Achana na tetesi: Lil Ommy, go and get 'em, bro!

mayowela

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
2,124
1,746
Baada ya Mtangazaji mwenye ushawishi wa kituo cha Times FM Ommary Rajabu Saleh Tambwe aka Lil Ommy kuaga rasmi kuwa hatoendelea kuwa mfanyakazi wa kituo hikch alichokifanyia kazi kwa muda mrefu akitokea VoT FM (Voice of Tabora FM) takribani miaka 10, tetesi zimekuwa nyingi.

Wengine wanadai nguvu ya pesa imemnyakua, na kuwa anaenda kujiunga na kituo cha redio cha Wasafi FM.

Ukirejea kauli zake kadhaa na mahojiano aliofanya kwenye kipindi cha Salama, alidai alishawahi kukutana na Marehemu Ruge na alikuwa akimuhitaji ila walikuwa kwenye mazungumzo.

Kikubwa alisisitiza ofa ni nyingi ila hawafiki kwenye makubaliano/muafaka na kupelekea abaki kwenye kituo mama anachofanyia kazi.

Lil Ommy ana deal nyingi sana. Pengine mshahara wa Times ulikuwa wa kawaida ila aliamua ajitengenezea himaya akiwa pale.

Kuna maswali kadhaa ya kujiuliza:

Je, ni kweli anaenda kujiunga na Wasafi FM?

Je, Clouds wanatimiza mazungumzo yaliyoanzishwa na Ruge?

Anaenda kujenga empire yake na kuwa mkubwa zaidi kama walivofanya Sky Walker, Sam Misago na MillarAyo?

Anaenda ku-deal na kipindi chake walichokuwa wameanza kukitengeneza na Raque?

Kuna kampuni kubwa imemtaka kumsimamia kwa ukubwa zaidi ndiyo maana kasepa na timu yake?

Tuache muda uzungumze na tuachane na "Tetesi", pesa anayopata/alizopata kutoka kwenye matangazo ni nzuri: Minutes Maid, TOTAL, Johar Rotana, Coca Cola, nk zinaweza kumfanyia kitu na siyo kwenda kuwa chini ya watu tena.

NB: Next week, J3, atawajuza nini anafanya na yupo wapi.

Tchao!
 
huu mwandiko wa Lil Ommy kabisaa
 
Ni tetesi au ni kweli maana hata dida ilianza hivi hivi wa kasema ni tetesi kumbe ni kweli
FB_IMG_1581764819798.jpeg
Screenshot_20200215-134108_YouTube.jpeg
 
Sheria ndo zinawabana ili uweze kipata kibali cha kusikika nchi nzima lazima uwe umetimiza angalau miaka mi3 toka uanze kurusha matangazo ya radio yako kwa iyo sio kwamba diamond hana uwezo bali ni taratibu na masharti ndo yanambana we subir atimize hivo vigezo uone ni swala mda mfupi kuskika nchi nzima.
Itasurvive Kama Mondi mwenyewe akaweka misingi mizuri na mfumo imara bila kumtegemea yeye Kama alivyofanya mengi ipp media.
 
Sheria ndo zinawabana ili uweze kipata kibali cha kusikika nchi nzima lazima uwe umetimiza angalau miaka mi3 toka uanze kurusha matangazo ya radio yako kwa iyo sio kwamba diamond hana uwezo bali ni taratibu na masharti ndo yanambana we subir atimize hivo vigezo uone ni swala mda mfupi kuskika nchi nzima.
WCB waanze na coverage kwanza sasa redio inapatikana Dar na Pwani ndio unaenda kusajili watangazaji maarufu kama wote?
 
Back
Top Bottom