Mkuu CPU mlikuwa mnahadithiana haya wapi? tehetehetehetehe ila nimeona tu kwa kusoma huyo mume ana wivu sana hadi inapelekea kutokujiamini kabisa,inaonekana huyo bibie ni mrembo wa haja. Mke anatakiwa amwelewe huyo mumewe vizuri ili kuepusha mambo kma hayo, akitoka mwenyewe avae nguo ndefu akiwa nae avae hizo fupi. Mh ndoa hizi zina vijimambo haswaHii topic ina mambo mengi sana my dia
Yaani ni kama umekusanya mafaili ya ofisi tatu za Mamlaka za Kodi nchi za USA, China na Brazil halafu umeweka ktk kajidude kamoja kadogo (flash)
Kwanza naomba nikurekebishe kwamba Sexual Abuse tunatafsiri kwa kiswahili kama Unyanyasaji wa Kijinsia
Naomba sasa nielezee kisa kimoja cha Unyanyasaji wa Kijinsia.
Kuna mdada ana mtoto mmja ameolewa, ana miaka minne katika ndoa yake, alizaliwa miaka 24 iliyopita.
Yeye na mume wake walikua wana pendana sana na mpaka sasa mdada anasema bado anampenda tena sana mume wake.
Ananiambia, " Yaani CPU, siku hizi mume wangu kabadilika sana kiasi najuta hata kuolewa yaani kidogo kanitukana mara mshenzi mara mjinga mara ananitisha kunipiga kwa kusema mimi simjui vizuri ndio maana nashindwa kufanya atakavyo.
Ukweli ninachanganyikiwa mume wangu anakuwa kigeugeu anaweza akakwambia "mimi sipendi uvae nguo ndefu", ukivaa fupi kwa muda huo aliosema anafurahi sasa itokee siku nyingine akuambie tutoke ukivaa hiyo nguo fupi anaanza
" . . . . unaenda kumuonyesha nani? Unatakautongozwe kwani mimi sikutoshi? "
Ukivaa ndefu au suruali ananyamaza.
Juzi simu yangu ilijizima nikiwa salon iliyo nje ya uzio wa nyumba tunayo ishi. Akampigia rafiki yake akaja mpaka saloon nikaongea naye kupitia simu ya rafiki yake. Jamani hakutaka kukata simu mpaka muda wa kazi uishe, karudi home hakuna salam ananiambia "utanieleza uliko kuwa" huku anatafuta mkanda aanze shunghuli. Mimi nikamwambia mimi sijatoka hata gengeni sikwenda.
Siku hiyo ndipo alipo mwita mtoto wake mwenye miaka minne nilimkuta naye akamuuliza, ndipo mtoto akamwambia "mama leo hajaenda mahali zaidi ya saloon anako sema" mume wangu akaona aibu akaondoka.
CPU, hata sasa nikimuuliza kwa nini ananifanyia hivyo ananiambia nisimkumbushe anakasirika mpaka nashindwa hata kuendelea kumuuliza. Ni mengi lakini naomba unisaidie "
Ni vitu ambavyo viko sana kwenye jamii yetu
- Verbal abuse (matusi),
- Physical abuse (kimwili),
- Sexual abuse(unyanyasaji wa ki jinsia,)
- (Neglect)kutelekezwa)
- Hate (chuki)
ni vitu ambavyo vinatokea kila saa, tonaona jinsi watoto wetu
wanavyo danganywa na wazee wazima, tunaona jinsi mama zetu
wanavyopigwa na kutukanwa, tunaona jinsi watu wanavyotengwa na jamii
sababu ya vitu wanavyofanya au jinsi walivyo na ambayo ipo kila sekunde
ni sisi kwa sisi kuchukiana .
wandugu ningeomba sana leo tuongelee hizi Dhuluma..
Nini kinampeleka mtu kufanya haya mambo??
Je kila afanyaye haya mambo ni mtu mmbaya??
na ni vipi tunaweza kuwasaidia waliokuwa kwenye hizi
situation
.... You are more than welcome to share anything....
(samahani wakuu ningeomba sana tutumie lugha ya kiswahili na English kidogo)
(ili kila mtu aelewe )
AD
unaweza sema asilimia 75
ya ndoa zina unyanyasaji hasa kwa wanawake......
na athari zake ni mpaka kwa watoto.....
tanzania...
AD,
Hii topic imenigusa sana. Labda kwa vile mimi ni victim kwa namna moja au nyingine wa domestic violence na pia kwa vile mimi nachukia haya mambo. Nadhani haya matatizo yanajitokeza sana kwenye familia zetu kwa sababu watu wanatanguliza ubinafsi zaidi. Iweje mtu amtendee mwenzie yale ambayo asingependa kutendewa?
Kuna jamaa yangu alikuwa mpenzi sana wa vibinti vidogo. Ila watoto wake (girls) walipofikia umri wa puberty alipiga marufuku vijana wa kiume hata ndugu zake wa karibu kuja kukaa kwake!!!
Nitarudi tena baadaye.
Mzee DC.
Upo sahihi ila yanasababishwa na ubinafsi,kukosa elimu,umasikini na magonjwa kama kichaa
Badilika Elia hailipi hata kidogo, unajua tunapofanya haya mambo tujiulize kama sie au watoto wetu wakiishi na watu wengine wakafanyiwa hayo tutajisikiaje? tubadilike na wengine wataigaBaada ya kusoma comments nyingi hapa, najihisi na mimi nina abuse sehemu flani, ngoja nijitizame
Gaga umenena cha maana sanaWamama wengi wanavumilia hii dhuluma sababu ya kipato, maisha magumu na mwanamme anachukua advantage hapohapo na kuanza kumnyanyasa, utakuta mwanamke hajajaliwa kupata watoto anaambiwa unajaza choo, unafikiri hii ni sababu ya nini? hii yote nayo ni dhuluma na unyanyasaji wa hali ya juu
Mtoto hana kosa maskini ni sababu tu mzazi wake mmoja alifariki akaanza kuishi na baba/mama wa kambo hapa wamama ndio mara nyingi wananyanyasa watoto hawa, nafikiri ni ile hali ya kuona kama vile huyu mtoto anashare nae mapenzi ya baba yake. anahisi kama hastahili tena kupata yale mapenzi sababu tu mzazi wake mmoja kafariki.
Ajabu ya yote hii dhuluma, unyanyasaji, unyanyapaaji wote tunafanya sisi sisi wanadamu tunaojiuliza ni kwa nini, sasa basi kwa vile tunafanya sisi ni rahisi kila mmoja wetu ajiangalie, na ajichunguze kama kwa namna moja au nyingine anamnyanyasa mke/mume/mtoto/ndugu yake? tukiweza kubadilika wenyewe na wengine pia wanaweza kubadilika wale wanaotuzunguka na sisi tukawaonyesha mfano bora watoto wetu wanaokua na wao wakiwa watu wazima watafata tuliyowafundisha tangu wadogo
Wengi wetu tukibadilika watabakia wachache mwishowe wataona aibu, ila kwa kiukweli hili tatizo halitaweza potea kabisa ila tunaweza lipunguza kwa kiasi kikubwa sisi wenyeweGaga umenena cha maana sana
Specially your conclusion..
Kwamba sisi tujichunguze na kujibadilisha..
Lakini kuna wale ambao tayari wako Sugu..
Unadhani hao watabadilika kirahisi hivyo???
Umeona eee Manumbu! ndio maana nikasema tunaweza anza generation yetu kulimaliza hili kwa kuwalea watotot wetu na ndugu zetu kwa upendo bila manyanyaso na ubaguzi na watoto wetu kuiga hili kama weweHoja yako ni ndefu sana na kwa mtazamo wangu haiwezi kujibiwa kwa upana wake. nadhani inabidi kuchagua eneo la kujibu kwa sababu hizo abuse ziko tofauti na inawezekana kabisa zinakasabishwa na vitu tofauti na hata namna ya kuzitatua ni tofauti from each other. kwa upande wangu ntachangia kuhusiana na phyisical abuse i.e. kupiga/kupigwa mwili.
ntaanza na mfano wa familia yangu. sie tuko wanane kwa baba na mama. 7 wanaume. tuna dada mmoja. katika maisha yetu, mimi ni wa 6, sijawahi kumwona baba akimpiga mama hata siku moja. mama mwenyewe hulikiri hili kila cku. hali kadhalika, hatujawahi kupigwa na baba hata cku moja. ni kaka yetu mmoja ambaye aliwahi kupigwa na bb na ni kwa vile alimpiga mama! nadhani kwa malezi hayo, hata nasi hatujawahi kuwapiga spouses na watoto wetu hata siku moja! hapa nilipo kuinua mkono wangu kumpiga mtu, hata kama ni mwanaume mwenzangu, ni ngumu sana. nasikia kabisa mkono ni mzito.
nadhani hali ingekuwa tofauti kama tungekua kwenye familia ambayo kupigwa/piga ni hali ya kawaida. so kwa ufupi malezi yanaweza kusababisha abuse, walau za aina hii (physical abuse). Nadhani mchango wangu unatosha kwa sasa
AD Hivi kwa nini umeiweka mada yako kama Tetesi???