Hapa tuache ngono tu na kuwa waaminifu,na hizo condom hazisaidii chochote,ni kufarijiana na kuongeza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi. Dawa ni kuacha ngono,na kuwa na mpenzi mmoja ila mwaminifu na hii ni kutokana na sala.
Yes kuwa mwaminifu ndiyo njia pekee lakini hebu tuende mbele kidogo utakuwaje mwaminifu? yaana ni kufumba na kufumbua tu umekuwa mwaminifu! hapana ni lazima kuwe na nguvu fulani inayokufanya uwe mwaminifu,, ni lazima tuamini kuwa ipo nguvu kuu iliyo juu yetu (Mungu) ambayo hata ukiwa peke yako chumbani inakuona,, unayowaza anayajua,, na unalotaka kutenda analijua,, ujanja unaotaka kuufanya kusaini mkataba wa 10% anauona,, nk
vinginevyo watu wa Mungu uaminifu hauwezi kuja hivi hivi kwa kuamua mimi leo niwe mwaminifu. Uaminifu lazima uwe na base si kitu cha mchezo.
Tukijiuliza mbona Lowasa, Mkapa, Rostam, Chenge na wengine wanaenda kanisani au msikitini lakini hawana uaminifu? jawabu ni kuwa kanisani au msikitini si sehemu ya hatua moja ya kuutafuta uaminifu na si ndiyo umefikia uaminifu.
Ni lazima kuamini ya kuwa yupo Mungu anakuona,, anachukia matendo mabaya,, lasivyo uaminifu kwa mpenzi mmoja utausikia tu.
Ukisoma ufunuo wa Yohana utakundua ya kuwa siku hizo zinakuja nazo zaja tauni itaruhusiwa duniani (Tauni ni magonjwa yasiyo na tiba na hata ikipatikana inakuwa tayari tauni nyingine inaingia).
Tweni Waaminifu na tuwe na base ya uaminifu wetu hii itatusaidia siyo tu kupambana na ukimwi bali hata Ufisadi, Rushwa, uchoyo, ujambazi utaisha.