Absalom Kibanda: Kilichobaki ni Kuandika kitabu cha Maovu yako Samwel Sitta!

Nimependa ulivyoandika DSN juu ya mada hii ya kibanda,wasiwasi wangu asije akawa ni Salva Rweyemamu wa pili kumbe nyuma ya pazia anatumiwa na akina EL,vinginevyo huyu acha aje na hicho kitabu chake,itajulikana jinsi ya kumjibu na kama hatakuwa na hoja zenye nguvu atakuwa amejimaliza.Naamini wengi hawakupenda jinsi Sitta na kundi lake walivyolikimbia suala la Richmondi tena wakati watz wanasubiri waone mwisho.Salva alichumia tumbo alipotumika kuwachafua waliokuwa wanapambana na kikwete hasa Salim Ahmed Salim anachotaka kukifanya kibanda sidhani kama kinatofauti na mbio za mapema za urais kwa hao mafisadi kuelekea 2015 but all in all let him bring the book.
 
kibanda.jpg

Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima ambaye pia ni mwenyekiti wa jukwaa la Wahariri nchini Bw Absolom Kibanda ametoa matamshi makali dhidi ya Samwel Sitta kwa kumwambia kuwa yeye (Sitta) si mpambanaji kama anavyojifanya lakini kali ya yote amemwambia kwasasa hana muda wa kupoteza kulumbana na Samwel Sitta bali yeye yuko hatua za mwisho kuandaa kitabu kitakachoeleza uovu wa Samwel Sitta ikiwa ni pamoja na kuhusika kwake na UFISADI WA KUTISHA NCHINI wakati akiwa spika wa Bunge la tisa.

Tafadhali kibanda msamehe bure mzee wa watu ,kweli ni fisadi na mnafiki mkubwa na ambaye hajui michezo ya siasa lakini umuache maana roho yake iko nje nje kila wakati ukimwona . Haamini mtu yeyote hata kivuli chake
 
1.namtetea kibanda kwani yeye kama muhariri mtendaji anabeba sifa na lawama za media anayoiongoza, last week sitta amenukuliwa runingani itv akiwahukumu wahari na media houses zao tzdaima ndani kuwa wamenunuliwa na mafisadi, wengine wamemjibu sita kupitia tahariri lakini absalom amethubutu kutenda haki zaidi,amemwambia hatalumbana naye mzee 6 bali atamuweka wazi ktk madhalimu yake kama spika kwa andiko lake yeye, nawashangaa mnaomlaumu kibanda! Kama atapotosha maudhui na ujumbe wa kitabu dhidi ya 6 sheria zipo, historia itajiandika lakini kama 6 atashindwa kuupinga ushahidi basi tz itaamu. 2. Sitta si muumini wa mipaka ya mamlaka kama mnavyotaka tuamini, mnakumbuka ile kesi ya petrol stesheni moro iliyoamriwa na mh. Amir msumi? Sitta aliliingiza bunge ktk malumbano na mahakama,jaji ramadhan-cj alimuwakia 6 mbele ya jk akionya hulka za kurukia mamlaka pili 6 alimtuhumu rais mbele ya bunge na nchi eti si mkali...! 3. Mbona kila anayemgusa 6 anabatizwa ulowasa? Waacheni wtz wapewe taarifa za pande zote ili waamue. Kibanda amekomaa na 6, mnaompinga mje na ushahidi dhidi yake na pia wale mnaoamini ndio hasaa, tutawapima na tutaamua, kuzibana midomo siungi mkono hata kidogo
 
unajua absolom anaumia kama niumizwavyo mimi na hizi tabia za sita na mwakyembe kwanini wanang'ata na kupuliza? Sita kama siyo fisadi kwanini aliamua kuumaliza mjadara wa richmond baada ya kuagizwa na wakuu wake ambao wana link na mafisadi? Naye mwakyembe kwnini aliamua kuamua kutokusema kila kitu kwa kisingizio cha kutunza heshma ya serikali? Alafu leo hii wanaendelea kujidai wanachukizwa na ufisadi, wangekuwa siyo mafisadi na wanachukia ufisadi sita angeruhusu mjadala uendelee mpka kieleweke na mwakyembe angesema kila kitu ili serikali iumbuke kwa maovu yake
hapo umesema ndugu, wote ni wanafiki!
 
Ni kweli kwamba niliandika makala ya kumkosoa Samuel Sitta. Katika sehemu moja nikasema nakusudia kuandika kitabu kuhusu vita ya ufisadi na namna iolivyotekwa nyara na wanasiasa wa ndani ya CCM wa aina ya Sitta kwa maslahi binafsi. Kitabu hicho hakina lengo hata moja la kumlenga Sitta kwa maana ya kumshambulia au kumsifu. Kitabu hicho kinalenga kuwakosa akina Sitta kwa kuiteka hoja ya ufisadi lengo la kwanza likiwa ni kuizima na kuidhibiti Chadema na la pili likiwa ni kujipanga kwa ajili ya urais wa mwaka 2015. Naamini na nitaendelea kuamini kwamba mwelekeo huu wa akina Sitta. Kwa kuwa huu ni uwanja wa hoja, unaposhambuliwa, kukebehiwa na kupondwa unalazimika kuheshimu maoni hata ya wale wanaokuona fedhuli, fisadi, kuwadi na kila aina ya majina mabaya.
 
Nakumbuka ule wimbo wa mmasai "Njaa inauma, chunga usikule nyau......." mwishoni anasema...."Na wewe kula yeye"
 
Kibanda anatumiwa na hili si siri, lakini wacha aje tu, kama anafikiri ati ndo atammaliza Sitta basi ajue atamuweka juu zaidi. Kuhadi wake EL na RA hata wafanyeje havuki huu mto, wakati wa EL umewkisha hii ni historia nyingine kabisa
 
Ni kweli kwamba niliandika makala ya kumkosoa Samuel Sitta. Katika sehemu moja nikasema nakusudia kuandika kitabu kuhusu vita ya ufisadi na namna iolivyotekwa nyara na wanasiasa wa ndani ya CCM wa aina ya Sitta kwa maslahi binafsi. Kitabu hicho hakina lengo hata moja la kumlenga Sitta kwa maana ya kumshambulia au kumsifu. Kitabu hicho kinalenga kuwakosa akina Sitta kwa kuiteka hoja ya ufisadi lengo la kwanza likiwa ni kuizima na kuidhibiti Chadema na la pili likiwa ni kujipanga kwa ajili ya urais wa mwaka 2015. Naamini na nitaendelea kuamini kwamba mwelekeo huu wa akina Sitta. Kwa kuwa huu ni uwanja wa hoja, unaposhambuliwa, kukebehiwa na kupondwa unalazimika kuheshimu maoni hata ya wale wanaokuona fedhuli, fisadi, kuwadi na kila aina ya majina mabaya.

Binafsi katika post hii naona kulitakiwa majibu mawili.
1. Jibu kwa wachangiaji.
2. Jibu kwa thread.
Nikionacho hapa ni kuwa umetujibu wachangiaji (japo tumegawanyika kimitazamo lakini jibu linajitosheleza), ulichoacha na ambacho ndiyo chanzo ni hii thread hujaikosoa na kwa jinsi ilivo ipo very clear kuwa you pointed Sitta to be you business and Logo.
 
Ni kweli kwamba niliandika makala ya kumkosoa Samuel Sitta. Katika sehemu moja nikasema nakusudia kuandika kitabu kuhusu vita ya ufisadi na namna iolivyotekwa nyara na wanasiasa wa ndani ya CCM wa aina ya Sitta kwa maslahi binafsi. Kitabu hicho hakina lengo hata moja la kumlenga Sitta kwa maana ya kumshambulia au kumsifu. Kitabu hicho kinalenga kuwakosa akina Sitta kwa kuiteka hoja ya ufisadi lengo la kwanza likiwa ni kuizima na kuidhibiti Chadema na la pili likiwa ni kujipanga kwa ajili ya urais wa mwaka 2015. Naamini na nitaendelea kuamini kwamba mwelekeo huu wa akina Sitta. Kwa kuwa huu ni uwanja wa hoja, unaposhambuliwa, kukebehiwa na kupondwa unalazimika kuheshimu maoni hata ya wale wanaokuona fedhuli, fisadi, kuwadi na kila aina ya majina mabaya.

Nimekuwa nikifatilia hii topic tangu ilipotumbukia hapa JF jana ila nilishindwa kuchangia kwasababu sikuwa na uhakikaa na mimi imani yangu hainiruhusu kudhani au kusingizia mtu ila kwa vile umekuja mhusika Bw KIBANDA(bilashaka ndiye mtajwa kwenye thread) sasa vizuri naweza kuhoji maswali mawili matatu kama ifuatavyo;
1.Je wewe kwa imani yako na uelewa wako unaamini kuwa Samwel SITTA amefikia ufisadi wa kuandikiwa kitabu?
2.Je kipi bora kuandika kitabu dhidi ya ufisadi nchini Tanzania au kuandika kile unachokijua kuhusu Samwel SITTA?
Naomba kwanza nijibu haya maswali kisha mengine yapo njiani yanakuja!
 
Kuna mtu anajua maisha binafsi ya Kibanda, naomba tuyaweke hapa ili siku kitabu cha SItta kinatoka na cha kumhusu yeye kinazinduliwa. Kuna jamaa kaniambia yeye ufisadi wa Kibanda katika maisha yake ya ndoa. Tuna mahali pa kuanzia, maana ufisadi ni ufisadi tu..................
 
Sijasema mahala popote kwamba ninakusudia kuandika kitabu cha ufisadi wa Sitta. Kwanza sijapata hata mara moja kumhusisha Sitta na ufisadi japo nimesoma makala na habari kadha wa kadha zinazomhusisha na masuala hayo. Mimi napingana na Sitta kuhusu ukamanda wake wa kupambana na ufisadi. Sijapata kuamini hata mara moja kwamba ndani ya kundi la mtandao ambalo Sitta alikuwa mmoja wa vinara wake anaweza akajitokeza mpambanaji wa ufisadi, hiyo ndiyo hoja yangu. Pili kwangu mimi ndani ya CCM ufisadi ni mfumo siyo mtu binafsi kwa hiyo naamini vigogo wote ndani ya chama hicho ni matunda ya ufisadi...hakuna hata mmoja mwenye ubavu wa kumnyoshea mwenzake kidole. Naomba hoja yangu isipotoshwe kwa malengo ya kikundi cha watu fulani...
 
Watu wanapokosa hoja wanakimbilia katika masuala ya kipuuzi kama haya. Eti "ufisadi wa ndoa". Nina msimamo thabiti katika masuala yanayohusu mahusiano. Pengine fisadi kinara wa ndoa ni huyo mnayejaribu kumtetea hapa hata kufikia hatua ya kunisingizia kwamba nataka kumuandikia kitabu. Dhamira yangu safi ndiyo maana ninayo jeuri ya kujitokeza kwa jina langu kamili na halisi na siyo majina ya kidaku kama Ntambaswala. Kwani mtu ukipata msukosuko katika ndoa maana yake ni ufisadi...pengine hakuna ufisadi mbaya kama ule wa kufisidi ukweli katika mambo ya msingi
 
Huyu Abasalomu ni kilaza kuliko maelezo. Naona anafuata mkumbo wa kina Kubenea ili na yeye aingie kwenye payroll ya RA na LA. Kweli hatuna waandishi kabisa ila waganga njaa tu.
Kilaza katika lipi?Kwani sitta kwanini nae asianikwe mauza mauza yake tumjue manake anachonga sana!Kwahiyo wakimwandika sita anavotaka si waganga njaa?Na mimi mkweche nipo kwenye payroll ya nani?
 
Nani kawaambia Sita sio fisadi papa?Je mnajua tabia ya Sita ni hatari zaidi ya ufisadi papa kama mnavyosema kina Lowasa na Rostam ni mafisadi papa?
Hivi yanayotukuta leo watanzania mtayatenganishaje na Sita,kama ni wafuatiliaji wa mambo mtakumbuka mwaka jana jinsi Sita akiwa spika alivyoufunga mjadala wa Richmond ambao ndio unaotutesa hadi leo,Angalieni jinsi Mwakyembe alivyoficha baadhi ya aliyoyapata wakati wa uchunguzi wa sakata la Richmond.
Kibanda huenda anakerwa na unafiki na usaliti wa Sita,sasa tukimlaumu eti kwanini anaandika ya sita anacha mengine tutakuwa tunamlazimisha hisia zake ziwe zetu.tumuache aandike ya sita na wengine kama mnachukia ufisadi andikeni ya wengine.na ni ndoto za mchana kusema Mbowe na SLaa wamenunuliwa na Lowasa ili aje awe president wa TZ.
 
hicho kitabu utasoma mwenyewe na mke wako. Hatutaki wanafiki katika dunia ya SASA tupo tayari kupindua nchi lakini siyo kuwapigia debe mafisadi.Nchi tutaikabidhi iongozwe Kijeshi wakati tunaanda Demokrasia ya Kweli..........................Hata walikuchagua kuwa M/kiti inabidi wajipime vizuri
Copy ya kwanza ntanunua mimi Mkweche!Hakikisha vitabu vinafika Iringa na mie mkweche nikinunue!Ilimradi bei iwe poa 10,000 to 100,000/-
Upo tayari kupindua nchi na mwenzako nani!Unajitekenya halafu unacheka!
 
Sijasema mahala popote kwamba ninakusudia kuandika kitabu cha ufisadi wa Sitta. Kwanza sijapata hata mara moja kumhusisha Sitta na ufisadi japo nimesoma makala na habari kadha wa kadha zinazomhusisha na masuala hayo. Mimi napingana na Sitta kuhusu ukamanda wake wa kupambana na ufisadi. Sijapata kuamini hata mara moja kwamba ndani ya kundi la mtandao ambalo Sitta alikuwa mmoja wa vinara wake anaweza akajitokeza mpambanaji wa ufisadi, hiyo ndiyo hoja yangu. Pili kwangu mimi ndani ya CCM ufisadi ni mfumo siyo mtu binafsi kwa hiyo naamini vigogo wote ndani ya chama hicho ni matunda ya ufisadi...hakuna hata mmoja mwenye ubavu wa kumnyoshea mwenzake kidole. Naomba hoja yangu isipotoshwe kwa malengo ya kikundi cha watu fulani...

Asante Bw Kibanda, naona unajikanyaga hapa! mbona hueleweki mkuu, unaposema kuwa huamini kama hilo kundi la "MTANDAO" ambalo SITTA ni mmoja wao anaweza kutokea mpambanaji wa ufisadi una maana gani? je mtu kama haupingi ufisadi maana yake ana usapport sivyo? kwa maana kwenye vita ya ufisadi hakuna uvuguvugu, sasa kama Sitta hawezi kuwa mpambanaji basi yeye ni kinyume chake UNAKATAA NA HILI? na pili kama sijakosea kwenye makala yako uligusia swala la Sitta kuzima mjadala wa Richmond, sasa na hili la kuzima mjadala wa Richmond unataka kutwambia halina harufu ya Ufisadi? mbona unajikaanga mkuu? naomba unijibu kabla sijahamia kwenye hiyo hoja yako ya kuandika kitabu ambayo ndiyo haswa kiini cha mwanzisha thread.
 
Sijasema mahala popote kwamba ninakusudia kuandika kitabu cha ufisadi wa Sitta. Kwanza sijapata hata mara moja kumhusisha Sitta na ufisadi japo nimesoma makala na habari kadha wa kadha zinazomhusisha na masuala hayo. Mimi napingana na Sitta kuhusu ukamanda wake wa kupambana na ufisadi. Sijapata kuamini hata mara moja kwamba ndani ya kundi la mtandao ambalo Sitta alikuwa mmoja wa vinara wake anaweza akajitokeza mpambanaji wa ufisadi, hiyo ndiyo hoja yangu. Pili kwangu mimi ndani ya CCM ufisadi ni mfumo siyo mtu binafsi kwa hiyo naamini vigogo wote ndani ya chama hicho ni matunda ya ufisadi...hakuna hata mmoja mwenye ubavu wa kumnyoshea mwenzake kidole. Naomba hoja yangu isipotoshwe kwa malengo ya kikundi cha watu fulani...

wanaomshambulia kibanda kwa hoja ya kununuliwa na wao wamenunuliwa. Kama hawajanunuliwa kwanini wanaibuka kumtetea. Tuwe wakweli ccm niwachafu na wezi, hawana utu na hawajali chochote zaidi yakujinufaisha wenyenyewe. Tz ipo hapa ilipo kwasababu ya wizi. Viongozi wetu ni wezi na wapo tayri kutetea wezi wenzao bila kujali athari kwa raia. RA na EL ni baadhi yao kwanini kumtetea 6. Andika kitabu tujue zaidi mwenye kujua ya RA na EL nae ayaweke hadharani na hatimaye tuweke wazi uozo wote wa serikali yetu bila kumwonea aibu mtu. Mafisadi wajiulize na watz tujiulize baada ya kujilimbikizia na kuwa na utajiri mkubwa Mobutu na wengineo wapo wapi! Lets make Tz a better place for next generation.
 
Haya mambo na haya majamaa yanachanganya kweli kweli. Hivi kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kulinganisha ufisadi wa Sitta na ule wa Lowassa?

Mkuu mwenzangu Kibanda sijaelewa kilichokusibu ukapiga bonge la U-turn. Tuambizane tusijegeuziana silaha sisi kwa sisi. Kweli Sitta na Mwakyembe ndiyo waliomuokoa Kikwete akawapa Uwaziri. Lakini bado Sitta hajafikia hata kiatu cha Lowassa na Jakaya kwa ufisadi.

Ndugu yangu Mpayukaji, nenda kaisome tena makala ya TUENDAKO ya Oktoba 26, 2011. Siujui huo unaoitwa ufisadi wa Sitta na wala hata kama ningeujua nisingeifanya hoja ya kuandikia kitabu. Kitabu ninachokusudia kuandika ni kuhusu unafiki wa vita ya ufisadi inayodaiwa kupiganwa na akina Sitta na Mwakyembe ambao kwa mtazamo wangu wana malengo yao binafsi na wala hawajapata kuwa makamanda wa ufisadi.

Kibanda ukiandika kitabu kuhusu uchafu wa Sitta basi nakumbushia unichapishie na changu juu ya ufisi wa Lowassa. Nadhani unakikumbuka kitabu changu cha NYUMA YA PAZIA ambacho mchapishaji wangu aligwaya kukichapisha na wengine wengi likiwemo Tanzania Daima, pamoja na kuliandikia, kukataa kuki-serialize.

Mpayukaji siujui ufisadi wa Sitta sasa sijui nitauandikaje? Kusudi langu ni kuandika tafsiri yangu ya mapambano ya ufisadi ya akina Sitta na wanafiki wengine CCM wanaojiita wapambanani ilhali wakiwa na malengo mengine
 
Inawezekana kabisa Mh Sitta sio msafi lakini kwa mwandishi wa habari/mwenyekiti wa jukwaa la wahiriri kutoa matamshi aliyotoa ni nje kabisa ya mipaka ya taaluma yake - very unethical. Kama kweli Kibanda anataarifa za ufisadi wa Sitta kwanini kama mwandishi asifanye kazi yake -aandike hizo habari? Alizipata lini hizo habari za Sitta? Pia Kibanda ana taarifa za ufisadi wa watu wengine mbali ya Sitta? Why Sitta and not others? Mimi naona kama Kibanda anatishia wanasiasa hapa, kwamba ukiwa karibu naye hata kama utafanya madudu atakaa kimya lakini mara unapokuwa upande wa pili atatoa habari zako. Na ukiangalia makala za Kibanda ni wazi utaona yuko upande gani.

Nategemea baada ya kuandika kitabu kuhusu ufisadi wa Sitta utaandika pia vitabu kwa mafisadi papa. Hapo ndio tutaona hujanunuliwa. Lakini kama ni kitabu cha Sitta peke yake tutaendelea kuamini wewe ni mwandishi uchwara.

Brother, I could not have written better!!!
 
Back
Top Bottom