Acha waseme Chama cha Mapinduzi kina wenyewe

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Hii ndiyo habari ya mjini kwa sasa. Kauli ambayo ameitamka waziwazi bila kificho NAPE MOSSES, MBUNGE WA MTAMA.

Kwa hali hiyo na maana pana ni kwamba hii nchi imepo mikononi mwao hakuna wa kutoa maneno kwa sasa mheshimiwa polepole amebaki kuwa kiroboto ambaye muda wowote atanyunyuziwa dawa na atapotea hatosikika tena!

Ndugu zangu wananchi tuwe makini na makundi haya ambayo yanaonesha waziwazi hii nchi kuwa ni ya kwao na kutaka kuaminisha umma bila wao hakuna mambo yanaenda na bila wao CCM hakuna CCM.

Chama cha Mapinduzi hakipo kwa ajiri ya kutengeneza ulaji wa vikundi vya watu wenye mlengo mmoja hasa wa kinyonyaji dhidi ya nchi yetu, kwamba mtoto wa flani kila inapotokea nafasi serikalini lazima awemo haijalishi utendaji wake uwe mzuri au mbaya.

Nchi hii kama itaendeshwa kindugu kikundi cha watu na wenye uroho wa madaraka watu wa kipato cha chini wataendelea kuumia, kunakitu kinaitwa CONNECTION zama zimerudi vilevile kama huna anwani kubwa na watu wenye nafasi kubwa serikalini sahau kupata kazi! Baadhi ya watu hasa viongozi wa CCM wanashindwa kuongea kwani inaonekana waziwazi kuwa maisha yao wamewekeza kwenye siasa na wanaamini wakiongea watakuja kukatwa mbeleni kwenye ubunge iwe udiwani.

Mimi niwakumbushe kuwa kwa sasa chama kimerudi kwa wenyewe kama ni kukatwa jina utakatwa tu hata usipoongea mda unakuja wale wote waliotemwa awamu ya tano kwa kuwa awamu ya nne waliboronga wanarudi kama kawaida na hao ndio wapiga zumali wakuu kuitetea serikali huku watu wenye kipato cha chini wakiumia na baadhi ya rasilimali zikitoroshwa na kuibwa! Mtakumbuka ya escrow viongozi wakubwa kila mtu alisema yake pesa hazikuwa za umma wengine wakisema za umma!

Pamoja na sauti kupazwa nani aliyeshughulikiwa zaidi ya kutolewa kwenye nafasi aliyokuwa nayo! Umeiba bilion 300 unaambiwa ujiudhuru na bado unapitishwa na ccm unakuwa mbunge unaendelea kutetea jimbo lako! Watu wenye utendaji mzuri wanaachwa wanachaguliwa hao hao.

Msingi mkuu kwa sasa tusimuone polepole ni mtu mbaya wote tupaze sauti tupate KATIBA MPYA

*KATIBA MPYA MWAROBAINI WA NCHI YETU
ZAMA ZA UNANIJUWA MIMI NI NANI TAYARI ZIMESHAANZA KUOTA MIZIZI TENA*
 
Huyu mpuuzi anadhania hii nchi ni ya ukoo wake. Hako ka kikundi kake ni suala la wakati tu. Watanzania sio wajinga kiasi hicho.
 
Wacha wapuruane wenyewe maana hakuna cha maana wanacho kifanya ndani ya taifa hili
 
Sukuma gang wajue kabisa kuwa hii nchi IPO mikononi mwa wenyewe akina Nape....Mzee WA msoga ni Mafia kwelikweli kama ameweza kuirudisha nchi mikononi mwake nyie sukuma gang ni Nani?
 
Sukuma gang wajue kabisa kuwa hii nchi IPO mikononi mwa wenyewe akina Nape....Mzee WA msoga ni Mafia kwelikweli kama ameweza kuirudisha nchi mikononi mwake nyie sukuma gang ni Nani?
Ipo siku inakuja wale mema ya nchi watakuja kuyatapika * KATIBA MPYA MHIMU KWA SASA NA KIZAZI KIJACHO*
 
Tutamkumbuka sana huyu mzalendo wakweli kabisa kuwai kutokea nchini kwetu.
FB_IMG_16355106496066878.jpeg
 
Nape ni mmoja wa Kikundi cha Wahuni kinachomzunguka Mama Rais. Hajamaliza mwaka, tumpe nafasi pamoja na kwamba maamuzi anayotoa si yake ila ya shoga na hicho kikundi.

Hivyo, basi 2025 siyo mbali kama vyama vya upinzani vitajipanga sawasawa, kwa maana ya kuandaa na kuzieleza kwa wapiga kura Sera mbadala zenye kubeba makundi yote kwenye safari ya maendeleo.
 
Hata chama kilipoondoka mikononi mwa wenyewe watu waliendelea kukatwa sana majina.
 
Back
Top Bottom