Ndata
JF-Expert Member
- Mar 2, 2017
- 227
- 333
COMEDY ZA NDUGU ZANGU ACT.
Kwanza moja ya maombi makubwa ya ACT ni Chadema asishiriki uchaguzi, hii itampa nafasi ya kuwa chama kikuu cha upinzani na Zitto kuwa KB automatically. Hivyo Chadema wajue kabisa ACT wanalao kwenye hili.
Pili, Chadema kwenye movement yao ya NO REFORM NO ELECTION hakuna mahali popote wameomba sapoti ya chama chochote, wao wana malengo yao na wanajua ni namna gani watayafikia. Mnafiki anajitokeza na ku ACT kama vile yupo sambamba na Chadema ila leo Ado kagonga suti na kutimba Dodoma kuhakikisha wao wanakubaliana na CCM uchaguzi uwepo.
Baada ya kusaini wanaanza kutoa maandiko kibao kujitetea, hivi wanajitetea kwa nani? Wao ni wao na Chadema ni Chadema kila mmoja na mipango, malengo na njia zake kufikia mafanikio..
Anachofanya ACT ni kula kidogo Chadema na kula kidogo CCM hio ndio pumzi yake.
Swali ni kwakua wamekubali Uchaguzi ufanyike katika hali hii iliyopo, watakuwa na haki ya kulia wamefanyiwa faulo?
ACT sawa na Jahazi Asilia tuu, vyama maalum kuhalalisha mambo ya CCM zikiwemo chaguzi hizi zisizo za haki kwa malipo kidogo. Hivi vyama vipo pote duniani ingawa Africa imekuwa zaidi. Serikali kuwa na vyama vyao vya mfukoni na kuvitumia pale itapohitajika kuionesha dunia demokrasia ipo.
ACT kama alivyo Kiongozi wao wa Maisha Zitto Kabwe, hucharuka pale tuu makubaliano yao yanapokiukwa. Mfano ni baada ya Magufuli (RIP) Kumnyima Zitto uwaziri sote tuliona alivyoanza kuwa mkali.
Mwisho kabisa, ACT mshakubali kushiriki uchaguzi ujao pasipo mabadiliko yoyote, basi mjitahidi kukubaliana na matokeo ya kabla na baada ya uchaguzi. Wananchi tumewaona na tumewaelewa tayari.