ACACIA: Hatujafikia makubaliano yoyote ya kuilipa Tanzania

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
IMG_20170614_193830_623.JPG
haya sasa,Barrick wamekanusha kufikia makubaliano ya kuilipa Tanzania japo wameongea na Rais
 
Makubaliano waliyofikia ni kuwa na mazungumzo na Serikali na "kama" kuna fedha itathibitika hazijalipwa kama kodi ama hazijatolewa kama mrabaha basi zitalipwa. Hakuna mahali pamesemwa hata na taarifa ile ya Ikulu kwamba watalipa zile fedha zote zilizotajwa kwenye taarifa ya zile tume mbili za Rais.
 
Tatizo watanzania tunapenda umbea,chokochoko na Majungu! Wengine walikuwa happy kama Tanzania Tungeshtakiwa,na kutakiwa lipa Acacia.Wewe ,Mimi na ata aleandika hiyo note hapo juu toka Acacia atukuwepo Ikulu wakt hayo yanaongelewa sote tumeadithiwa tu! Tuache ushabiki maandazi acheni Serikali yetu ifanye kazi.
 
View attachment 523919 haya sasa,Barrick wamekanusha kufikia makubaliano ya kuilipa Tanzania japo wameongea na Rais

Hata ukiwasikiliza kwenye mazungumzo yao , wanaongelea swala la kujadiliana. Hii maana yake ni lazima:
1. Wajiridhishe na hizo ripoti kama ni za kweli au la
2. Wakokotoe nao hesabu zao ili kufikia muafaka
3. Wajadili the way foward baada ya majibu ya hapo juu.

Ngoma hii bado mbichi sana. Magufuli awe mpole tu . Na kama walidanganya hiyo ripoti kwa namna yoyote ile, wajiandae kuomba msamaha mchana kweupe.

Lissu bado ana hoja.
 
Back
Top Bottom