Acheni maisha yaitwe maisha

Basi Nenda

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
20,138
45,807
Kuna picha nimeiona sehemu imenifanya niyatafakali sana maisha yetu hapa duniani.huyu mzee enzi za ujana wake au tuseme mwaka 1996-1997 hapo alikuwa ni mtu wa heshima zake,alikuwa na pesa,nyumba nzuri na gari nzuri bila kusahau kazi nzuri akiwa mshauri wa rais mobutu ila sasa ni masikini na omba omba mtaani
IMG_5398.png

Wapo vijana waliokuwa na vyeo vidogo tu jeshi la Zaire ila leo wanaishi maisha mazuri huko Ulaya lakini huyu mzee na Elimu yake yote na cheo kikubwa alichokuwa nacho leo yupo hivo,kutoka maisha ya mshahara wa zaidi ya tsh 20m kwa mwezi (makadirio ya haraka)
 
sijajua ilikuwaje ndio nafuatilia nini kilimkuta.lakini nina uhakika alikuwa na akiba ila kujua ilipoenda ndio tabu
lakini pia majumba ya watu wa karibu wa mobutu yalitaifishwa mwaka 1997
Inawezekana pia alipitiwa na fagio la mabadiliko ya waliochukua nchi,kufilisiwa sometimes kuwekwa jela etc.unajua Mobutu wengi walikuwa na hasira nae sana so isingewezekana mtu ajulikane kwamba alikuwa mtu wake wa karibu halafu asiguswe na wapinzani wa boss wake.
 
Inawezekana pia alipitiwa na fagio la mabadiliko ya waliochukua nchi,kufilisiwa sometimes kuwekwa jela etc.unajua Mobutu wengi walikuwa na hasira nae sana so isingewezekana mtu ajulikane kwamba alikuwa mtu wake wa karibu halafu asiguswe na wapinzani wa boss wake.

mkuu hiyo inawezekana ndio sababu maana nimefikilia sana sikupata jibu.hapo lazima visasi vimeusika kama ulivosema kwa sababu ni mtu ana Elimu kubwa angeweza kuajiliwa
 
Dada yangu, hili la kusomesha watoto litoe. Siku hizi watoto wetu si sawa na sie tuliosoma ili kukomboa familia. Unless ni wasichana huwa hawamtupi baba yao ila wavulana Mh!!!!
Wakishaoa basi wanasahau kuwa wana wazazi
 
hongera sana kwa kukumbuka wazazi
Ni majukumu yetu mkuu. Ila kwa sasa usipokuwa makini unakuwa sawa na huyo jamaa baada ya 80, hawa wetu siyo wa kuwategemea. Mambo yamegeuka sasa ambapo wazazi wetu waliacha kuwaendeleza wasichana (si kwa vile walikuwa hawawapendi ila resouces zilikuwa ni chache kiasi huwezi kuzitawanya kwa wote) waka invest kwa wavulana na kweli tukaleta returns hata kwa kusaidia watoto wa dada zetu ili wawasaidie mama zao ambao kutokana na umaskini hawakuendelezwa. Kizazi cha sasa kinafanya wazazi wasione umuhimu wa kuwa na watoto - Mojawapo ya sababu ya kuwa na watoto wengi zamani hapa Afrika ni social security; wazazi wali invest katika watoto. Ndo maana unaona nchi kama Kenya au west africa kila mtu anahakikisha mtoto wake angalau mmoja aende ulaya ili akomboe familia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom