Abood Bus Service this is too much!

Jotojiwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2012
Posts
334
Reaction score
130
Ndugu wanajamii nimepatwa na jambo la kuumiza sana na naamini tupo wengi wahanga wa kuibiwa katika hizi bus za abood, nasema hivi kwakulingana na wingi wa taarifa ambazo police wamekua wakipokea kutoka kwa abiria wa mabasi hayo.

Binafsi nimeibiwa begi ktk basi hilo lililo kua na vyeti vyangu vyote toka shule ya msingi hadi chuo kikuu, na vinginevyo ikiwepo laptop na simu.

Ombi: Kwa mwanajamii yeyote atakae weza kuona vyeti popote naomba tuwasiliane kwa hii namba 0752172710

Angalizo: ukipakia haya mabasi usiweke begi chini ya miguu yako au juu ya keria ni bora uweke ktk boot nje au upakate.

Hofu: je ni kweli abood service wameshindwa kudhibiti hii hali?, na vipi kuhusu police pia wao hawana mbinu za kudhibiti uhalifu wa aina hii?
Na je ushirika wa police na wamiliki pamoja na police jamii hawafui dafu pia kwa wezi hawa?

Tafadhali naombeni mawazo yenu ndugu Watanzania wenzangu.
 
Pole sana ndugu ila ungejaribu kuweka details za vyeti kama vile majina, shule ama chuo pamoja na namba za vyeti.
 
Pole sana jamaa!

Huwa mara nyingi kwenye tiketi au kwenye basi huandika "Mizigo ya ndani si dhamana yao" abiria mwenyewe ndiye unapaswa kuwa makini na mzigo wa ndani coz si konda wala dereva anayeweza kukariri hili begi ni la huyu au yule!

Ndiyo maana huwa napenda kusafiri na mabasi yasiyosima simama njiani kushusha na kupakia abiria coz inakuwa ngumu kuangalia kwa umakini mali zako!

Kwa wasafiri wa Mbeya-Dar watakuwa na ushahidi watu wanavyolizwa kwenye vituo vya Morogoro, Iringa na Mafinga
 
Kuna jamaa yangu nae kaibiwa begi lenye laptop mwezi uliopita kwny abood hyo hyo!
 
Abood najua ni moro dar au wana route nyingine zaidi ya hiyo?.Je wewe umeibiwa kwenye route gani
 
Kuna jamaa yangu nae kaibiwa begi lenye laptop mwezi uliopita kwny abood hyo hyo!


Pole kwa mhanga, kwa tahadhari tu, Abood za sasa si zile za nyakati za nyuma, siku hizi zipo kiholela zaidi na njaa njaa za watendaji wake ndizo zinawafikisha abiria wengi kwenye hasara

Ule wizi wa mle kwenye yale mabasi ni chanel ya watu wengi tangia unapoingia kwa bus, na mara nyingi hufanyika kati ya Dsm na Chalinze au Morogoro na Chalinze, moja ya mbinu itumiwayo ni kuzidisha abiria na wakati mwingine ni pale wanaposhusha abiria waliozidi ili bus lipite kwenye mizani au mnapochepushwa mchimbe dawa ukifuatilia kwa makini utabaini baadhi ya wanaoshuka pale mizani au kuchimba dawa huwa hawarudi

Kwa ufupi wizi ule una wahusika wengi, nadhani mwenye kampuni ndiye wakushauriwa adhibiti mienendo ya wasimamizi wa hayo mabus vinginevyo vilio vya wizi vilianza kitambo sana

Ushauri wangu ni kuwa mizigo yenye vitu sensitive kama vyeti laptops etc ni vema kuipakata

Abood anatakiwa kuwa karibu sana na wateja wake kwa kusikiliza malalamiko yao na kufanyia kazi changamoto zote kuliko ilivyo sasa, baadhi ya watumishi wake wanahusika na yanayotokea isipokuwa wanalindana kwa sababu wanazozijua wao

Kuna sababu gani kwa madereva kuzidisha abiria kiasi cha abiria kushindwa kuona kinachoendelea kwenye carrier za ndani?

Kuna sababu gani kupakia au kuzidisha abiria halafu wanashukia Mikese, Bwawani, Mdaula na Chalinze? Au Kiluvya, Mailimoja, Mlandizi na Chalize
 
Abood najua ni moro dar au wana route nyingine zaidi ya hiyo?.Je wewe umeibiwa kwenye route gani

Abood mbali ya route ya Dar- Moro, pia ana route ya Iringa Dar, Mbeya Dar na Tunduma Dar.

Kwa taarifa tu Gari zake za Mbeya na Tunduma ndio zinazoongoza kwa kukimbia njia hizo.

Hilo la wizi wa mizigo ya ndani kuibiwa naona mara nyingi baadhi ya abiria wenzetu sio waaminifu, nilishawahi kushuhudia abiria akishuka na mzigo sio wake, kwa bahati nzuri mwenye begi akastuka lakini jamaa asingestuka ndio ingekuwa imekula kwake
 
Ngoja hii kitu ntaifanyia utafiti. Ntakula ndizi mbivu halafu najaza maganda kwenye begi la laptop! Nikiingia naliweka kwenye carrier ya ndani halafu najifanya sina habari wakati akili yangu yote ipo hapo....akilichomoa begi namuacha alichukue hadi afike nalo mlangoni. Namrukia kung-fu kama za bruce lee....kudadadeeeeki zao!
 

Pole sana.
Waamininifu TZ ni wachache sana, na wengi ni majizi. We angalia tu mijizi ya maofisini, serikalini na kwenye vyama vya siasa. Wakishindwa kukuibia watakutapeli. Na kwa mabasi ya Abood hakuna cha kufanya kwa sasa, ni mabsi ya Mbunge anayependwa sana Morogoro mjini.

Always Keep your vigil!
 

ukipakia usiku utaona mambo yalivyo, kwanza dereva utamkuta viroba, alafu hakuna utingo na taa haziwashwi hadi watu wanapokua wamekusanyika pale mlangoni. Kuna linanijia kua lipo kundi fulan wanafanya hii kazi.
 
Shit!!!!!mbona ni kama umetumwa kuharibu biz za watu mkuu?nimetumia abood kwa miaka11 sasa,never hear that sound.Alafu unaibiwaje wakati beg ipo ndani kwenye kelia na unaiona?pil yale mabasi huwa hayana konda wala utingo,pili huwa wanapanda wale wauza korosho na juice ambao si rahisi kuiba,wewe vp uibiwe?
 
Laptop na briefcase za watu zimeibiwa Sana.Nakumbuka kuna Mzee alilizwa briefcase lenye milioni moja na jamaa alishukia ubena.kufika Mikese Mzee akawa halioni briefcase
 

Pandeni basi zuri BM couch la mtanzania halisi.achaneni na mwarabu huyo
 

unakosea mzee mimi sipo kuwaharibia chochote na niwazi mimi siezi kufanya hivyo, chamsingi nenda kituo cha police pale ubungo uombe kujua hili swala naloongelea utapata ukweli. Nachofanya nikuimarisha huduma zao na kuwafungua watu macho wasipatwe na kilichonipata.
 
wangekuwa wezi wanakatwa mikono haya yote yangepungua sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…