ACHA MFUPA UNAKUPOTEZEA MUDA

ACHA MFUPA UNAKUPOTEZEA MUDA

101 East

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
1,057
Reaction score
2,257
*Masaa machache yalopita..*
Mbwa amenikumbusha kitu kikubwa sana katika tukio hili..
Gari ndogo nililokuwamo nikienda kwenye pilika za maisha ilikuwa speed kama 80/90 hivi....
Ghafla tukamwona Mbwa akijitahidi kushindana na speed ya gari kuvuka barabara....
Sikutamani kabisa kuona akigongwa..na moyoni nikawa natamani ajitahidi kuongeza mwendo..
Gari likiwa limekaribia kabisa ....
Nikaona mbwa ameongeza mwendo ghafla na kufanikiwa kuvuka....pumzi ikanishuka.
Lakini kuna kitu tulikiona kimedondoka kabla mbwa hajaweza kuongeza mwendo....
Nikamwomba dereva turudi nyuma kidogo..
Nilipoona kitu mbwa alichodondosha...Nikajifunza somo kubwa sana..
MBWA alidondosha
*Mfupa wa nyama* .....
Simple.....Ilifika mahali mbwa aliona bora aache mfupa apate speed aokoe maisha!!!!!
*Hii ni akili kubwa sana*
*_ACHA MFUPA_*
KUNA MIFUPA TUMEING'ANG'ANIA 2017
TUKIFANIKIWA KUWAMAJASIRI WA KUACHIA MIFUPA TULOING`ANG`ANIA ....MWAKA 2018 TUTAKUWA WA MAFANIKIO MAKUBWA SANA.
KUNA MIFUPA YA KILA AINA TUMEING`ANG`NIA *2017*
_*NA HAKIKA IMETUKWAMISHA MNOO*_
HEBU TUFANYE MAAMUZI MAGUMU..
TUSIVUKE 2017 NA MIFUPA YETU.
*TUIDONDOSHE HARAKA SANA*
KUTOKUHUDHURIA IBADANI KWA WAKATI NI MFUPA...
_UZITO TULIONAO WA KUOMBA MSAADA WA MAWAZO NI MFUPA.._
_KUTUMIA MBINU ZILE ZILE ZINAZOSHINDWA NAO NI MFUPA.._
_KUDHANI KWAMBA HELA PEKE YAKE INAWEZA KUKULETEA FURAHA..HUU MFUPA MGUMU SANA_
_KUTO WAHI KAZINI NA KUTOTIMIZA MAJUKUMU YETU IPASAVYO NI MFUPA_
_KUTOHUDHURIA IBADA HUU HATA FISI HAWEZI KUULA_
_KUTOKUJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA NI MIFUPA_
_KUFURAHIA KUONA WENZETU WANASHINDWA WAKATI TUNGEWEZA WASAIDIA WAKAFANIKIWA NI MIFUPA_
HII NI BAADHI TU YA MIFUPA TULIYO BEBA.
*TUDONDOSHE MIFUPA....* *ILI 2018 UKAWE MWAKA WA MAFANIKIO KWA KILA MMOJA WETU*
MUAMBIE JIRANI YAKO DONDOSHA MIFUPA INAKUCHELEWESHA.
*I WISH YOU HAPPY NEW YEAR 2018*
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom