Abuja vs Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Abuja vs Dodoma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BondJamesBond, Aug 9, 2012.

 1. B

  BondJamesBond Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nigeria waliamua kuhamisha mji mkuu na serikali nzima ikahamia Abuja bila mgogoro na wameujenga hasa mji wao, sisi Nyerere alikuja na unafiki wa kuhamisha makao makuu to Dodoma miaka hiyo lakini leo kila anayekuja anakikita Dar

  Hivi mnajua kama airport ya Dodoma haina taa usiku?

  Hivi kwa nini waandishi wa habari hawaulizi maswali kama haya? na je kulikuwa na umuhimu gani wa kuanzisha CDA na pesa za walipakodi ambazi zlifujwa bila mahesabu?

  Last but not least hivi kuna mtu anayo masterplan ya mji wa Dodoma?
   
 2. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,048
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  We Bondjamesbond unaishi kwenye sayari ya Mars?
  Sio kweli kwamba Nyerere alikuja na unafiki. Nyerere alikuwa siriaz kabisa na kuamishia makao makuu Dom.
  Suala la kusuasua kwa serikali kuhamia Dom limeandikwa na kuzungumzwa sana katika vyombo vya habari na bungeni. Kwa sasa hivi hiyo nia haipo kwa sababu za msingi japokuwa watawala hawako tayari kutamka wazi.
  Kwa kifupi, nia ya kuhamishia makao makuu ya serikali Dom enzi za JKN ilifungamana na itikadi ya ujamaa (iliyolenga maendeleo vijijini kuliko mijini). Kumbuka itikadi ya ujamaa iliaga dunia na mwasisi wake na hivyo nia ya kuhamia Dom ikatoweka. Zama hizi tumekumbatia itikadi ya 'soko huria' (ubepari) ambayo msisitizo wake ni maendeleo mijini ikiwa ni pamoja na upanuzi wake (urbanization) na kwa mantiki hiyo Dar es Salaam naturally ime-retain hadhi yake ya awali na kuzidi kupanuka kama unavyoiona leo (idadi ya watu, shughuli, vikwanguaanga) japokuwa, kwa bahati mbaya, miundombinu iliyo mingi imebaki kuwa ileile ya enzi za ujamaa - chanzo, kwa mfano, cha msongamano wa magari, mafuriko ya maji machafu na ya mvua wakati wa masika, nk. Kwa hiyo ni suala la kiitikadi za siasa.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,077
  Likes Received: 5,242
  Trophy Points: 280
  Mlitaka Nyerere hadi awafungie mizigo kuhama? Yaani hakuna mtu mwingine yeyote mwenye uwezo wa kufanya lolote isipokuwa "Nyerere mbona hakufanya"? Mlitaka mkue mkute kila kitu kiko tayari nyie mle na kunywa tu msifanye lolote?
   
 4. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,524
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  inapokuja kwa nyerere watanzania tunakuwa kama infants. very dependent!
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,807
  Likes Received: 1,592
  Trophy Points: 280
  Wakuu ni kweli serikali imeonekana kusuasua kuhamia Dodoma kwa sababu mbalimbali lakini hivi karibuni inaonekana kama imezinduka kidogo. Kuna taasisi ambazo zimeanza kujenga makao yao makuu huko dodoma. Huu ni mwanzo mzuri japokuwa nao una shida kwa kuwa taasisi ambazo zina makao makuu dodoma huwa zina maintain ofisi zingine Dar wenyewe huzipa majina kama ofisi ndogo lakini kwa uhakika huwa ni double office.
   
 6. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Acheni matusi. Mleata hoja ana kinyongo dhidi ya Mwalimu Nyerere. Maana anasema eti alifanya kuhamisha makao makuu kwa unafiki. Thibitisha unafiki wa Nyerere isije kuwa unachoona ni unafiki wa Nyerere ni welewa wako mdogo au chuki zisizokuwa na sababu. Nyerere aliacha madaraka miaka mingi iliyopita. Je ndiye amewazuia akina Kikwete kuhamia Dodoma? Ni bahati mbaya kuwa Nyerere aliona mbali akarithiwa na watu wenye kuona karibu na wengine vipofu kabisa. Kila siku mnasikia vifo vitokavyo na ajali vya wabunge hata mawaziri wakikimbia kwenda kutumia Dar weekend kutokana na kutopenda kuhamia Dodoma. Hii pekee ingepaswa iwafungue macho wanaoona kama kuhamia Dodoma hakuna maana. Ni jana tu naibu waziri kapata ajali mbaya akitoka Dodoma kwenda Dar. Jaribuni kutafiti na kufikiri kabla ya kulaumu.
   
 7. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 812
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Mkuu, mi naona Nyerere hakuwa mnafiki kwenye hili. tatizo ni hawa waliomfuata.

  Halafu sera nyingi za ccm utekelezaji wake mi binafsi naona umekuwa 15%-20% wakati kwa mujibu wa rasilimali za taifa letu, walitakiwa hii miaka hamsni ya uhuru wawe japo wamefika 70%-80% hivi. ukiwagusa kina Tyason a.k.a Wassira, Vangimembe Lukuvi na wengine wa dizaini hiyo wanafura kama mbogo aliyejeruhiwa halafu wanakulazimisha uwamini wanachokisema badala ya kukushawishi uamini kwa uhalisia wa vitu ambavyo kweli serikali ya ccm imefanya. hapo ndo mimi huwa wananifanya niangalia uwezekano mwingine. kwa kifupi hawa wameshindwa. mbaya zaidi hawaoneshi dalili za kukubali tu kiungwana kuwa wameshindwa, mbona Nyerere angalau alikiri kushindwa kwa sera ya ujamaa na kujitegemea?????? huo ndo uungwana.

  CCM KUBALINI KUWA MMEJARIBU, LAKINI MMESHINDWA. sio kila anaejaribu huwa anaweza bhana. acheni na wengine waendelee kutoka hapo mlipoishia na nyie muwe wakosoaji, hii nchi si ni yetu wote bhana, tatizo lipo wapi?????????
   
 8. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Jamani sikieni kwa kifupi hatuwezi kuhamia Dodoma kwanza hakuna bahari, tutapata wapi upepo mwanana, hoteli za kifahari, vimwana mwanana. kwanza mpaka leo starehe zenu mwisho saa 6 usiku siku za wikiendi, wakati muda huo Dar ndiyo tunatoka out, serikali haiwezi kulala mapema kiasi hicho.
   
Loading...