Acheni kuuza magari kwa kuthaminisha thamani ya gari na NAMBA

byakunu

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
513
1,141
Hii trend ya kuuza gari mtu anaangalia usajili wa namba namba ya gari ni ya lini mfano EEM, DYL, DME ndo atamke bei ni ushamba sana unaendekezwa na washamba, Kwamba gari nzuri ni yenye namba latest?

Unakuta mtu anauliza kabsa namba gani? Tanzania tuna mambo ya kishamba sana. Kuna gari zina hali mbaya kabsa kuliko AAD ziko ovyo sana zinasajiliwa namba ya leo ndo mtu anaamini ni gari nzuri.

Sijui kifanyike nini kuondoa huu utaratibu wakipuuzi, magari mazuri yaliyo tunzwa vizuri yana hukumiwa na namba.
 
Namba ni kielelezo cha gari kujua muda ulioingia nchini(japo zipo watu wanapata serikalini na taasisi)
Soakiona namba anajua muda wa chombo kuingia nchini kisha mengine yanafata, wabongo sisi sio watunzaji saana, ni nadra mnoo uikute gari ishatumika miaka 15 bongo na haigongi wala haina ugonjwa wowote ni mtihani kidogo, japo wapo watunzaji wachache, ndio maana wengine wakisikia gari ya mdada sijui muhindi wanawahi kuiona.
 
Sirikali tukufu inazuia magari chini ya miaka 10 wewe unalalamika nini..Tuendelee kutembea kwa miguu shekh mpaka viatu vibanduke waache wenye uwezo wanunue miguu minne
 
Ni kweli kigezo cha kuangalia namba ni muhimu kina kupa picha ni gari ya mwaka gani japo mara nyingi hai guarantee uzima wa gari husika.
Lakini napenda kuwashauri watu, ukitaka gari ya kununua nenda kaikague hata kama ni namba E kagua gari kwa uhakika. Sipingani na wale wanaoangalia namba ila uzoefu wangu wa kununua na kuuza magari namba huwa inanipa "assumption" lakini gari sio namba.
 
nilinunua gari 2009 sikujali namba kabisa ilikuwa noah no b...nilijali gari nzuri kwanza mambo ya mamba nani alikuwa anazingatia....kikapita kipindi kirefu sana 2016 nikataka kununua gari nikawa nzingatia sana namba kila nikipishana na gari wee nikamenya dgp ndio nkajua sijui nkaanza kukutana na no aab vx zimesimama kama imeibwa ikabandikwa no....tokea hapo mi nakagua gari body engine diff sisomi namba kabisa...
 
Hii trend ya kuuza gari mtu anaangalia usajili wa namba namba ya gari ni ya lini mfano EEM, DYL, DME ndo atamke bei ni ushamba sana unaendekezwa na washamba, Kwamba gari nzuri ni yenye namba latest?

Unakuta mtu anauliza kabsa namba gani? Tanzania tuna mambo ya kishamba sana. Kuna gari zina hali mbaya kabsa kuliko AAD ziko ovyo sana zinasajiliwa namba ya leo ndo mtu anaamini ni gari nzuri.

Sijui kifanyike nini kuondoa huu utaratibu wakipuuzi, magari mazuri yaliyo tunzwa vizuri yana hukumiwa na namba.
Uko sahihi sana. Niko kwenye taasisi fulani, nimengalia cruiser za Kanisa Katoliki, zina namba AAF lakini utadhani zimeletwa mwaka huu, nikilinganisha na za umma. Gari ni matunzo, kuna namba D ni mbovu kuliko namba B
 
Ni kweli kigezo cha kuangalia namba ni muhimu kina kupa picha ni gari ya mwaka gani japo mara nyingi hai guarantee uzima wa gari husika.
Lakini napenda kuwashauri watu, ukitaka gari ya kununua nenda kaikague hata kama ni namba E kagua gari kwa uhakika. Sipingani na wale wanaoangalia namba ila uzoefu wangu wa kununua na kuuza magari namba huwa inanipa "assumption" lakini gari sio namba.
Kivipi number mkuu...huo ni ushamba..nilishawahi kuagiza gari japani ikaja imejaa kutu sehemu kibao ikabidi kuipolish tena..lakini usajili mpya huo..mshkaji wangu alinunua range kwa mtu namba C lakinimmiliki wa kwanza aliinunua 0km kutoka UK jamaa ni mmiliki wa pili na mpaka leo chuma iko vizuri sana..so kuna vitu vya kuzingatia lkn sio namba matter of fact watu nchi nyingine hawana huu utaratibu kabisa ni hapa kwa nyerere tu
 
Uko sahihi sana. Niko kwenye taasisi fulani, nimengalia cruiser za Kanisa Katoliki, zina namba AAF lakini utadhani zimeletwa mwaka huu, nikilinganisha na za umma. Gari ni matunzo, kuna namba D ni mbovu kuliko namba B
Nyingi zinakuja 0km mkuu..hizi namba E zimejaa mjini lakn nyingi zinakuja na 100k kuendelea ni craps
 
Hii trend ya kuuza gari mtu anaangalia usajili wa namba namba ya gari ni ya lini mfano EEM, DYL, DME ndo atamke bei ni ushamba sana unaendekezwa na washamba, Kwamba gari nzuri ni yenye namba latest?

Unakuta mtu anauliza kabsa namba gani? Tanzania tuna mambo ya kishamba sana. Kuna gari zina hali mbaya kabsa kuliko AAD ziko ovyo sana zinasajiliwa namba ya leo ndo mtu anaamini ni gari nzuri.

Sijui kifanyike nini kuondoa huu utaratibu wakipuuzi, magari mazuri yaliyo tunzwa vizuri yana hukumiwa na namba.
Sasa Kama serikali imeanza kupangia Gari ziingie Stand mpya za namba fulani tu sisi ni nani tusifute, Kiufupi ni mfumo rahisi wa kujua gari bado haijagongwa gongwa sana na makachanja wa Bongo wa chini ya mti, ambao kila fault kwenye gari wao ni nyundo naku Bypass.
 
Subiri ukutane na namba E kumbe imetoka hapo kisiwa ndui na iliingia Zanzibar 10yrs ago ila nimeivusha bara na kuipa usajiri mpya
 
Back
Top Bottom