Acacia Yaikana Barrick Mchana Kweupe!. Yatoa Press Release na Kumruka Barrick Kuwa Haijui Chochote Kuhusu Makubaliano Yoyote na Tanzania

Pia ni tatizo la serikali kudanganya uma! Barrick wenyewe wanasema watapeleka mapendekezo yote kwenye bodi ya ACACIA kwa ajili ya approval lakini serikali inasema BARRICK wamekubali kila kitu walichojadili wakati approval bado kutoka ACACIA

Mwisho wa siku usishangae migodi ikifunguliwa bila mirejesho ya nini walikubaliana
Tatizo ni lugha wanayotumia kwa makubaliano. Barick wanatumia kizungu, sasa anayemtafsilia magu ndye anayekuwa anamdanganya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida kubwa sana tuliyonayo ni kukariri tukidhani tumesoma na kuelimika. Sishangai mambo yetu hayasogei.
Barrick owns the deal....Acacia came into picture to meet specific demands. Whether in open or in secrecy, that is no longer possible.
Hawa jamaa wanataka kufanya biashara bila kuathirika na ujinga tulionao na kupenda rushwa kwetu.
Wamewaachia Acacia mnayoipenda wanahangaika na serikali maana wanajua kabisa hawana namna.
They are majority shareholders. Acacia watawazuiaje kwa mfano?

Siku deal liki mature natembea uchi toka butiama hadi chato, ntashangilia kwa kurukaruka na kujinyea hovyo.
 
Maweeeee! Hapa tumeliwa (kama sio kutiwa) mchana kweupe. Kiko wapi sasa? Zile mbwembwe zote za kujifanya kutetea rasilimali za taifa ziko wapi? Tuwasubiri matutusa wa Lumumba sasa waje hapa kutoa mapovu yao pamoja na kutunisha mknd yao mipana. Tumekwishaaaaaa!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna deal litakalofanywa na vichaa litakaloleta neema, maana unapokuwa kichaa unakuwa incapacitated, you cant negotiate terms exactly but you will endup with press release, serikali ya ma press ni serikali tapeli.
 
Hakuna deal litakalofanywa na vichaa litakaloleta neema, maana unapokuwa kichaa unakuwa incapacitated, you cant negotiate terms exactly but you will endup with press release, serikali ya ma press ni serikali tapeli.
serikali ikionana tu na wanaume hao wanakuja na press release
 
Lissu ndio anaharibu, ni ningekuwa JPM kama issue kubwa kwa Wazungu hasa Wamarekani ni rasilimali za nchi nawaachia tu, ili nione kama upinzani utanitoa madarakani.
 
Sisi hatuhusiki na makubaliano yao kati ya accacia na barrick,tunae deal with naye ni barrickGold,body approval or disapproval ya accacia katika madai yetu haituhusu na hayana msingi wowote kwetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi
Salaam.
Angalizo la Uzalendo.
Naomba kuanza bandiko hili na angalizo la uzalendo wa kweli wa nchi yako, ni pale unapo note nchi yako inataka kupigwa changa la macho, rais wako anataka kudanganywa mchana kweupe, unatoa angalizo ili kuwagutusha kabla, ili likija kutokea kuwa hakuna excuse kuwa viongozi wetu hawakujua.

Kuhusiana na sakata la Makinikia na Mazungumzo kati ya serikali yetu na Barrick huku mhusika Mkuu Acacia akiwekwa pembeni, leo yamefanyika mambo makubwa matatu.
Jambo la kwanza ni Barrick ambaye ndiye mmiliki wa Acacia, ametoa press release kwenye website yao kuhusu mazungumzo na Tanzania. taarifa hiyo ya Mark Bristow, President and CEO of Barrick. inapatikana hapa Barrick Gold Corporation - Barrick and Tanzanian Government Progress Discussions in Settlement of Acacia Disputes
Press release hiyo imesema hivi
Barrick and Tanzanian Government Progress Discussions in Settlement of Acacia Disputes


Ufafanuzi mfupi wa taarifa ya Barrick inasema Barrick na Serikali ya Tanzania leo wamefikia mapendekezo ya kuumaliza rasmi mgogoro wa makinikia kati ya Acacia na serikali ya Tanzania. Taarifa hiyo imesema. wamekubaliana mambo matatu
  1. Itaundwa kampuni mpya kuimanage Acacia in Tanzania
  2. Tutagawa 50/50 za economic benefits ambapo ndani ya hiyo economic 5-% ya Tanzania itajumuisha zile 16% shares, royalties na taxes zote
  3. Watatulipa dola milioni 300 to resolve outstanding tax claims.
Taarifa hii ya Mark Bristow, President and CEO of Barrick, imesema proposal hiyo, itawasilishwa kwenye bodi ya Acacia in the near future (haikusemwa lini), lakini imesisitiza Bodi ya Acacia ndio yenye mamlaka ya mwisho kukubali au kukataa proposal hiyo.

Jambo la pili ni Baada ya taarifa hii, Acacia nao, wakatoa press release kwenye website yao,
Leo leo, Acacia wametoa Press Release kuwaruka Barrick

Jambo la tatu ni Bosi wa Barrick Afrika, leo katinga ikulu yetu kumuona rais wetu na Taarifa ya Ikulu ni hii kuhusu mazungumzo hayo

My Take.
Huu ni uchambuzi wangu kuhusu taarifa zote tatu naomba niuweke in points format ili ikitokea tunabishana mahali, tubishana kwa hoja kuhusu kifungu fulani.
  1. Taarifa ya kwanza ni habari njema kuwa hatimaye mazungumzo haya yamefikia mwisho na wamekubaliana mambo matatu ya msingi.
  2. Itaundwa kampuni mpya kuimanage Acacia in Tanzania, hili limekaa vizuri
  3. Tutagawa 50/50 za economic benefits ambapo ndani ya hiyo economic 5-% ya Tanzania itajumuisha zile 16% shares, royalties na taxes zote. Mwanzo tulielezwa tutagawana faida, kumbe sasa sio faida tena bali imekuwa ni Economic benefits. Aliyetutangazia tutagawa faida ni rais wetu na Waziri wetu Kabudi, alifafanua vizuri. Kwa vile haya sasa ndio makubaliano ya mwisho, hii maana yake ni ama rais wetu pale mwanzo alipotoshwa, na waziri alipotosha, ukweli wenyewe sasa ndio huu, ama tangu mwanzo ilikuwa ni economic benefits tatizo ni lugha za watu. Hili mimi nililiuizia rasmi humu Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la kugawana 50/50 ya faida ni kweli au ni changa la macho tu?. - JamiiForums
  4. Watatulipa dola milioni 300 to resolve outstanding tax claims. Deni tunalowadai ni do;a bilioni 190, Ile dola milioni 300 ya goodwill iliahidiwa kuonyesha nia njema, lakini sasa ndio pekee inatajwa kama settlement deal!. Hapa kuna changa la macho!, tusubiri hiyo settlement deal yenyewe maana hizi lugha za watu ni shida.
  5. Kule mwisho anaposema makubaliano yoyote lazima yaridhiwe na Acacia, who is this Acacia kama mmiliki wa Acacia ni Barrick na mazungumzo hayo sio tuu ni serikali ya Tanzania na Barrick, nali ni makubaliano ya rais wa Tanzania na rais wa Barrick, baada ya kukubaliana then kuna mtu mkubwa zaidi yao ndiye ataamua kutekeleza au laa!. hii haijakaa vizuri na niliizungumzia hapa Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye uamuzi wa mwisho ni Acacia!, Kwanini hakushirikishwa?!. Je, Tutalipwa?. - JamiiForums
  6. Tukija kwenye taarifa ya Acacia, kiukweli kabisa haijakaa vizuri na hii sii dalili nzuri, wewe kama mwana jf, be the first to know from me, kuwa mapendekezo yoyote ya settlement kati ya Barrick na Tanzania, hata yakifikishwa kwenye Bodi ya Acacia, yatakataliwa!, Kitakachofuata ni baba Barrick ndiye atalipa fedha hizo, Kisha atamwadhibu mtoto jeuri huyu kwa kuivunjilia mbali Acacia na kuunda Kampuni mpya yenye bodi yenye Watanzania.
  7. Sababu za kusema hivi ni huyu Acacia ni mtoto tuu, baba ni Barrick, haiwezekani baba azungumze, na kutuma ujumbe kuja kuzungumza na rais wetu na atoe ahadi kwa rais, kisha atoe press release kuwa mtoto ataarifiwa halafu wewe mtoto, licha ya kusoma Press Release ya baba, halafu wewe mtoto unatoa press release kumkana baba yako kuwa bado hujaarifiwa!. huu ni ujeuri wa aina gani au hiki ni kiburi cha aina gani?, kiafrika hapa mtoto unaweza hata kupata laana, lakini mambo haya kwa wenzetu wazungu tena jeuri hii ya mtoto huyu haikuanza leo na hapa niliwahi kuizungumza Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto Anatakiwa Kunyamaza. Bora Wafungashe Tuu, Waondoke? - JamiiForums
  8. Nikija kwenye taarifa ya Ikulu taarifa ya Ikulu, inaonyesha sasa the settlement ni ile dola milioni 300 tuu, ambacho sasa kinaitwa kifuta machozi ya zile dola bilioni 190!. Niliwahi kutoa angalizo humu kuwa rais Mkapa alidanganywa akadanganyika, JK pia akadanganywa akadanganyika, nikasema naziona dalili za rais Magufuli kutaka kudangaywa, kama tume settle dola bilioni 190 kwa dola milioni 300, tuelimishwe labda tutaelewa. Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika? - JamiiForums
  9. Pia taarifa ya Ikulu imethibitisha mgawo wa 50/50 ni wa economic benefits, hili linahitaji ufafanuzi wa ziada.
  10. Msingi mkuu wa yote haya ni mgogoro wa makinikia. Tulizuia makontena ya mchanga, kwa sababu tunaibiwa kwa kutokujua, kilichomo, ili tujue tunaibiwa nini, ilibidi ule mchanga uchenjuliwe ndipo tupigiane hesabu za kweli. Sijasikia tena kuhusu ununuzi wa kichenjulio, kiukweli mchanga ukiondoka bila sisi kujua kilichomo, kiukweli sitashangaa bali nitaamini sisi Watanzania .... naomba nisimalizie
Hitimisho.
Watanzania wote wazalendo wa kweli wa taifa hili, tumuunge mkono rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli katika vita vya kulibda rasilimali zetu ndidi ya mabeberu, na kama una jicho la tatu la kuangazia visivyoonekana na wenye macho mawili tuu, then share what you see which others dont see so that we can all see, kwenye hili, there is something fishy.

Nawatakia Jumatano njema
Paskali

Rejea kuhusu makinikia

Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa Kishika Uchumba Cha Dola Milioni 300 - JamiiForums

Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa Kishika Uchumba Cha Dola Milioni 300

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi? - JamiiForums"]

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi? - JamiiForums

Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa? - JamiiForums

Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie Kwenye Madini Tuu na Gesi Jee?!. - JamiiForums

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike! - JamiiForums

Wataalamu Hawa Wachunguzwe!,Jee Kuna Posibility Walihongwa Kutoa Ripoti Kuwa "Tanzania Hatuwezi?!". - JamiiForums

A Compromised Possibility: Iweje Ripoti ya Kamati ya 2 iibukie Acacia-London kabla ya kwa Magufuli? - JamiiForums

Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika? - JamiiForums

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!. - JamiiForums

Makinikia: Je, Vyombo Vya Habari Vifukue Makaburi ya Chanzo, Au Kushangalia Tuu Matokeo?.Jicho Letu. - JamiiForums

Zita Act Retro-Respectively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo?, Can we Stand?, Do we Have The Guts?. - JamiiForums

Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto Anatakiwa Kunyamaza. Bora Wafungashe Tuu, Waondoke? - JamiiForums

Paskali huwa kuna siku unaonyesha uwezo wako, njoo huku ili tukupe ubunge ukaonyeshe umahiri wako kule mjengoni, ila baada ya yule mzee mgonjwa atakapoondoka kwenye kile kiti maana akili zake zimeliwa na kale kaugonjwa hoja zenye nguvu anazizuia na kale kabinti kapate mafua ya nguruwe kadhindwe kuhudhuria vikao vyooote mjengoni
 
Msukuma kila siku ni kupigwa tuu....tangu ameingia ametuaminisha tutapata noah....mara Balimi....sasa hata jojo hakuna... korosho nayo kapigwa....sijui wakenya bado simu zao hazina chaji?

Washauri wa nchi mko wapi?
Hizi hasara na aibu kwa taifa mpaka lini?
 
Pascal Mayalla hongera sana kwa bandiko lako la Kizalendo. Ninavyoana kama kuna delaying technique ya hao jamaa ambao huwezi kujua kati yao nani mkubwa.
Mwanzoni things were very clear kwamba tulijua nini tunawadai.
As days go on naona kama tunapoteza focus ya nini hasa tunawadai na nini tunataka.
Lazima tujue bado hawa jamaa wako nchi wakifanya operation zao. Sina shaka na maono ya Rais Magufuli kwa nchi yake lakini nafikiri bado mawaziri na wataalam wake hawajanya vya kutosha kuainisha nini Tanzania inaenda kupata kutoka kwa hao jamaa.
Haya modelity ya kupata chetu bado haijulikani vizuri.
Nani atatupa chetu saaa tukomae nane kati ya Barrick na Acacia maana naona kama wanatupiana mzigo.
Wazungu ni welevu sana bila kuwabana vema tutazeeka bila kulipwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eh mbona hawajakana?
Haya makubaliano si mapya na hayana tofauti sana na yale ya mwaka 2017 Mwenyekiti wa zamani wa Barrick, John Thornton, alipokutana na Rais Magufuli. Ambao wamefaidika na tangazo hili mpaka sasa ni Acacia ambao hisa yao imepanda kwa asilimia 6%.

Kwa kweli haya hayakuwa makubaliano bali ni mapendekezo na kama kawaida tunapiga vigelegele kwa mapendekezo ambayo si lazima yakubalike kwa wahusika ambao ni Acacia. Tanzania ni kama kichwa cha mwenda wazimu.


wanaweza vipi kukana kauli ya mmiliki wao?
Mzee mwenzangu, nani anammiliki nani? Hebu soma hii taarifa...

Barrick and Tanzania agree on October 2017 terms

Acacia Mining’s (LSE:ACA) Tanzania crisis looks a step closer to being resolved, two years after the government banned concentrate exports.

New Barrick CEO Mark Bristow said the confirmation of the October 2017 arrangement was in progress.

"Significant amounts of real value have been destroyed by this dispute and, in Barrick`s view, this proposal will allow the business to focus on rebuilding its mining operations in partnership with their respective stakeholders, and most importantly long-suffering investors, including Barrick," he said.

Barrick says it is not in control of Acacia and so the proposal will now go to the miner's board for approval.

There have been reports Bristow is interested in bringing Acacia back into Barrick.

Acacia stopped mining at Bulyanhulu and Buzwagi after the export ban, just processing tailings and stockpiles, respectively.

The miner's share price increased 6% in London on the news to £2.40 (US$3.13) per share.

Acacia's market capitalisation is half what it was before the concentrate ban came in.

Jefferies analyst Alan Spence said an Acacia shareholder vote could take place in the September quarter, after being signed off by the board and the UK listing authority.

"Assuming a successful shareholder vote and the lifting of the concentrate export ban, Acacia could fairly quickly monetise the $240 million worth of concentrate stockpiles," he said.

Tatizo ni lugha wanayotumia kwa makubaliano. Barick wanatumia kizungu, sasa anayemtafsilia magu ndiye anayekuwa anamdanganya
Eti proposal ni makubaliano! Badala ya kutafsiri kwamba wamekubaliana kuwasilisha hayo mapendekezo kwa wahusika, Acacia, wao wanadai wamekubaliana kutekelezwa kwa mapendekezo. Lugha, lugha, lugha...
 
Back
Top Bottom