ACACIA INAWAHUSU HII?

Mlanga

JF-Expert Member
Jun 7, 2014
1,023
467
UWEZEKANO WA KUYASHITAKI MAKAMPUNI YA MADINI KUREJESHA HASARA TULIYOIPATA HUU HAPA.

Na Bashir Yakub. +255784482959

Mikataba yoote ya kimataifa huongozwa na wajibu wa aina mbili. Wajibu ulioandikwa(express obligation) na wajibu ambao haukuandikwa(implied obligation).

Wajibu ulioandikwa ni masharti yote ya mkataba yaliyo katika maandishi ambayo wahusika husoma na kuridhia, wakati wajibu usioandikwa ni masharti ya mkataba ambayo hayakuandikwa katika mkataba lakini yapo kwa asili au yapo kwakuwa tayari yalishasemwa na sheria na hivyo si lazima kuyaandika ktk mkataba.

Mathalan, mfanyakazi wako wa duka hawezi kukuibia halafu akasema kwenye mkataba wangu wa ajira hakuna sharti la uaminifu. Laa hasha uaminifu ni sharti la asili "implied obligation" kwa hiyo liandikwe au lisiandikwe bado lipo tu.

Kwenye mikataba ya kimataifa kama ile ya kwetu na makampuni ya madini masharti yafuatayo ni ya asili na hayahitaji kuwa yameandikwa ili kuyatekeleza :
1. Wajibu wa kuanika taarifa zote muhimu kuhusu shughuli inayotekelezwa katika mkataba( Implied covenant to disclose all necessary information over the subject matter).

2. Wajibu wa kutekeleza na kutenda kwa nia njema(Implied covenant to act in good faith and fair dealing).

3. Wajibu wa kila mhusika katika mkataba kuwa mkweli . Hili huwa ni katazo la udanganyifu(Fraud).

Haya yawe yameandikwa kwenye mkataba au hayakuandikwa yakikiukwa tafsiri yake ni kukiuka masharti ya mkataba.

Matendo kama kulaghai kuhusu uzito wa madini yanayochukuliwa, kulaghai kuwa unachukua dhahabu huku ukijua unachukua zaidi ya dhahabu, kulaghai kuhusu bei , kutotoa taarifa sahihi za kipi unapata na kipi hupati,nk ni kukiuka wajibu na masharti ya mkataba jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Na ikiwa wamekiuka mkataba kwa misingi hiyo basi Tanzania inaweza kufanya yafuatayo;

1. Kuendelea na mkataba lakini kwa sharti la kurudisha kile chote kilichopotea kwa mda wote( specific performance).

2. Kutoendelea na mkataba na kudai fidia, hasara tuliyopata,pamoja na riba zake kwa kipindi chote(
breach of contract).

Ndugu zangu, wajibu wa kutekeleza na kutenda kwa nia njema (implied covenant to act in good faith and fair dealing), kuwa mwaminifu na kutoa taarifa sahihi katika utekelezaji mikataba ni matakwa ya lazima duniani kote.

Sheria ya biashara ya Amerika Uniform Commercial Code vifungu vya 1 - 12 habari hii imeelezwa kwa upana.

Sheria ya biashara ya Ufaransa na Ujerumani The German Civil Code(BGB) na Civil Code of France zimeeleza vitu hivi.

Pia mahakama kuu ya Uingereza katika kesi ya Yam Seng PTE vs International Trade Co. Ltd (2013) EWHC 111 ( QB) iliamua kuwa masuala ya uaminifu na kutoa taarifa sahihi katika kutekeleza mikataba ni wajibu ambao upo hata Kama haukuandikwa kwenye mkataba.

Halikadhalika sheria yetu ya Mikataba, Sura ya 345 vifungu vya 18 na 13 vimeyafanya masuala ya udanganyifu na kutoa taarifa zisizo sahihi kama mambo ambayo ni makosa na yanayobatilisha mkataba.

Kamati ya Profesa Mruma imebaini upotevu wa Bilioni 829.4 x Miezi 12 kwa miaka 18 = Trilioni 829.4. Hizi ni pesa nyingi mno. Tunayo kesi nzuri ya madai na uhakika wa kurejesha fedha tulizopoteza. Ni vema mda huu pamoja na mambo mengine, nguvu nyingi ikatumika kuona ni namna gani tunapata hii fedha. Makosa yapo na yametendwa na hilo halina Shaka. Iko wapi haja kukhofu, hakika haipo.

Yumkini haitakuwa rahisi kutokana na aina ya mabepari ambao tunashughulika nao. Ni mabepari hatari wenye mtandao mkubwa wa kisiasa na nchi wafadhili pamoja na taasisi kubwa kama IMF, WB, UN nk.

Hata hivyo tumeshasema hii ni vita na vita sharti ipiganwe ili waliosiginwa wawe huru. Tunaweza kuumia kwa mda ila mwisho wa maumivu hayo itakuwa ni neema kubwa na ya milele.

Mungu ibariki Tanzania na mbariki rais kwa pamoja tushinde vita hii.
 
Bado tunakazi kubwa ili kila mtu aweze kujua sheria na kuweza kuzitetea katika kulinda rasilimali zetu.
 
UMESEMA UKWELI WOTE NA UKO MAKINI SANA: KINA LISSU KAZI YAO KUTISHA WATU BADALA YA KUTOA USHAURI MZURI KAMA HUU
 
UWEZEKANO WA KUYASHITAKI MAKAMPUNI YA MADINI .
Mkuu tambua ya kwamba kama mtu atakiuka masharti ya mkataba kuna namna ya kumshtaki au kuvunja mkataba. mkataba ukishafungwa unabaki kuwa mkataba wala huwezi dai chochote kilicho nje ya mkataba. Hautadai fidia ya mali iliyopotea kisa tu uliyefunga nae mkataba alichukua zaidi ya alichotakiwa kuchukua katika mkataba. sana sana kama kachukua zaidi ya mkataba basi mkataba utakuwa umevunjika na huwezi ku inforce specific perfomance kama unavyodai.
Fidia utadai tu pale uliyefunga nae mkataba atakiuka masharti ya mkataba na fidia yenyewe iwe katika mipaka ya mkataba wenyewe.
Msimtupie madongo tu lissu, ni mwanasheria na anauhakika na anachosema
 
Vipi kuhusu hizo
'implied obligations' unasemaje, ni applicable kwa kesi hii?
 
mkatana wowote una implied obligations. hata hivyo implied obligation yoyote iwayo haiwezi kupindukia na kuwa penal, au kwa maana nyingine kama hakuna express obligation inayoainisha makosa flani haitawezekana mfunga mkataba akabambikwa kosa lililo nje yea mkataba. Implied obligations zinatoa general obligations za mikataba, ambazo sanasana ni kanuni tu za kuendesha mkataba huo
 
UWEZEKANO WA KUYASHITAKI MAKAMPUNI YA MADINI KUREJESHA HASARA TULIYOIPATA HUU HAPA.

Na Bashir Yakub. +255784482959

Mikataba yoote ya kimataifa huongozwa na wajibu wa aina mbili. Wajibu ulioandikwa(express obligation) na wajibu ambao haukuandikwa(implied obligation).

Wajibu ulioandikwa ni masharti yote ya mkataba yaliyo katika maandishi ambayo wahusika husoma na kuridhia, wakati wajibu usioandikwa ni masharti ya mkataba ambayo hayakuandikwa katika mkataba lakini yapo kwa asili au yapo kwakuwa tayari yalishasemwa na sheria na hivyo si lazima kuyaandika ktk mkataba.

Mathalan, mfanyakazi wako wa duka hawezi kukuibia halafu akasema kwenye mkataba wangu wa ajira hakuna sharti la uaminifu. Laa hasha uaminifu ni sharti la asili "implied obligation" kwa hiyo liandikwe au lisiandikwe bado lipo tu.

Kwenye mikataba ya kimataifa kama ile ya kwetu na makampuni ya madini masharti yafuatayo ni ya asili na hayahitaji kuwa yameandikwa ili kuyatekeleza :
1. Wajibu wa kuanika taarifa zote muhimu kuhusu shughuli inayotekelezwa katika mkataba( Implied covenant to disclose all necessary information over the subject matter).

2. Wajibu wa kutekeleza na kutenda kwa nia njema(Implied covenant to act in good faith and fair dealing).

3. Wajibu wa kila mhusika katika mkataba kuwa mkweli . Hili huwa ni katazo la udanganyifu(Fraud).

Haya yawe yameandikwa kwenye mkataba au hayakuandikwa yakikiukwa tafsiri yake ni kukiuka masharti ya mkataba.

Matendo kama kulaghai kuhusu uzito wa madini yanayochukuliwa, kulaghai kuwa unachukua dhahabu huku ukijua unachukua zaidi ya dhahabu, kulaghai kuhusu bei , kutotoa taarifa sahihi za kipi unapata na kipi hupati,nk ni kukiuka wajibu na masharti ya mkataba jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Na ikiwa wamekiuka mkataba kwa misingi hiyo basi Tanzania inaweza kufanya yafuatayo;

1. Kuendelea na mkataba lakini kwa sharti la kurudisha kile chote kilichopotea kwa mda wote( specific performance).

2. Kutoendelea na mkataba na kudai fidia, hasara tuliyopata,pamoja na riba zake kwa kipindi chote(
breach of contract).

Ndugu zangu, wajibu wa kutekeleza na kutenda kwa nia njema (implied covenant to act in good faith and fair dealing), kuwa mwaminifu na kutoa taarifa sahihi katika utekelezaji mikataba ni matakwa ya lazima duniani kote.

Sheria ya biashara ya Amerika Uniform Commercial Code vifungu vya 1 - 12 habari hii imeelezwa kwa upana.

Sheria ya biashara ya Ufaransa na Ujerumani The German Civil Code(BGB) na Civil Code of France zimeeleza vitu hivi.

Pia mahakama kuu ya Uingereza katika kesi ya Yam Seng PTE vs International Trade Co. Ltd (2013) EWHC 111 ( QB) iliamua kuwa masuala ya uaminifu na kutoa taarifa sahihi katika kutekeleza mikataba ni wajibu ambao upo hata Kama haukuandikwa kwenye mkataba.

Halikadhalika sheria yetu ya Mikataba, Sura ya 345 vifungu vya 18 na 13 vimeyafanya masuala ya udanganyifu na kutoa taarifa zisizo sahihi kama mambo ambayo ni makosa na yanayobatilisha mkataba.

Kamati ya Profesa Mruma imebaini upotevu wa Bilioni 829.4 x Miezi 12 kwa miaka 18 = Trilioni 829.4. Hizi ni pesa nyingi mno. Tunayo kesi nzuri ya madai na uhakika wa kurejesha fedha tulizopoteza. Ni vema mda huu pamoja na mambo mengine, nguvu nyingi ikatumika kuona ni namna gani tunapata hii fedha. Makosa yapo na yametendwa na hilo halina Shaka. Iko wapi haja kukhofu, hakika haipo.

Yumkini haitakuwa rahisi kutokana na aina ya mabepari ambao tunashughulika nao. Ni mabepari hatari wenye mtandao mkubwa wa kisiasa na nchi wafadhili pamoja na taasisi kubwa kama IMF, WB, UN nk.

Hata hivyo tumeshasema hii ni vita na vita sharti ipiganwe ili waliosiginwa wawe huru. Tunaweza kuumia kwa mda ila mwisho wa maumivu hayo itakuwa ni neema kubwa na ya milele.

Mungu ibariki Tanzania na mbariki rais kwa pamoja tushinde vita hii.

NA WEWE MUNGU AKUBARIKI NA KUKUPA MAISHA MAREFU KWA KUMUUNGA MKONO RAIS WETU NA WATANZANA KWA UJUMLA ACHANA NA MLAANIWA TUNDU LISU ASIYEITAKIA MEMA TANZANA KWA KUWA UPANDE WA ADUI ZETU ALANIWE KOKOTE ALIKO IWE MCHA AU USIKU
 
Ahsante Bashiru Yakubu, pia hii makala inazunguka katika makundi ya wasapu, Mbunge wa Mtwara akisema ameandika yeye, ila nilipata wasiwasi
 
Back
Top Bottom