ndio hao hao baadhi yao waliomua kuanzisha na kujiunga ACT.
Mbishi pekee atakayekataa kuwa uanzishwaji wa ACT na kupata usajili wa kudumu wa chama hicho mara baada ya kudhaminiwa na wanachama zaidi ya 200 katika mikoa 18 ya bara na visiwani unatokana na nguvu ya asili ya NCCR. Wanachama wengi wa ACT hawakutoka kwa wananchi ambao hawakuwa na chama au hawakuwa mashabiki wa chama, wanachama wengi wa ACT wengi wao walikuwa wanachama wa CHADEMA, CUF na ADC. Waliokuwa viongozi wa CHADEMA katika mikoa mbalimbali wamejiunga na ACT na kundi kubwa la wanachama na mashabiki wa chama hicho, vivyo hivyo kwa CUF na ADC.
CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kilikuwa kinaituhumu CUF kuwa kibaraka wa CCM, lakini mara baada ya kuona chama hicho kinapoteza mvuto na wanachama wake na kinaendea kupoteza kofia yake, kikaona njia pekee ya kuendelea kubaki katika chati ni kuiangukia CUF na NCCR, kwa hivyo ajenda ya katiba ilikuwa njia tu kufikia lengo hilo la CHADEMA. Pamoja na hayo, nikiangalia nguvu ya CUF na NCCR, kwa vyovyote vile kuning'inia kwa CHADEMA ndio kuning'inia kwa UKAWA, na huko ndio kupenya kwa ACT kati ya UKAWA na CCM.
Hatuwezi kuukwepa ukweli kuwa NCCR na CUF vimejitahidi kurudisha hadhi yao vimeshindwa, CHADEMA imestuka kuwa inaenda kupoteza hadhi yake kwa ACT mara baada ya wanachama na waliokuwa viongozi wake kujiunga na ACT, hivi yenyewe CHADEMA inategemea muujiza wa UKAWA kuwa itapona ugonjwa unaowasumbua hata sasa CUF na NCCR? Thubutu labda viongozi walioipaisha na sasa kuishusha CHADEMA watoke katika ofisi za Ufipa, na si hivyo tu hata ile tabia iliyoifikisha CHADEMA katika anguko hili ikomeshwe, kinyume chake ACT inakwenda kukalia kiti cha CHADEMA na huko ndio kupenya kwa ACT kati ya UKAWA na CCM.
View attachment 197697
NNE: MASHABIKI SI WANACHAMA WA CHADEMA.
Vyama vyote vya upinzani isipokuwa ACT havina wanachama zaidi ya mashabiki, na hii ndio sababu iliyopelekea NCCR, CUF na sasa CHADEMA kupoteza nguvu. Vyama hivi vina mashabiki wa wanasiasa au mashabiki wa matukio ya kisiasa. NCCR ilikuwa na mashabiki wa Mrema na ajenda ya kuitoa CCM madarakani, CUF imepata nguvu kutokana na msimamo dhidi ya muundo wa muungano, CHADEMA imepata nguvu kutokana na matukio ya Buzwagi, EPA na Richmond, na UKAWA inapata nguvu hizi kutokana na ajenda ya KATIBA. Mashabiki wa ajenda ya KATIBA wataachana na UKAWA endapo likitokea ajenda nyingine kubwa au itakayowavutia kuliko hata ya KATIBA au suala la KATIBA likifikia mwisho huku mashabiki wa ajenda hiyo wakiwa wameridhika. Ikiwa CUF, NCCR na CHADEMA zimepoteza mvuto sababu ya kuhama kwa washabikiwa au kupoteza mvuto kwa ajenda zilizokuwa zinashabikiwa, UKAWA itawezaje kukwepa mtego huo?
Ndio maana ACT tunajikita katika kuzitangaza na kutoa elimu juu ya uzuri na manufaa ya itikadi yetu ya mrengo wa kati kushoto na falsafa yetu ya unyerere na ile misingi yetu kumi. Tunataka watanzania waikaribishe ACT katika nyumba zao kwasababu ya uzuri na manufaa ya itikadi, falasafa na misingi kumi ya ACT. Chama kitashughulikia matukio ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa kuongozwa na itikadi, falasafa na misingi kumi ya ACT.
Kwa kufanya hivyo tutakuwa na wanachama wa ACT na si mashabiki wa watu na matukio, na chama hakitayumba hata kidogo sababu ya kiongozi kutishia kujitoa au kujitoa kama ilivyo sasa kwa CHADEMA kinavyoyumbishwa kutokana na sakata la Mwigamba, Prof Kitila na Zitto. UKAWA wana mashabiki wa matukio na watu lakini ACT ina wanachama na mashabiki wa chama, na huku ndio kupenya kwa ACT kati ya UKAWA na CCM.
View attachment 197698
TANO: UBEPARI, UJAMAA NA ULIBERALI.
Tupozungumzia UKAWA katu huwezi kuepuka kuona mchanganyiko huo wa kiitikadi; ubapari wa CHADEMA, ujamaa wa NCCR na uliberali wa CUF. Vyama hivi kila kimoja kimeshindwa kujenga itikadi zao hizi kwa wanachama na mashabiki wao, hivi huo mseto wanakwenda kufafanua vipi hata waeleke kwa watazania kama si kujichanganya na kupoteza dira?
Wakati UKAWA wakivurugana juu ya misingi ya itikadi gani waisimamie na kutoka nayo mbele ya umma yenyewe ACT itakuwa inaendelea kutangaza misingi yake kumi inayozingatia misingi ya demokrasia jamii. Hivyo ACT inaenda kueleweka kwa haraka zaidi kuliko UKAWA, na huku ndio kupenya kwa ACT kati ya UKAWA na CCM.
SITA: WATANZANIA WAMECHOKA NA CCM, LAKINI HAWANA HILA.
Kuendelea kwa CCM kupewa ridhaa ya kuongoza dola na ushindi wa chama hicho katika chaguzi ndogo hakumaanishi kuwa watanzania bado wanaipenda CCM, ufisadi na kulewa madaraka kwa CCM kuna julikana vizuri kwa watanzania. Pamoja na kujulikana huko lakini bado wanaendelea kuichagua, hivi waache kuichagua CCM waichague CHADEMA ambayo kabla haijakabidhiwa dola imeshaanza kupata hati chafu? Hivi waichague CUF ambayo mwenyekiti wake ni mfalme? Kuchaguliwa kwa CCM ni kuthibiti kwa msemo wa ZIMWI likujualo halikuli likakwisha.
Vyama vinavyounda UKAWA na vyama vyote vya upinzani tulivyovikuta vimeshindwa kuonesha kwa vitendo ni kwa namna gani vitakuwa tafauti na CCM pindi vikipewa dola, badala yake vinaonekana vitakuja kufanya maovu makubwa kuizidi hata CCM. Watanzania walikuwa wanatafuta chama cha kuitoa CCM madarakani na sasa wameshakipata, na hivi ndivyo ACT inavyokwenda kupenya kati ya UKAWA na CCM.
ACT-TANZANIA ==========> TAIFA KWANZA.
UWAZI NA MABADILIKO ===> CHUKUA HATUA
Njano5.
0784845394.