ACACIA: Hatujafikia makubaliano yoyote ya kuilipa Tanzania

Sisi tumeongea na Mfuga Mbwa basi.
Report ilisema hawa watu ni wezi?
c91f1b172084ab5dc64eb9953ee73f64.jpg
 
Mimi nilifikiri wanaipeleka Tanzania mahakamani kama mwanasheria wenu nguli alivyokuwa akidai. Sijui MIGA na takataka zingine. Nashangaa wanasema watajadiliana na serikali. Hawa wanasheria wasio na nidhamu na wanaoongea kwa kukurupuka wanapaswa wabadilike. Sasa watapolipa hela wanayodaiwa na Tanzania sijui mwanasheria wenu mropokaji atawaeleza nini Watanzania. Kukariri nako ni kubaya sana
Mkuu mbona una haraka we ngoja cku magu awaambie anataka trilion 100 zake ndio utoke povu??? Maadam mazungumzo bado tutulie tu muhim haki itendeke ila sioni wapi lisu kapotosha zaidi alitoa rai ambayo kwa ssa haina maan kwako ila kufikia cku ya mazungumzo ndio mtakuja niambia kma hamtomkumbuka

Time will tell
 
Anasema@Rutashubanyuma

Mikutano karibu yote ya chadema ina wasifu wa jazba, hoja za nguvu na kufoka kunakopita kiasi na hivyo kuwafanya wafuasi wao kuonyesha nia ya kujichukulia sheria mkononi na haya kama hatutaelezana mapema nionavyo uhuru wa wengineo ambao hawaafiki misimamo ya cdm uko njia panda.....

CDM wanapatwa na taswira hii ya kuuandaa umma kuvunja amani ni kwa sababu zifuatazo:-

1) HAWAJIAMINI/ INSECURE!

Viongozi wengi wa cdm ni makapi ya ccm na hivyo kujiona ni bidhaa choka na hivyo kutafuta mbinu mpya ya kujirudish a ulingoni kama hii ya jazba, hasira, kufoka na kudai hata yale ambayo hawastahili.

2) VISASI/ VENGEANCE.

kawaida ya makapi ni kuwinda mwanya wa malipizi na huo mwanya usipopatikana kwa haraka basi "hasira za mkizi" hutawala kama tunavyoona sasa kwenye mihadhara yao.

3) UTAPELI WA KISIASA/ POLITICAL HYPOCRISY

Unapoona vinara wao bungeni wanakuja na khoja binafsi ambazo zimekithiri kwa kukiri hatua za serikali katika kutatua kero kama ile ya maji ya Dar kwenye khoja ya Mnyika lakini bado wanadai nayo ni khoja binafsi kwa vile mkakati wa serikali umepungua bilioni mia! Basi ujue taifa limeingiliwa na matapeli wa kisiasa ambao kwa raia wasiojua lolote wanafikiri cdm ndiyo mkombozi kumbe khoja tajwa hazina ufumbuzi ila malalamiko yasiyo na kichwa wala miguu........

Mnyika alipaswa kutathmini mkakati wa serikali na kubaini mianya ya wizi na ubadhirifu ambayo ni lukuki na hivyo kutoa ushauri wa kuiziba.............................hilo hakufanya sasa purukshani za cdm kupeleka khoja tajwa kwa wananchi kama siyo ulimbukeni ni nini?

4) USHAWISHI FINYU \ LIMITED PERSUASIVE POWER!

Ukifuatilia manung'uniko mengi ya CDM bungeni yanatokana na madai potofu kuwa wao wako wachache kama vile ukubwa wa pua ndiyo wingi wa makamasi badala ya kujikita katika kuajiri wataalamu wawasaidie katika kujenga khoja zenye mashiko na kubuni mikakati endelevu. Unapoona cdm wanatafuna ruzuku badala ya kuwekeza kwenye utalaamu jiulize ni masilahi ya nani ambayo wanayapigania? Wabunge wote bila ya kujali vyama vyao wanalengo la kuona nchi inasonga mbele na cdm kudhani ni wao tu nao ni kukosa dira ya kisiasa.

Wakati umefika tukawaelimisha cdm kuwa wabunge waachie nafasi ndani ya chama ili wazame kwenye shughuli ya kuibana serikali badala ya utaratibu uliopo wa kujirundikia madaraka ndani ya serikali na ndani ya chama.

pia watendaji ndani ya chama wawe wataalamu badala ya sasa upayukaji kwenye mihadhara sasa ndiyo sifa ya kukwaa madaraka chamani.

5) KUWADHARAU WAPIGAKURA/ UNDERESTIMATING AND ABUSING VOTERS!

CDM ni magwiji wa kutengua sauti ya wapigakura lakini wakifika majukwaani huwahadaa kuwa kuna kitu kiitwacho "people's power"...........huu ni uzandiki usiyo na kifani.

tatizo la uongozi wa CDM ni kuwaona wapigakura ni mbumbumbu na wao ndiyo wajuaji na kwa kufanya hivyo wamewadharau na ni wale tu ambao kweli ni mambumbumbu wataendelea kufuata hilo giza nene ndani ya kivuli cha CDM.

6) KWELI MWAMBA NGOMA HUVUTIA KWAKE/ TWISTED SELF EVALUATION!

CDM kamwe hawako tayari kukemea maovu ndani ya CDM lakini ni magwiji wa kuinyoshea vidole serikali ya CCM! Huu ni unafiki haswa pale ambapo jazba, ukelele, mayowe, ndulu, na kupayuka kwatumika kufukia mashimo ya mapungufu ndani ya CDM na wajanja hawa kujipatia mtaji wa kuonekana wao ni swafi huko wananuka na ufisadi mashabiki wao humezwa na hilo wimbi la kitapeli na hatari yake ni kuwa viashiria vya kukosekana amani vimeanza kushamiri kama sasa tunasikia hata spika Anne Makinda anapigiwa simu na watu wasiojulikana na kutukanwa matusi ya nguoni.

Ni juzijuzi tu CDM kwenye mikutano yao Dar waligawa namba za simu za wabunge wa CCM kwa mashabiki wao bila ya hata ya kuomba kibali cha wabunge tajwa. Unapopewa namba ya simu na mtu ujue hiyo ni dhamana na wala siyo kuitumia dhamana hiyo utakavyo na hata kuhatarisha maisha ya mwenzio ili wewe upate mkate wako wa kisiasa.

Ni vyema polisi wakakamata viongozi wote wa cdm waliokuwa wanagawa namba za simu za wabunge wa ccm kwa wanachama wao na kuwafungulia kesi za kuchochea uvunjikaji wa amani na matumizi mabaya ya dhamana ya simu walizopewa.........Ikiwa na pamoja ya wale wote ambao itabainika namba zao tajwa zilitumika kuwakashifu wabunge wa CCM ambao wanatumia haki yao kidemokrasia kuyatekeleza yale ambayo wanaona yanatija kwa taifa............

7) MAJEMADARI WA LAWAMA LAKINI HAWANA MAJIBU YA KERO/ GRUMBLING WITHOUT ALTERNATIVES!

Ukihudhuira mikutano mingi ya CDM utakuta ni malalamiko dhidi ya serikali ya CCM lakini hata siku moja hawatoi ufumbuzi wa kero husika na kudhani kama wakifanikiwa kuing'oa CCM basi shida zetu nazo zitakuwa zimefikia ukingoni jambo ambalo ni udanganyifu mkubwa. Kenya walikuwa wakidai upinzani "YOTE YAWEZEKANA BILA MOI" lakini miaka 10 tangu Moi atoke madarakani tunaona ulikuwa ni utapeli wa kimataifa kabisa!!! ........................tatizo siyo mtu bali mfumo wa kuendesha nchi...........................acheni CDM kutupotosha juu ya hili.

8)............nitaendelea wakati mwingine...............
 
Mimi nilifikiri wanaipeleka Tanzania mahakamani kama mwanasheria wenu nguli alivyokuwa akidai. Sijui MIGA na takataka zingine. Nashangaa wanasema watajadiliana na serikali. Hawa wanasheria wasio na nidhamu na wanaoongea kwa kukurupuka wanapaswa wabadilike. Sasa watapolipa hela wanayodaiwa na Tanzania sijui mwanasheria wenu mropokaji atawaeleza nini Watanzania. Kukariri nako ni kubaya sana
Ni hatua nzuri ila kumbuka katika issue za hivi kwanza yaanza majadiriano ukionekana upande wowote unaleta zaidi utata hautaki kuridhia ndipo hatua zingine zinafuata. Nashauri serikali iwanoe wanasheria wake wakae mkao wa kula maana tusibweteke kwa kuambiwa wamekubari kufanya discussion then tukaconclude ndio wamekubali hapana tukae vizuri katika hili wao wasingeweza kwenda mahakani wakati raisi ameshatoa nafasi ya kukaa nao na kujadiri hili. Mimi naanza kuandaa parking yangu ya noah
 
Leo nimeangalia taarifa za habari chanelvtatu nimeona maajabu. Kuna utofauti katika chanel hizi zote ila angalau chanel ten walijitahidi waliweka alipoongea rais alafu wakaweka alichokiongea yule wa barick pia ni tofauti na nilichokisoma kilichosambazwa mitandaoni au mimi kiingereza sikijui? Sijamsikia yule wa bariki kusema wamekubali kuripa hicho kilichotajwa katika tume ila kwa raisi nilisikia akisema wamekubali kuripa na mitandaoni pia, ebu msinichanganye naombeni audio au video ya huyu wa barick akikiri kukubali kuripa hizo hela ili niandae parking kabisa ya noah yangu
Sizonje hajui kiingereza, hakuna cha Noah Wala vitz mkuu, endelea na Mambo Yako!
 
Hii vita imekosa maana baada ya kugeuzwa kuwa vita ya CCM vs chadema badala ya vita ya kiuchumi, wengine wanatamani magufuli ashinde wengine wanatamani ashindwe. Wasome kwa comments zao utawaelewa. Sio siri mnaboa.
 
Tatizo ni uelewa wa kiingereza na matarajio makubwa. Mzungu kasema tutafanya mazungumzo yenye lengo la win-win situation. Sisi tunasema wamekubali kulipa. Malipo yatategemea matokeo ya mazungumzo. Angalizo hawa waxungu ni wazuri sana wa negotiations. Tusipokuwa makini tutapigwa kiulaini sana mezani
 
Mbona mnaita watu WEZI halafu kesho yake mkishiba "ugali na mnafu" mnaita watu haohao kuwa ni WANAUME?? Ina maana issue ya makinikia ndo imekufa rasmi? Ina maana hoja ya kampuni kutosajiliwa imekufa? Ina maana mikataba na sheria hazitapitiwa tena kama mlivyoahidi? Kwahiyo tukubali kuendelea na mikataba ya hovyo ya kupewa 4% na mwekezaji aendelee kuchukua 96%, kisa tu kuna "MWANAUME" amekuja leo?? Sidhani kama hii ni sahihi.

Hivi shida yetu ilikua huyo MWANAUME kuja au ilikua mikataba mibovu, na sheria mbovu kupelekwa bungeni kupitiwa upya? Hivi kuja kwa huyo aliyeitwa MWANAUME kunaondoa ukweli kwamba kampuni yake haijasajiliwa nchini?

Mbona mnajichanganya? Mlisema kampuni yake haijasajiliwa, then amekuja mnamuita MWANAUME. Mwanaume ambaye ameshindwa hata kusajili kampuni, huyo ni mwanaume kweli au dume suruali??

Halafu mmekaaje kwenye mazungumzo na mtu ambaye kampuni yake haitambuliki kisheria? Na aliposema atawalipa, mmekumbuka kumuuliza atawalipaje wakati kampuni yake haijasajiliwa? Ili kampuni ilipe kodi lazima iwe imesajiliwa. Sasa yeye atalipaje wakati mlituambia kampuni yake haijasajiliwa? Au mlikua mnatupiga fix??

Halafu JK alipocompromise na "wezi" wa EPA akawaambia warudishe pesa mlimuita dhaifu. Sasa mbona nyie leo mnacompromise na "wezi" wakubwa kuliko wa EPA, halafu mnawasifia kwa kuwaita WANAUME? And by the way kama mliowaita "wezi" wamegeuka kuwa wanaume, raia wanaoibiwa ni kina nani? Mbona mna matusi ya rejareja kwa raia wenu?

Naanza kuelewa kwanini "watangulizi wawili" wameambiwa wasiguswe. Hakuna dhamira ya kweli ya kupambana na jambo hili. Tutaendelea kuibiwa kwa sheria zilezile mbovu, kwa mikataba ileile ya kinyonyaji, kwa kampuni zilezile zisizosajiliwa halafu tukiulizwa tutasema "atakuja mwanaume kulipa". Kama ujinga ni kipaji, basi ccm wana kipaji maalumu.!!

Malisa GJ
 
Barua imeandikwa na Acacia, mazungumzo yalikuwa kati ya rais na Barrick. Kwanini watu hawasomi?
 
Lakni si mazungumzo yameanza, na siyo wenu alivyokuwa anadanganya watu tutashitakiwa mbona hatujashitakiwa na makontena bado tumeyashikilia?

Kushitakiwa ni endapo mngejidai kuvunja mkataba kienyeji. Halafu kuhusu malipo, msijeshangaa kukuta mnaishia kulipwa "mlio wa fedha" na bwana Abunuwas bin Barrick ibn Acacia.
 
Mbona mnaita watu WEZI halafu kesho yake mkishiba "ugali na mnafu" mnaita watu haohao kuwa ni WANAUME?? Ina maana issue ya makinikia ndo imekufa rasmi? Ina maana hoja ya kampuni kutosajiliwa imekufa? Ina maana mikataba na sheria hazitapitiwa tena kama mlivyoahidi? Kwahiyo tukubali kuendelea na mikataba ya hovyo ya kupewa 4% na mwekezaji aendelee kuchukua 96%, kisa tu kuna "MWANAUME" amekuja leo?? Sidhani kama hii ni sahihi.

Hivi shida yetu ilikua huyo MWANAUME kuja au ilikua mikataba mibovu, na sheria mbovu kupelekwa bungeni kupitiwa upya? Hivi kuja kwa huyo aliyeitwa MWANAUME kunaondoa ukweli kwamba kampuni yake haijasajiliwa nchini?

Mbona mnajichanganya? Mlisema kampuni yake haijasajiliwa, then amekuja mnamuita MWANAUME. Mwanaume ambaye ameshindwa hata kusajili kampuni, huyo ni mwanaume kweli au dume suruali??

Halafu mmekaaje kwenye mazungumzo na mtu ambaye kampuni yake haitambuliki kisheria? Na aliposema atawalipa, mmekumbuka kumuuliza atawalipaje wakati kampuni yake haijasajiliwa? Ili kampuni ilipe kodi lazima iwe imesajiliwa. Sasa yeye atalipaje wakati mlituambia kampuni yake haijasajiliwa? Au mlikua mnatupiga fix??

Halafu JK alipocompromise na "wezi" wa EPA akawaambia warudishe pesa mlimuita dhaifu. Sasa mbona nyie leo mnacompromise na "wezi" wakubwa kuliko wa EPA, halafu mnawasifia kwa kuwaita WANAUME? And by the way kama mliowaita "wezi" wamegeuka kuwa wanaume, raia wanaoibiwa ni kina nani? Mbona mna matusi ya rejareja kwa raia wenu?

Naanza kuelewa kwanini "watangulizi wawili" wameambiwa wasiguswe. Hakuna dhamira ya kweli ya kupambana na jambo hili. Tutaendelea kuibiwa kwa sheria zilezile mbovu, kwa mikataba ileile ya kinyonyaji, kwa kampuni zilezile zisizosajiliwa halafu tukiulizwa tutasema "atakuja mwanaume kulipa". Kama ujinga ni kipaji, basi ccm wana kipaji maalumu.!!

Malisa GJ

Huyo Malisa si ndio alikuwa anampigia debe Dr Kafumu? Kila kitu yeye mjuaji.
 
Hivi kwa nini watanzania tunataka kugeuzana mazuzu , ile taarifa ya Msigwa ilisemaje?
Na hapa mbona naona kitu tofauti?
 
Back
Top Bottom