Acheni kumshambulia Rais Magufuli personally, tumpe moyo!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,342
24,232
Wana JF, nasikitishwa sana na wana jukwaa wanaomshambulia Rais Magufuli on personal terms.

Tukumbuke, Magufuli ni binadamu ambaye tumembebesha nzigo mzito wa kutuongoza watanzania milioni 50.

Kama binadamu yeyote ana napungufu, maana si malaika kuwa hawezi kukosea.

Ila kutukana, kukejeli juhudi za dhati kabisa si tabia ya kitanzania.

Yes kuna wana JF wana mawazo mazuri ya kutia moyo, na tulione hili in goodlight.
Mfano mzuri ni huu wa Accacia kuanza kuelewa kuwa Magufuli si nguvu ya soda na kukubali kuchenjua mchanga wa madini humu nchini.

Tumpe pongezi panapostahili.
 
Mkuu sidhani kama watakuelewa humu ndani... Member wengi humu ndani wanaendeshwa na mihemuko ya Kichama zaidi... siku zote wamekalia kuleta hoja za kumkebehi Mhe. Rais bila kujua kuna mambo mengi tu keshaifanyia serikali yetu...

Maendeleo ni sawa na mwanamke mzuri hajifichi.
Ebu tuseme kafanya kipi tangible zaidi ya matamshi km yupo kwenye uchaguzi
 
Wana JF, nasikitishwa sana na wana jukwaa wanaomshambulia Rais Magufuli on personal terms.

Tukumbuke, Magufuli ni binadamu ambaye tumembebesha nzigo mzito wa kutuongoza watanzania milioni 50.

Kama binadamu yeyote ana napungufu, maana si malaika kuwa hawezi kukosea.

Ila kutukana, kukejeli juhudi za dhati kabisa si tabia ya kitanzania.

Yes kuna wana JF wana mawazo mazuri ya kutia moyo, na tulione hili in goodlight.
Mfano mzuri ni huu wa Accacia kuanza kuelewa kuwa Magufuli si nguvu ya soda na kukubali kuchenjua mchanga wa madini humu nchini.

Tumpe pongezi panapostahili.
Kamwambie aache kujishambulia mwenyewe.

Rais anayesema hakujiandaa kuwa rais, kasukumwa na wenzake tu (baada ya kusema hakupanguwa, kachukuwa fomu mwenyewe), kazi ngumu sana analialia kila siku, mara anatukana mawaziri wake wapumbavu, wakati yeye ndiye kawateua uwaziri, na hivyo anatuambia kuwa yeye ndiye mpumbavu zaidi yao.

Na anayesema ujinga mwingi kama huo.

Rais huyo kashaanza kujidharaulisha yeye mwenyewe.

Kwa hiyo mwambie mwenyewe alinde kauli zake, alinde matendo yake.

Ama sivyo anajishambulia mwenyewe kabla mtu mwingine hajamshambulia.
 
Mkuu sidhani kama watakuelewa humu ndani... Member wengi humu ndani wanaendeshwa na mihemuko ya Kichama zaidi... siku zote wamekalia kuleta hoja za kumkebehi Mhe. Rais bila kujua kuna mambo mengi tu keshaifanyia serikali yetu...

- Nilisoma kwa mkopo wa 70% nikawa natafuta 30% za kumalizia Ada

- Nimehitimu chuo Magufuli kafunga ajira ( Anatoa viajira kiduchu mpaka akijisikia mwenyewe )

- Nimeamua kuwa machinga kwa vipesa kidogo nilivyopata, kila siku nafukuzwa na migambo kama jambazi

- Nikajaribu kuanzisha biashara rasmi hata kabla ya kuuza unakadiriwa kodi kubwa kuliko mtaji.

- NDOTO ZA VIJANA WENGI ZINAKUFA, yeye yuko busy na kina MANJI, LISSU, CHADEMA, SETHI

- Watumishi mwaka wa 3 sasa wanaishi kama MANAMBA hawana AMANI kwa kutishiwa kufutwa KAZI huku watu wake wakilipana maposho ya LAKI 4 PER DAY!

- Nchi imemshinda kabisa huyo jamaa, Amebaki na kelele, matamko na miropoko tu ile ile tu majukwaani
 
Back
Top Bottom