Abood Jumbe hali tete, alazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573

RAIS mstaafu wa awamu ya pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Abood Jumbe Mwinyi (94), yupo hoi baada ya kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akisumbuliwa na maradhi ya moyo.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Muhimbili, Doris Ishenga, alisema Jumbe alipokewa hospitalini hapo tangu Oktoba 12, mwaka huu.

Amelazwa katika Taasisi ya Moyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.Alisema kwa mujibu wa taarifa za madaktari za Kitengo cha Moyo hospitalini hapo, baada ya kumfanyia uchunguzi wamebaini Jumbe anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo hali inayobabishwa na kuwa na umri mkubwa.

"Ni kweli Alhaj Jumbe alifikishwa hapa Muhimbili tangu Jumamosi iliyopita na amelazwa katika wodi ya moyo akisumbuliwa na maradhi ya moyo.
"Unajua ugonjwa huu unawapata zaidi watu wenye umri mkubwa, madaktari wamesema hali yake si mbaya na wala si nzuri sana," alisema.
Jumbe alikuwa Rais wa Zanzibar kuanzia mwaka 1972 hadi 1984 akishika nafasi hiyo baada ya kuuawa kwa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, marehemu Abeid Aman Karume Septemba 5, 1972.

Alijiuzulu mwaka 1984 baada ya kutokea mfarakano wa kisiasa kati yake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na kile kinachoelezwa kuwa na msimamo wa kutaka mfumo wa Serikali tatu ili Zanzibar iwe na mamlaka yake kamili.

Baada ya kutoa msimamo huo, Jumbe alipata upinzani ndani ya Serikali na chama chake na kutakiwa ajiuzulu urais wa Zanzibar. Baada ya uamuzi kutolewa kwenye vikao vya juu vya CCM, Jumbe aliachia nafasi hiyo ambayo ilichukuliwa na Ali Hassan Mwinyi mwaka 1984, ambaye baada ya mwaka mmoja alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Chanzo:Mtanzania
 
Miaka 90 plus si mchezo. Hata ukisoma vitabu vitakatifu amepitiliza umri wa kuwepo Duniani. Hata hivyo tumuombee kwa Mwenyezi Mungu amponye maradhi yake
 
Mwenyezi Mungu amjalie maisha marefu ili ashuhudie kile alichokiamini kwa wazanzibar kwani kinakaribia.
 
ccm msije mkawa mnaendeleza kolimbalism baada ya nchi kuwashinda
 
RAIS mstaafu wa awamu ya pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Abood Jumbe Mwinyi (94), yupo hoi baada ya kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akisumbuliwa na maradhi ya moyo.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Muhimbili, Doris Ishenga, alisema Jumbe alipokewa hospitalini hapo tangu Oktoba 12, mwaka huu.

Amelazwa katika Taasisi ya Moyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.Alisema kwa mujibu wa taarifa za madaktari za Kitengo cha Moyo hospitalini hapo, baada ya kumfanyia uchunguzi wamebaini Jumbe anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo hali inayobabishwa na kuwa na umri mkubwa.

"Ni kweli Alhaj Jumbe alifikishwa hapa Muhimbili tangu Jumamosi iliyopita na amelazwa katika wodi ya moyo akisumbuliwa na maradhi ya moyo.
"Unajua ugonjwa huu unawapata zaidi watu wenye umri mkubwa, madaktari wamesema hali yake si mbaya na wala si nzuri sana," alisema.
Jumbe alikuwa Rais wa Zanzibar kuanzia mwaka 1972 hadi 1984 akishika nafasi hiyo baada ya kuuawa kwa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, marehemu Abeid Aman Karume Septemba 5, 1972.

Alijiuzulu mwaka 1984 baada ya kutokea mfarakano wa kisiasa kati yake na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na kile kinachoelezwa kuwa na msimamo wa kutaka mfumo wa Serikali tatu ili Zanzibar iwe na mamlaka yake kamili.

Baada ya kutoa msimamo huo, Jumbe alipata upinzani ndani ya Serikali na chama chake na kutakiwa ajiuzulu urais wa Zanzibar. Baada ya uamuzi kutolewa kwenye vikao vya juu vya CCM, Jumbe aliachia nafasi hiyo ambayo ilichukuliwa na Ali Hassan Mwinyi mwaka 1984, ambaye baada ya mwaka mmoja alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Wewe Ulitaka Aishi Milele? Amechatufanyia Sana Kazi WADANGANYIKA ( Watanzania ) Hivyo Mwenyezi Mungu Akitaka Kumchukua Akampumzishe Ni Kheri Pia Kuliko Kumwacha Mzee Wa Watu ktk PASUA Kichwa Yetu Ya UKAWA na TANZANIA KWANZA Na Upuuzi Mwingine Uliopo.
 
Mkuu, ni lini Abood Jumbe alitoa maoni yake kuhusu muundo wa serikali?

Kama hujui hata hili la Jumbe basi huwa nakuonea tu tunapo elekezana utata wa Muungano wetu!

Rais Jumbe
Jaji Mkuu Dourando
Jaji Mkuu Othman
Maalim Seif
Rashid Ahmad
Machano Khamis Machano
Jaji Mbwelezeni
Juma Duni Halj
Abubakr Khamis
NK
Hawa wote walitimuliwa baada ya kudai ZNZ yenye mamlaka kamili
 
Back
Top Bottom