Acacia Yaikana Barrick Mchana Kweupe!. Yatoa Press Release na Kumruka Barrick Kuwa Haijui Chochote Kuhusu Makubaliano Yoyote na Tanzania

Wanabodi
Salaam.
Angalizo la Uzalendo.
Naomba kuanza bandiko hili na angalizo la uzalendo wa kweli wa nchi yako, ni pale unapo note nchi yako inataka kupigwa changa la macho, rais wako anataka kudanganywa mchana kweupe, unatoa angalizo ili kuwagutusha kabla, ili likija kutokea kuwa hakuna excuse kuwa viongozi wetu hawakujua.

Kuhusiana na sakata la Makinikia na Mazungumzo kati ya serikali yetu na Barrick huku mhusika Mkuu Acacia akiwekwa pembeni, leo yamefanyika mambo makubwa matatu.
Jambo la kwanza ni Barrick ambaye ndiye mmiliki wa Acacia, ametoa press release kwenye website yao kuhusu mazungumzo na Tanzania. taarifa hiyo ya Mark Bristow, President and CEO of Barrick. inapatikana hapa Barrick Gold Corporation - Barrick and Tanzanian Government Progress Discussions in Settlement of Acacia Disputes
Press release hiyo imesema hivi
Barrick and Tanzanian Government Progress Discussions in Settlement of Acacia Disputes

Ufafanuzi mfupi wa taarifa ya Barrick inasema Barrick na Serikali ya Tanzania leo wamefikia mapendekezo ya kuumaliza rasmi mgogoro wa makinikia kati ya Acacia na serikali ya Tanzania. Taarifa hiyo imesema. wamekubaliana mambo matatu
  1. Itaundwa kampuni mpya kuimanage Acacia in Tanzania
  2. Tutagawa 50/50 za economic benefits ambapo ndani ya hiyo economic 5-% ya Tanzania itajumuisha zile 16% shares, royalties na taxes zote
  3. Watatulipa dola milioni 300 to resolve outstanding tax claims.
Taarifa hii ya Mark Bristow, President and CEO of Barrick, imesema proposal hiyo, itawasilishwa kwenye bodi ya Acacia in the near future (haikusemwa lini), lakini imesisitiza Bodi ya Acacia ndio yenye mamlaka ya mwisho kukubali au kukataa proposal hiyo.

Jambo la pili ni Baada ya taarifa hii, Acacia nao, wakatoa press release kwenye website yao,
Leo leo, Acacia wametoa Press Release kuwaruka Barrick

Jambo la tatu ni Bosi wa Barrick Afrika, leo katinga ikulu yetu kumuona rais wetu na Taarifa ya Ikulu ni hii kuhusu mazungumzo hayo

My Take.
Huu ni uchambuzi wangu kuhusu taarifa zote tatu naomba niuweke in points format ili ikitokea tunabishana mahali, tubishana kwa hoja kuhusu kifungu fulani.
  1. Taarifa ya kwanza ni habari njema kuwa hatimaye mazungumzo haya yamefikia mwisho na wamekubaliana mambo matatu ya msingi.
  2. Itaundwa kampuni mpya kuimanage Acacia in Tanzania, hili limekaa vizuri
  3. Tutagawa 50/50 za economic benefits ambapo ndani ya hiyo economic 5-% ya Tanzania itajumuisha zile 16% shares, royalties na taxes zote. Mwanzo tulielezwa tutagawana faida, kumbe sasa sio faida tena bali imekuwa ni Economic benefits. Aliyetutangazia tutagawa faida ni rais wetu na Waziri wetu Kabudi, alifafanua vizuri. Kwa vile haya sasa ndio makubaliano ya mwisho, hii maana yake ni ama rais wetu pale mwanzo alipotoshwa, na waziri alipotosha, ukweli wenyewe sasa ndio huu, ama tangu mwanzo ilikuwa ni economic benefits tatizo ni lugha za watu. Hili mimi nililiuizia rasmi humu Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la kugawana 50/50 ya faida ni kweli au ni changa la macho tu?. - JamiiForums
  4. Watatulipa dola milioni 300 to resolve outstanding tax claims. Deni tunalowadai ni do;a bilioni 190, Ile dola milioni 300 ya goodwill iliahidiwa kuonyesha nia njema, lakini sasa ndio pekee inatajwa kama settlement deal!. Hapa kuna changa la macho!, tusubiri hiyo settlement deal yenyewe maana hizi lugha za watu ni shida.
  5. Kule mwisho anaposema makubaliano yoyote lazima yaridhiwe na Acacia, who is this Acacia kama mmiliki wa Acacia ni Barrick na mazungumzo hayo sio tuu ni serikali ya Tanzania na Barrick, nali ni makubaliano ya rais wa Tanzania na rais wa Barrick, baada ya kukubaliana then kuna mtu mkubwa zaidi yao ndiye ataamua kutekeleza au laa!. hii haijakaa vizuri na niliizungumzia hapa Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye uamuzi wa mwisho ni Acacia!, Kwanini hakushirikishwa?!. Je, Tutalipwa?. - JamiiForums
  6. Tukija kwenye taarifa ya Acacia, kiukweli kabisa haijakaa vizuri na hii sii dalili nzuri, wewe kama mwana jf, be the first to know from me, kuwa mapendekezo yoyote ya settlement kati ya Barrick na Tanzania, hata yakifikishwa kwenye Bodi ya Acacia, yatakataliwa!, Kitakachofuata ni baba Barrick ndiye atalipa fedha hizo, Kisha atamwadhibu mtoto jeuri huyu kwa kuivunjilia mbali Acacia na kuunda Kampuni mpya yenye bodi yenye Watanzania.
  7. Sababu za kusema hivi ni huyu Acacia ni mtoto tuu, baba ni Barrick, haiwezekani baba azungumze, na kutuma ujumbe kuja kuzungumza na rais wetu na atoe ahadi kwa rais, kisha atoe press release kuwa mtoto ataarifiwa halafu wewe mtoto, licha ya kusoma Press Release ya baba, halafu wewe mtoto unatoa press release kumkana baba yako kuwa bado hujaarifiwa!. huu ni ujeuri wa aina gani au hiki ni kiburi cha aina gani?, kiafrika hapa mtoto unaweza hata kupata laana, lakini mambo haya kwa wenzetu wazungu tena jeuri hii ya mtoto huyu haikuanza leo na hapa niliwahi kuizungumza Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto Anatakiwa Kunyamaza. Bora Wafungashe Tuu, Waondoke? - JamiiForums
  8. Nikija kwenye taarifa ya Ikulu taarifa ya Ikulu, inaonyesha sasa the settlement ni ile dola milioni 300 tuu, ambacho sasa kinaitwa kifuta machozi ya zile dola bilioni 190!. Niliwahi kutoa angalizo humu kuwa rais Mkapa alidanganywa akadanganyika, JK pia akadanganywa akadanganyika, nikasema naziona dalili za rais Magufuli kutaka kudangaywa, kama tume settle dola bilioni 190 kwa dola milioni 300, tuelimishwe labda tutaelewa. Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika? - JamiiForums
  9. Pia taarifa ya Ikulu imethibitisha mgawo wa 50/50 ni wa economic benefits, hili linahitaji ufafanuzi wa ziada.
  10. Msingi mkuu wa yote haya ni mgogoro wa makinikia. Tulizuia makontena ya mchanga, kwa sababu tunaibiwa kwa kutokujua, kilichomo, ili tujue tunaibiwa nini, ilibidi ule mchanga uchenjuliwe ndipo tupigiane hesabu za kweli. Sijasikia tena kuhusu ununuzi wa kichenjulio, kiukweli mchanga ukiondoka bila sisi kujua kilichomo, kiukweli sitashangaa bali nitaamini sisi Watanzania .... naomba nisimalizie
Hitimisho.
Watanzania wote wazalendo wa kweli wa taifa hili, tumuunge mkono rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli katika vita vya kulibda rasilimali zetu ndidi ya mabeberu, na kama una jicho la tatu la kuangazia visivyoonekana na wenye macho mawili tuu, then share what you see which others dont see so that we can all see, kwenye hili, there is something fishy.

Nawatakia Jumatano njema
Paskali

Rejea kuhusu makinikia

Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa Kishika Uchumba Cha Dola Milioni 300 - JamiiForums

Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa Kishika Uchumba Cha Dola Milioni 300

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi? - JamiiForums"]

Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter, Jee Tununue Au Tuzitumie Kwa Mahitaji Muhimu Zaidi? - JamiiForums

Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa? - JamiiForums

Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie Kwenye Madini Tuu na Gesi Jee?!. - JamiiForums

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike! - JamiiForums

Wataalamu Hawa Wachunguzwe!,Jee Kuna Posibility Walihongwa Kutoa Ripoti Kuwa "Tanzania Hatuwezi?!". - JamiiForums

A Compromised Possibility: Iweje Ripoti ya Kamati ya 2 iibukie Acacia-London kabla ya kwa Magufuli? - JamiiForums

Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika? - JamiiForums

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!. - JamiiForums

Makinikia: Je, Vyombo Vya Habari Vifukue Makaburi ya Chanzo, Au Kushangalia Tuu Matokeo?.Jicho Letu. - JamiiForums

Zita Act Retro-Respectively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo?, Can we Stand?, Do we Have The Guts?. - JamiiForums

Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto Anatakiwa Kunyamaza. Bora Wafungashe Tuu, Waondoke? - JamiiForums
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Vita ya kiuchumi ni ngumu sanaaa.....Masikini Lissu namkumbuka sana kwenye hii sakata.alitutahadharisha lakini ujuha ukatupoza. saa hizi yupo anauguza majeraha yake kwa kutaka kuwasaidia wadanganyiaka.pole sana Lissu
 
Pascally unataka kutwambia kuwa ni yale yale ya mkataba wa kuuza korosho tani laki moja kwa wakenya?

Any update plse.
P
 
P
I and all the people know its all bulshit
Time will tell
Time will witness
 
Huyu Barick naye si alikuja kwa ndege binafsi kutoka huko watokako kama alivyo kuja yule jirani wa vile vitu vya buku tano, buku mbili, na buku mwisho, ambavyo tumesikia hivi karibuni vimeanza kupata exhastion ghalani mwake?
 
Mimi katika hii senema bado kuna baadhi ya scene sijazielewa,

1. Sisi tunaowadai ni Barrick au Accacia!?

2. Kama tunawadai Accacia, kwanini tunafanya mazungumzo na Barrick!? Na kama tunawadai Barrick, kwanini tukifanya mazungumzo na Barrick Accacia wanatoa press release against mazungumzo yetu yasiyowahusu!?

3. Leo walikuwa wanazungumza kukubaliana nini wakati tangu 2017 tuliambiwa tulishafikia makubaliano tusubiri kurudishiwa chenji!

Sent using Jamii Forums mobile app
hakuna tunaye mdai ila sisi ndiyo tuta daiwa, ni kama ile kesi ya kina mbowe na akwelin. Tusubiri tu muda huwa haudanganyi
 
Wewe Paskali nakuheshimu sana, lkn ndio mtu anayeongoza kuniudhi. Kuna shida gani kwenye haya maandishi yako ukitu-update status za Noah zetu? Shubamiti zako
Mkuu Mwana Mtoka Pabaya, najua bandiko hili litakuwa lilikupita, soma taarifa ya Ikulu kuhusu deni la Noah zetu niliisha eleza humu
  1. Nikija kwenye taarifa ya Ikulu taarifa ya Ikulu, inaonyesha sasa the settlement ni ile dola milioni 300 tuu, ambacho sasa kinaitwa kifuta machozi ya zile dola bilioni 190!. Niliwahi kutoa angalizo humu kuwa rais Mkapa alidanganywa akadanganyika, JK pia akadanganywa akadanganyika, nikasema naziona dalili za rais Magufuli kutaka kudangaywa, kama tume settle dola bilioni 190 kwa dola milioni 300, hapa kiukweli kabisa, Watanzania tutahitaji tuelimishwe labda tutaelewa na ikiwa jili deni la kodi ni deni fake, lets come clean kwa kuusema ukweli kuwa tuliwazushia tuu, hii maana yake TRA ni wazushi?. Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika? - JamiiForums
P
 
Pascal, niliwahi kukwambia kwamba wazungu ni wajanja, wao watapotezea na wanazunguka ili mradi tu Mh wa nchi amalize muda wake waje kivingine. Alafu kwani wao Accacia mzozo huu unawazuia kuchimba dhahabu Tz au wanaendelea na uchimbaji? After all, kumbuka wakichimba dhahabu mgao watagawana na Barrick.
 
Wanabodi,
Hatimaye huu mtanange wa Acacia kununuliwa na Barrick, hatimaye umefika mwisho jana, kwa Barrick kutoa tangazo la kuinunua Acacia, na Acacia kutoa tango la kukubali kununuliwa na Barrick.

Tangazo la Barrick la Kifo cha Acacia ni Hili
PRESS RELEASES
Recommended Final Offer For Acacia Mining Plc By Barrick Gold Corporation โ€“ July 19, 2019

Tangazo la Acacia kukubali kununuliwa na Barrick ni hili

Hii maana yake ni
  1. Sasa mgogoro wa Acacia na serikali yetu, umemalizika rasmi kwa sababu sasa Acacia doesnt exist anymore.
  2. Migodi yote mitatu iliyokuwa chini ya Acacia, sasa itakuwa chini ya Barrick
  3. Yale makubaliano ya serikali yetu sasa yatatekelezwa.
  4. Kwa kuanzia tutalipwa dola milioni 300 zilizokuwa ni kishika uchumba, lakini sasa sio kishika uchumba tena bali ni kifuta machozi cha kusamehe lile deni kubwa la kodi la dola bilioni 190.
  5. Barrick ataunda kampuni mpya ya ubia na Tanzania kuchukuwa shughuli za Acacia
  6. Kwenye hiyo kampuni mpya, serikali ya Tanzania itakuwa na shares asilimia 16%.
  7. Bodi ya hiyo kampuni mpya itakuwa na Watanzania.
  8. Makao Makuu yatakuwa Tanzania
  9. Menejiment itakuwa na Watanzania.
  10. Tutagawana manufaa ya kiuchumi pasu kwa pasu, yaani 50/50.(NB.Manufaa ya kiuchumi ni economic benefits na sio faida profits)
Huu ndio utakuwa ushindi wa kwanza wa kishindo wa rais Magufuli na awamu ya Tano kwa kuanza rasmi utekelezaji wa kwanza wa sheria mpya ya madini.
Hongera Kabudi, Hongera Magufuli, Hongera Watanzania, ila kwenye makinikia, bado kuna lakini!.
Leo tupongezane kwanza, lakini tuzijadili baada ya kusainiwa makubaliano yenyewe!.

Hureeee,
Hongera sana team coach JPM,
Hongera sana dealy striker Prof. Palamagamba Idan Kabudi
Hongera kwa Watanzania. Huu ni ushindi wa JPM, huu ni ushindi wa kamati yote ya majadiliano, huu ni ushindi wa Watanzania woteeee
 
Lissu alipoiita ile ni "professorial rubbish" mlimpinga sana.

Sasa endeleeni kujitekenya wenyewe kisha mcheke.

Hekaya zenu hazituhusu mpaka pale tutakapo pata Uhuru wetu kutoka kwa huyu mkoloni mweusi anayejipachika joho la uzalendo "hewa".
Yukowapi Lissu?
 
Pia ni tatizo la serikali kudanganya uma! Barrick wenyewe wanasema watapeleka mapendekezo yote kwenye bodi ya ACACIA kwa ajili ya approval lakini serikali inasema BARRICK wamekubali kila kitu walichojadili wakati approval bado kutoka ACACIA

Mwisho wa siku usishangae migodi ikifunguliwa bila mirejesho ya nini walikubaliana
Njoo tuzungumze tena kuhusu hili suala maana kipindi hicho ulikuwa na mihemko sana
Swali langu; iko wapi Acacia?
 
Back
Top Bottom