Kuna jamaa alikuwa rafiki yangu wakati nipo chuo miaka kadhaa iliyopita. Sasa kuna siku alilala na msichana bila kupima. Baada ya kumaliza ngono akawa amemsisitiza akapime baada ya mwezi halafu amtumie majibu, msichana akamwambia sawa.
Kama mwezi mmoja hivi kupita jamaa alimkumbusha msichana kwenda kupima. Siku moja tumekaa chini ya mdigrii kwenye Vimbweta pale UDSM, kuna ujumbe wa simu ukaingia kwenye simu yake kutoka kwa yule msichana, ambao baadaye niliusoma, ulisomeka hivi:
"Hello, nimeenda angaza kupima nikapewa majibu ya kutatanisha, nimeambiwa nirudi baada ya miezi 3, hapa nilipo nimechanganyikiwa".
Baada ya jamaa kusoma ujumbe alianza kama vile kuweweseka, anajinyosha, anasimama, anakaa, anazungukazunguka huku na kule na kurudi huku akiwa ameinamisha kichwa.
Muda kiasi wa ukimya ulipita, halafu akaniuliza, hivi kama mtu ameambukizwa ukimwi mwezi mmoja uliopita, akipima leo inaweza kuonekana kama ameambukizwa au lah?
Nikamjibu, UKIMWI hauna maana kabisa, mtu aliyeambukizwa juzi usiku anaweza kukuambukiza wewe leo, lakini akipima hata baada ya miezi 3 inaweza kusoma negative, pia anaweza kupima akaonekana hana hata baada ya mwaka. Wewe uliyeambukizwa inategemea sababu mbalimbali, unaweza kupima hata baada ya miezi sita ikaonekana huna, na baada ya mwaka au miaka hata 2 na zaidi ukajitokeza.
Alichukua makabrasha yake akaondoka kimyakimya bila kuniaga huku akiwa anatembea kwa kupepesuka kama mlevi.
Niliporudi Hostel pale Mabibo nikamkuta room amelala na viatu kitandani, ndipo nikachukua simu yake kimyakimya na kusoma sms zilizonipa tukio zima kati yake na yule msichana.
Kusema ukweli, jamaa alianza kuishi kama mwehu kadri siku zilivyoenda. Baada ya siku tatu nilihama maana nilihisi angeweza kunidhuru au hata kunichanja na wembe aliojikata ili kama ana UKIMWI aniambukize na mimi.